queen of the jungle
JF-Expert Member
- Mar 17, 2017
- 228
- 429
Ndugu wenzangu maisha yanazidi kuwa magumu mtaani lakini kila ukijaribu kufanya maarifa ili uweze kusimama bado hali ni tete. Zamani mtu alikuwa akisoma basi uhakika wa ajira ulikuwepo lakini ni tofauti na sasa mtu umesoma lakini miaka miwili unatafuta ajira bila mafanikio
Ukisema ufungue kibiashara unapata misukosuko mpaka biashara ya kusimama ni zaidi ya mwaka kwanza kodi kubwa, kodi ya pango ya mwaka, hujakaa sawa service levy, ukigeuka huduma ya taka sio chini ya elfu arobaini, mara hela ya sungusungu yoote hayo ni kwenye biashara changa
Lakini cha ajabu unaweza ukarudi nyumbani nako mwenyekiti wa serikali za mitaa naye anakutaka utoe hela ya sungusungu ya chumba unachokaa,
Ombi langu kwa serikali ni iangalie namna ya kusaidia vijana waliomaliza vyuo na hawajapa ajira maana wengine wazazi wao waliuza mpaka ngombe ili wanao wasome
Kilichoniuma sasa ni kwamba biashara haziendi, mume wangu katumbuliwa yuko tuu nyumbani na yeye ameanzisha miradi ambayo inachukua muda kuanza kumlipa.
Mbali na hivyo mama yangu ni mgonjwa anatakiwa kufanyiwa operesheni, mdogo wangu yuko anahitaji msaada wa ada kapata asilimia 40, mbali na hivyo nyumba tunayokaa kodi inakaribia kuisha kiukweli nataka nijilipue niende hata Zambia au South Africa