Hali ya kimaisha ya watanzania inatisha na ni mbaya sana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Tangu mwaka 2015 alipoingia madarakani Rais Magufuli, hali ya mambo ilianza kubadilika, wengi wakasifu hatua zake za awali na kujengewa hisia za mema. Lakini miaka mitatu baadae utawala huu umekua shimo la mauti ya wengi, umekua hatari kwa kila jambo ambalo awali lilikua jema na halikua na kuhofiwa na watu sana.

Mbali na ukandamizaji wa demokrasia, magufuli amegeuka na kua tishio la maisha ya kila siku ya Mtanzania mmoja badala ya mwingine.

Watanzania wengi wapo katika hali ya umasikini mkubwa, hali ya ukata mifukoni mwao, hawawezi tena kulipa ada za watoto wao kwa wakati, hawawezi kumudu kodi za malazi. Na wanashindwa kumudu hata huduma za msingi kama afya. Jamani! Watanzania wengi wana umia kwa njaa, familia nyingi ziliweza kumudu milo mitatu lakini sasa wanajikuta wanakula mlo mmoja na kushindwa kumudu milo mingine. Watu wanafamilia zao wanashindia uji na watoto zao, ili tu wasife.

Maana hawawezi tena kumudu kununua chakula chao kila siku.
Wakulima wanalia bei za mazao yao zimekua ovyo wanapata hasara kuliko kawaida. Wanashindwa kuendesha maisha yao kama zamani, haya yote ni kutokana na uongozi mbovu ma Magufuli na kundi lake.
Tunadalili ya kua na ongezeko na watoto wenye utapia mlo siku za usoni, kwa mwenendo huu wa ukandamizaji unaofanywa na Rais wa nchi hii yetu.

Ajira zimezuiwa sana, na walioajiriwa wengi mpaka sasa hawaanza kulipwa mishahara yao tangu mwezi wa 7, huu ni unyonyaji mkubwa unaofanywa na serikali ya CCM. Serikali isiyojali hali za Watanzania katika uhalisia zaidi zaidi wanajinadi kinafiki kwa maslahi yao na chama chao.

Tumechoshwa na hali ngumu ya maisha, unyanyasaji unaofanywa na serikali wa kuyageuza maisha yetu kua magumu inatisha sana.
Kwinyara
 
Tangu mwaka 2015 alipoingia madarakani Rais Magufuli, hali ya mambo ilianza kubadilika, wengi wakasifu hatua zake za awali na kujengewa hisia za mema. Lakini miaka mitatu baadae utawala huu umekua shimo la mauti ya wengi, umekua hatari kwa kila jambo ambalo awali lilikua jema na halikua na kuhofiwa na watu sana.

Mbali na ukandamizaji wa demokrasia, magufuli amegeuka na kua tishio la maisha ya kila siku ya Mtanzania mmoja badala ya mwingine.

Tuuongee ukweli wa hali bila unafiki wowote, wengi wa hata hao wanaounga mkono juhudi ni wanafiki watupu wote hao ni ugumu wa maisha unaosambaa kwa kasi nchini unawakimbiza katika kutazama fungu jema la matumbo yao.
Watanzania wengi wapo katika hali ya umasikini mkubwa, hali ya ukata mifukoni mwao, hawawezi tena kulipa ada za watoto wao kwa wakati, hawawezi kumudu kodi za malazi. Na wanashindwa kumudu hata huduma za msingi kama afya. Jamani! Watanzania wengi wana umia kwa njaa, familia nyingi ziliweza kumudu milo mitatu lakini sasa wanajikuta wanakula mlo mmoja na kushindwa kumudu milo mingine. Watu wanafamilia zao wanashindia uji na watoto zao, ili tu wasife. Maana hawawezi tena kumudu kununua chakula chao kila siku.
Wakulima wanalia bei za mazao yao zimekua ovyo wanapata hasara kuliko kawaida. Wanashindwa kuendesha maisha yao kama zamani, haya yote ni kutokana na uongozi mbovu ma Magufuli na kundi lake.
Tunadalili ya kua na ongezeko na watoto wenye utapia mlo siku za usoni, kwa mwenendo huu wa ukandamizaji unaofanywa na Rais wa nchi hii yetu.
Ajira zimezuiwa sana, na walioajiriwa wengi mpaka sasa hawaanza kulipwa mishahara yao tangu mwezi wa 7, huu ni unyonyaji mkubwa unaofanywa na serikali ya CCM. Serikali isiyojali hali za Watanzania katika uhalisia zaidi zaidi wanajinadi kinafiki kwa maslahi yao na chama chao.
Tumechoshwa na hali ngumu ya maisha, unyanyasaji unaofanywa na serikali wa kuyageuza maisha yetu kua magumu inatisha sana.
Kwinyara
Kuna wengi tuliofanya biashara na serikali tumefilisikka sababu magu hataki kilipa madeni ya ndani pesa yote ananunulia madege na sgr tu huku tra wakitukaba koo
 
Zamani hali ilikuwa nzuri?
Nyie si wale ambao "hata wananchi wakila nyasi" bado mtabakia na bajeti zenu za mishahara minono, bia na nyama kwenye friji kila wiki? Huwezi kuona wala hujui kinachoendelea. Zaidi zaidi labda uamkie kwenye ac yako hapo kuendelea kutumbua kodi zetu huku ukitype upuuzi humu jf ukisubiri lunch na muda kutoka.
 
Hali mbaya kweli kama ulizoea pesa ya bure, kama ulikuwa unatafuta tangu awali, awamu ya JPM ni furaha muda wote. Inuka toka kwenye vijiwe nenda kafanye kazi, ujiajiri. Tuache kulalama, tukatende kazi.
 
Back
Top Bottom