jaykiwele
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 552
- 414
Habari wapendwa humu JF, Mimi nina miaka 28 chuo nimepita nikapata degree ya masuala ya computer ila kama mnavyojua wimbi la kukosa ajira limekuwa tatizo kubwa kwasasa ndio maana nimeamua kuja kwenu naamini humu Kuna wadau wa Kila sekta ambao kwa namna noja au nyingine wanaweza kunipa muongozo au ushauri sahihi baada ya kibarua changu cha kwanza muajiri kuamua kupunguza wafanyakazi na kwangu imetokea ghafla kwani imekuja kipindi namuuguza Bibi yangu ambaye anasumbuliwa na maradhi ya uzeen mda mrefu sasa nikajikuta kasalio kangu kamepungua sana hivyo kwasasa nataman kupata kazi yoyote ili niweze kujikimu kimaisha na kutimiza ndoto zangu zingine. Tafadhali wapendwa msaada wenu.