Hali ni mbaya Dar es Salaam!


juve2012

juve2012

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
3,337
Points
1,250
Age
38
juve2012

juve2012

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
3,337 1,250
Ni saa kumi jioni, Natoka zangu taratibu kuelekea mazoezini. Inanibidi nipande daladala na kusafiri umbali wa kilomita tano kufika uwanjani maana huku kwetu hakuna viwanja vya michezo. Hata shule zilizopo karibu hazina viwanja.

Maeneo ya wazi yote yamejengwa nyumba na mabanda ya biashara.wakati nakaribia kituoni,nakutana na jamaa yangu mmoja akiwa anatoka mjini. Tunasalimiana, namuuliza "vipi hujapata tu?"ananijibu"ah,mie naona sasa niende mkoa tu,huu mji wenu umenishinda,watu wanapeana kazi kiukoo bwana!". Namtazama usoni, ingawa anaongea kwa utani,lakini anaonekana kumaanisha anachokiongea. Namuonea huruma jamaa huyu. Ana miaka miwili amemaliza UDSM shahada ya kwanza na bado anatafuta kazi!Tunaagana,naondoka.

Njiani nakutana na foleni kubwa ya magari isiyotembea, kuna ujenzi unaendelea na hivyo gari zote zinatumia njia moja.Wamekutana madereva wabishi,kila mtu anataka kuwa wa kwanza kupita,wamezibiana njia gari haziendi.Nafika kituoni nakuta hamna daladala maana gari zote zipo pale kwenye foleni isiyotembea! Ni sie tunaotambua umuhimu wa mazoezi ndio bado tunadiriki kupanda daladala kutafuta viwanja!wengi walishaacha tayari.

Siku hizi wakazi wa dsm wanafanya safari muhimu saaana tu,kama vile kwenda ofisini,hospitali,kununua mahitaji basi!Kwa nini,hali ni mbaya.Dsm hii ya leo sio ile ya mwaka 1986 wakati napanda UDA kwenda shule.Hii ni DSM nyingine kabisa! Joto kali na hili la mwaka huu hasa kuanzia mwezi October sijawahi kuliona kwa muda mrefu sana. Yaani ikishafika saa saba mchana unatamani tu jioni ifike uondokane na jehanam hii ya joto kali! Hatujaona mvua mwaka huu za maana. Tunasikia tu kutoka mikoani. Hali ya maisha ni juu.Hicho kilichopo watu hupigania hicho hicho na ndio sababu hupeana kwa kujuana.

Usipokuwa na mtandao utaiona dar chungu kama ndugu yangu huyu.Hali ya usafiri ni mbaya,miundombinu mingi imefumuliwa kwa ajili ya ukarabati,na hivyo dar ya sasa hutakiwi kuwa na haraka kabisa! Maadili ya jamii iliyopo yameporomoka vibaya. Hakuna upendo ule wa zamani. Kuna maeneo ukiibiwa utaita mwizii na watu watakutazama tu kama vile hawakusikii, huduma za kijamii ndio usiseme. Kila mahali foleni si hospitali,si maofisini. Sina haja ya kuzungumzia maji na umeme.Sina haja ya kuzungumzia kodi za nyumba! Mnaelewa vizuri sana balaa lake hapa dar.

Nawatazama watoto wetu wakigombania daladala kwenda shule,najiuliza ni mambo mangapi wanakutana nayo on the way to school and back home?!

Naikumbuka Dar ile ya mwaka 86 wakati nikiwa nyumbani Upanga,nikiwa na marafiki zangu tunacheza mpira hapo nje ya nyumba,Mzee anatunyamazisha ili asikie tangazo la kifo cha Samora Machel,halafu naitazama dar hii ya sasa,najiuliza,hivi hii bado ni bandari ya salama kweli?
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,167
Points
2,000
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,167 2,000
Aah kumbe tabu yote ni kwa kuwa barabara zinatengenezwa?
 
H

Hemed Maronda

Senior Member
Joined
Oct 27, 2010
Messages
138
Points
0
H

Hemed Maronda

Senior Member
Joined Oct 27, 2010
138 0
Dar Es Salaam siyo sehemu salama ya kuishi wala siyo sehemu salama ya kufanyia kazi maana kila siku kama ni Baba wewe ndiyo unakuwa wa mwisho kurudi nyumbani na wakwanza kuondoka nyumbani,watoto wako hakuoni unaporudi maana unarudi saa 5 usiku wao wameshakula na kulala na unaondoka saa 11 alfajiri wao wakiwa bado vitandani wanaendelea kulala,hiyo ndiyo Dar Es Salaam ya sasa.

