Hali ya huduma ya Maji Safi Dodoma

Hali ya huduma ya Maji Safi Dodoma

Emmanuel_DWSS

Verified User
Joined
May 30, 2023
Posts
2
Reaction score
11
Hali ya huduma ya Maji safi Dodoma.

Kufuatia ongezeko la watu katika jiji la Dodoma lililosababishwa na Serikali kuhamia Dodoma, mahitaji ya maji yaliongezeka kutoka Lita Milion 44 kwa siku mwaka 2017 hadi Lita Milion 133 kwa siku mwaka 2023. Vyanzo vyote vya maji vilivyopo Dodoma vina uwezo wa kuzalisha Lita Milion 67.8 kwa siku (takribani 50% ya mahitaji kwa kwa siku).

Ili kukabiriana na ongezeko hili, Serikali Ilitenga kiasi cha 7.8bn kwaajili ya hatua za muda mfupi za kupunguza tatizo hili. Hatua hizo ni uchimbaji wa Visima virefu na kuviendeleza katika maeneo ya Mzakwe, Ihumwa, Nala, Ntyuka Chimalaa, Bahi, Kongwa na Chamwino.

Hatua hizi zimetupa matokea yafuatayo:-

1.0 DUWASA imeongeza Uzalishaji kutoka Lita Milion 61.5 hadi 67.8 kwa siku Mjini Dodoma.

2.0 Bahi imeongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 37 hadi 95.

3.0 Chamwino imeongeza upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 42 hadi 87.

4.0 Kongwa imeongeza upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 44 hadi 88.

Aidha Serikali imetenga fedha kiasi cha Tsh. 23.8 bn kwaajili ya kuendelea kutekeleza kazi za muda mfupi za kuendelea kupunguza uhaba wa maji katika jiji la Dodoma hususani katika maeneno ya NZUGUNI, BIHAWANA na ZUZU.

Hatua za muda Muda wa kati na Muda mrefu
1.0 Ujenzi wa Bwawa la Farkwa.
- litatoa maji lita Milion 130 kwa siku
-Fedha za kuaza kujenga Bwawa na Mtambo wa kutibu maji zimepatikana - Dola Mil. 125.3 (phase 1). Kwasasa tayari wahandisi washauri (consultant) kwa ajili ya design review, catchment protection na panel of experts wamepatikana.
-Mradi utachukuwa muda wa miaka kati ya 5-7.

2.0 Mradi wa kuchukuwa maji kotoka Ziwa Victoria.
- Mradi huu upo katika hatua ya kumpata Mshauri (Consultant)

Hatua za Dharula
1.0 Mradi wa kuchukuwa maji kutoka katika Bwawa la Mtera.
- Mradi unalenga kuchukuwa maji lita Mil. 130 kwa siku
-Una umbali wa mita 131 kutoka Dodoma mjini.
- Unaweza kukamilisha ndani ya miaka mitatu
-Gharama yake ni Dola Mil 170.
-Mhandisi Mshauri (Consultant) yupo kazini na na anategemea kuwasilisha taarifa yake ya mwisho mwezi Juni tarehe 10 2023.

Tutaendelea kuwahabarisha hatua mbalimbali kadri zinavyotokea na kutekelezwa.

Asante
Eng. Emmanuel Mwakabole
DWSS-DUWASA
DODOMA
 
Tumekupata mkuu!Acha siasa tekeleza.
 
Rekebisha kwenye umbali wa Dodoma na bwawa la mtera.
 
Mipango yote ni ya muda mrefu na mingi ipo kwenye drawing boards, kwa sasa msitegemee uwekezaji wowote mkubwa wala ofisi za mabalozi kuhamia.
NB-: Namkumbuka yule Waziri wa nishati wa Kikwete na hekaya zake za megawati? 😁
 
Vumbi /Maji / Narudi/Upepo sura lazima ifubae ka Hali ya hewa haikupendi

Kila mkazi wa dodoma akiotesha angalau miti 10 kwa mwaka itaibadilisha mandhari ya dodoma
 
Sawa kazi nzuri pambaneni. Maji ya ziwa Victoria mpango upoje?
 
Maji Dodoma yatakaa sawa,kuwa mpole!
Umeona pumba zilizoandikwa hapo yani bwawa litachukua miaka mitano hadi saba maana yake hii tabu iliyopo sasa hivi itaendelea kuwepo hadi 2030+ maana halijaanza kujengwa bado.
 
Vumbi /Maji / Narudi/Upepo sura lazima ifubae ka Hali ya hewa haikupendi

Kila mkazi wa dodoma akiotesha angalau miti 10 kwa mwaka itaibadilisha mandhari ya dodoma
Kupauka ni asili ya mtu tu.
Singida kuna upepo na mavumbi kama hapa ila watu ni wazuri sana jinsia zote hata kama hana light skin

Nenda Kondoa uone kulivyo pauka ila watu ni wasafi, wazuri kama dhahabu
Kama ni mbovu utabaki kuwa mbovu tu
 
Mipango yote ni ya muda mrefu na mingi ipo kwenye drawing boards, kwa sasa msitegemee uwekezaji wowote mkubwa wala ofisi za mabalozi kuhamia.
NB-: Namkumbuka yule Waziri wa nishati wa Kikwete na hekaya zake za megawati? 😁
Na wanataka kuchukua maji mtera bwawa linalokauka kwa kuishiwa maji kila mwaka hadi linashindwa kuzalisha umeme 😝😝😝

Kuna sehemu lile bwawa hukauka kabisa hadi unavuka kwa miguu yani maji ni hamnaaa
 
Bwawa limefika hadi chipogoro mbona ni chini ya hizo KM
Yeye kaandika mita 131!! Nimefanya correction kutoka hapo.
Halafu bado point ya kuchukulia maji ni pale mtera kwenye maporomoko. Chipogoro bwawa lipo ila kitaalamu huwezi weka mashine za maji maeneo yale
 
Na wanataka kuchukua maji mtera bwawa linalokauka kwa kuishiwa maji kila mwaka hadi linashindwa kuzalisha umeme 😝😝😝

Kuna sehemu lile bwawa hukauka kabisa hadi unavuka kwa miguu yani maji ni hamnaaa
Maji kwa kawaida watachukua baada ya shuguki za kuzalisha umeme! Ni kweli mtera kuna kipindi inapungukiwa kabisa maji ! Hilo sijui watafanyaje
 
Yule jamaa alikurupuka kama kawaida yake, aliona wenzake wanaokwenda mdogo mdogo ni wajinga.

Tumelikoroga ndiyo tulinywe sasa, lakininkwamkuwa watekelezajinwoye inabidinwawepo Dodoma, tatizo hilo tulichukukie kuwa limekwisha, litatatuliwa kwa haraka sana kuliko mkoa mwengine wowote.
 
Yeye kaandika mita 131!! Nimefanya correction kutoka hapo.
Halafu bado point ya kuchukulia maji ni pale mtera kwenye maporomoko. Chipogoro bwawa lipo ila kitaalamu huwezi weka mashine za maji maeneo yale
Na kwenye mashamba ya miwa watapeleka nini?
Nimebahatika kufika mgodini mara kibao sana hata last week nilikuwa mule ndani hiyo project yao ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom