Hali ya Dar es Salaam kwa sasa

Muhubiri

Senior Member
Mar 11, 2012
140
120
Habari wakuu!
Naomba awali ya yote nitamke ya kuwa sina maslahi binafsi na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.
Binafsi, nachukua hatua hii kuupongeza uongozi wa mkoa wa Dar, kwa jinsi mabadiliko na maendeleo yanayoonekana.
Mathalani:

1.Huku kwetu TABATA tatizo la maji linaanza kuwa ni historia, kwa kweli zamani ilikuwa kila siku naacha 4,000tsh ya maji ila leo hii, nalipa bili ya maji mwezi mzima haizidi 8,000tsh.

2.BARABARA barabara za huku kuwa uswahilini kwetu pamoja ya kuwa nyingi ni vumbi ila wanajitahidi kuzirekebisha, mf.Segerea kupitia Tabata migombani, jeshini hadi external, ibawafaa sana, zaidi ya yote, route zimekuwa za kutosha kurahisisha usafiri

3.MIGOGORO YA ARDHI
Binafsi nina "vimaeneo" sehemu tofauti tofauti, kuna sehemu nilikuwa nimeanza kuzikatia tamaa, ila sasa RC kaziweka sawa, ofcoz hapa mh Lukuvi huwezi mnyima credi

MWISHO: Ni kweli namba tunazisoma ila kiukweli kuna vitu VIZURI VINGI vinatendeka.

HONGERA UONGOZI WA DAR
 
dar asilimia kubwa imekamatwa na wapinzani japo serekale huwa inawaletea figisu washindwe kufanya kzi zao vyema utasikia hapi sijui kamakamata boniface akikagua maendeleo kimara sisi tunataka maendeleo awe ccm chauma na kuendelea tunachotaka ni maendeleo
 
Wakishirikiana tutaenda kwa kasi zaidi, vyama na uchama ukae pembeni, maslahi ya wananchi kwanza
 
Wakishirikiana tutaenda kwa kasi zaidi, vyama na uchama ukae pembeni, maslahi ya wananchi kwanza
kabisa jambo jema ni kushirikiana wafanyekazi begakwa bega maramoja tutaondoka hapa tulipo ................. sijui kwanini huwa hawawazi hivi
 
Back
Top Bottom