Tatizo kubwa ni kuwa miundo mbinu iliyopo haikidhi idadi ya watu waliopa Dar pia kuna imani ambayo siyo rasmi kuwa endapo mtu unahitaji kufanikiwa basi ni lazima uishi Dar Es Salaam.

Mimi binafsi siamini jambo hili kwa kuwa wapo watu wamefanikiwa sana tu wakiwa nje ya Dar. Wakazi wa Dar wao ndiyo wanaona kuwa hapo walipo ndiyo Tanzania na huku waliko wengine siyo Tanzania na ndiyo maana ukiwa Dar na mara kaja rafiki yako kwa mfano katoka Mbeya utamtambulisha kwa marafiki zako wengine kuwa huyo rafiki yako katoka Mkoa hata pale Ubungo Bus Terminal panafahamika kama Stendi ya Mkoa, sasa ndugu zangu msilalamike sana maisha mabivu mnayapenda wenyewe kwani huku vijijini kwenu mmefukuzwa?
 
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
10,316
Points
2,000
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
10,316 2,000
aha embu acha kuumiza kichwa pungueni jijini mrudi makwenu...tatizo kili mtu anataka kuishi dsm
 
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,649
Points
1,225
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,649 1,225
Shida mnazitaka wenyewe kwa kuikumbatia ccm!!!!!
 
Mkereketwa_Huyu

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Messages
6,644
Points
2,000
Mkereketwa_Huyu

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2011
6,644 2,000
Matatizo haya yote ni ujinga wa serikali wa kutaka kila kitu muhimu kuwa Dar Es Salaam. Sote twajuwa, Dar ni mji mdogo sana na miundo mbinu iliyopo hapa haikidhi mahitaji ya jiji na wananchi wake. Serikali inabidi ifanye utafiti wa kuendeleza mikoa na miji yake ili watu wasirundikane tu hapa Dar. Moja ya mfano ni kurudisha gesi Mtwara ili wananchi wa huko wapate kujiajiri kwa biashara ndogo ndogo zitakazotokana na mzunguko wa pesa. Mifano iko mingi tu ila tatizo ni utawala mbovu wa CCM unaojali matumbo ya majambazi wachache waliopo madarakani.
 
Mkereketwa_Huyu

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Messages
6,644
Points
2,000
Mkereketwa_Huyu

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2011
6,644 2,000
CCM hata iwe madarakani miaka 100 tatizo la Tanzania kutokuwa na maendeleo litabaki pale pale na visingizo vya kutokuwa na maji, umeme vitakuwa vile vile.
 
Lole Gwakisa

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Messages
4,100
Points
2,000
Lole Gwakisa

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2008
4,100 2,000
Matatizo haya yote ni ujinga wa serikali wa kutaka kila kitu muhimu kuwa Dar Es Salaam. Sote twajuwa, Dar ni mji mdogo sana na miundo mbinu iliyopo hapa haikidhi mahitaji ya jiji na wananchi wake. Serikali inabidi ifanye utafiti wa kuendeleza mikoa na miji yake ili watu wasirundikane tu hapa Dar. Moja ya mfano ni kurudisha gesi Mtwara ili wananchi wa huko wapate kujiajiri kwa biashara ndogo ndogo zitakazotokana na mzunguko wa pesa. Mifano iko mingi tu ila tatizo ni utawala mbovu wa CCM unaojali matumbo ya majambazi wachache waliopo madarakani.
Hata London na Bombay zilijengwa na CCM.
 
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,619
Points
1,225
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,619 1,225
Chapeni kwazi, mzoee kuridhika na hali mliyonayo. Vinginevyo mtakuwa wezi sasa hivi.
 
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Messages
4,435
Points
2,000
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2008
4,435 2,000
2015 Chagua CCM tena, Maisha bora kwa Mafisadi
Shida mnazitaka wenyewe kwa kuikumbatia ccm!!!!!
Tatizo letu Watanzania tunalalamika na ikifika kipindi cha uchaguzi tukipewa khanga, Tshirt, Kofia na Sh. 1,000/= tu inatosha kuwachagua mafisadi kisha tunateseka miaka mitano.

Kwa hali ilivyo sasa chini ya uongozi wa awamu ya nne, kwa hakika Rais ajaye atakuta nchi imebaki mafuvu matupu.

Serikali inabinafsisha kila kitu na ikifika mwaka 2015 wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu wanamalizia na kuuza IKULU.MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Messages
9,257
Points
2,000
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined May 1, 2009
9,257 2,000
watu wanajazana dar kwakua maamuzi yote makubwa yanafanyika dar mfano interview na ajira zote nzuri zina anzia dar wewe ng,a ng,ania huko bush utashangaa sisi tulio dar tunaendelea kugawana cake ya taifa
 
Mshuza2

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Messages
5,860
Points
2,000
Mshuza2

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2010
5,860 2,000
Usikonde mkuu,si ushasikia wanasema kukaa tu Dar hata kwa wale wasioenda shule tayari wanakua na elimu ya kidato cha sita? Ngoja mminyane,mbio zako ndio zitazokuokoa!
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,992
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,992 2,000
Me nikitoka zangu joburg nikifika dsm sioni tofauti na kijijini tuh,,

kuita dsm jiji na arusha au mwanza mkoani naona ni ulimbukeni tuh,yote ni mikoa,na yote ni majiji sema tu dsm ilishatangulia tokea mda mrefu,,pia kama mnaona mipango mjini haiendi mjaribu siku moja moja kutoka mkoa huu kwenda kujaribu changamoto mikoa mingine,then mkiona huko nako hakufaia zaidi ya huku mnaweza kurudi,ridhk ya mbwa iko miguuni mwake,,msitegmee tena miujiza ya ccm
 
juve2012

juve2012

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
3,337
Points
1,250
Age
38
juve2012

juve2012

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
3,337 1,250
Usikonde mkuu,si ushasikia wanasema kukaa tu Dar hata kwa wale wasioenda shule tayari wanakua na elimu ya kidato cha sita? Ngoja mminyane,mbio zako ndio zitazokuokoa!
duh!kwa hiyo ukikaa dar tu tayari wewe form six?sasa huu uform six wetu mbona hautusaidii hali ya jiji inazidi kuwa mbaya?!
 
M

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
1,422
Points
1,225
M

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
1,422 1,225
Tatizo ni siasa ndugu. mlugaluga anatoka mkoa, mara uwaziri kabaa, unafikiri atakubali ofisi zihamie mkoani? si lzm nae akabanane masaki? ndo maana Dar kila siku linakuwa jiji la hovyo, ntamsifu sana Jk akiimplement bandari ya B'moyo na EPZ zake then reli na bandari ya Tanga ili Dar isiwe unique sana. Ikulu iwe full fledged Dom ili wasemelezeaji nao walazimike kuhamia Dom
 
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Messages
1,754
Points
2,000
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2012
1,754 2,000
dharau kwa watanzania wenzako eti tu, kwa sababu hawashabikii vyama vya upinzani. haswa kile unachokipenda wewe ni makosa kudhani kuwa nchi yetu, matatizo yake yatatatuliwa na wanasiasa na si watendaji wa serikali,jiulize hapa Dar jiji lilipoongozwa kwa muda na Mh Keenja, kila mkazi wa jiji hili alijionea utendaji kazi uliotukuka, jiji letu bila kuangalia chama ,likipata watendaji wazuri linaweza kufanya mambo, makubwa kwa rasilimali zake lenyewe na kuondokana na kadhia zote ulizoziorodhesha, hakika suala la foleni za magari hapa Dar, limeachwa mikononi mwa Traffic, ambao wanahangaika kutwa huku wakimwagiwa matusi na madereva, wakati wanaita magari upande tofauti huku ,wakipongezwa upande mwingine, suala la foleni ni la watendaji wa serikali na wakazi wa hapa jijini. hivi watendaji mnapoweka yadi kubwa ya magari pale SHAURIMOYO unasaidia au unaongeza tatizo la foleni, unapojenga machinga complex maeneo yale unaonaje, ujenzi wa ofisi ya uhamiaji kule kurasini unaonaje, makao makuu ya magereza kuwa mjini unaonaje, hali ya hewa ofisi zao kuwa Banana unaonaje, unaonaje huduma nyingi za jamii zikitoka nje ya mji, mfano halmashauri zikitoka na kuwekwa nje ya mji wananchi hawatafuata huduma, TEMEKE nendeni chamazi au tuangoma.au vianzi. KINONDONI nendeni mabwepande au mlonganzila ILALA nendeni chanika au mvuti, asubuhi magari yote yaelekee nje ya mji.WAKAZI wa DAR tumshinikize MH PINDA afanye kama alivyofanya MH SUMAYE ateue watendaji bora , jiji linauwezo wa kufanya mambo makubwa saaana, tujiulize zile akaunti zilizoachwa na mabilioni ya fedha katika kila wilaya na tukataarifiwa kuwa hazitaguswa na watendaji wapya baada ya kina Keenja kukabidhi utawala mpya ziko wapi?
 

Forum statistics

Threads 1,284,377
Members 494,064
Posts 30,823,405
Top