Hali inatisha Ocean Road, hakuna dawa

Hali inatisha Ocean Road, hakuna dawa

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
ocean_road_clip.jpg


Hali ni mbaya katika Hospitali ya saratani ya Ocean Road (ORCI), Dar es Salaam kutokana na uhaba mkubwa wa dawa. Wagonjwa wengi waliolazwa katika hospitali hiyo kwa nyakati tofauti wamesema wameshuhudia wenzao kadhaa wakipoteza maisha kwa kuwa taasisi hiyo haina dawa. Mmoja wa wagonjwa aliyekuwa amelazwa kutokana na saratani ya utumbo, Miriam Obadia kutoka Geita, alikata roho mbele ya mwandishi wa habari wa gazeti hili aliyeingia katika Wodi namba 322 huku kukiwa na taarifa kwamba alikosa dawa.

Muuguzi ambaye hakutaka kutaja jina lake kutajwa gazetini, alisema mgonjwa huyo alifariki dunia kwa kukosa dawa ambazo hazipo hospitalini hapo. "Ndugu zake waliambiwa wakanunue nje lakini hadi leo hawajamletea na hapa sisi hatuna dawa anazohitaji."

Mwandishi alijaribu bila mafanikio kuwatafuta ndugu zake ambao walikuwa wameondoka kwenda kutafuta fedha za kununua dawa hizo. Mkurugenzi wa Tiba wa ORCI, Dk Diwani Msemo alithibitisha kuwapo kwa uhaba mkubwa wa dawa katika taasisi hiyo. "Hilo halina ubishi, ni kweli kuwa tuna uhaba wa dawa, ni tatizo kubwa na lipo nje ya uwezo wetu."

Akizungumza kwa tabu, mmoja wa wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Miyana Mushi, aliyelazwa katika wodi namba 321 alisema ameshindwa kupata dawa za saratani ya koo alizoandikiwa mwezi mmoja uliopita baada ya kuambiwa kuwa zimekwisha hospitalini hapo.

"Sasa hivi natapika damu na usaha, siwezi kula wala kunywa chochote kwa sababu koo linauma sana. Mwanangu amejaribu kuulizia dawa nilizoandikiwa katika maduka ya dawa lakini tumeshindwa kununua kutokana na kukosa fedha." Ili Mushi aweze kupona, anahitaji dozi nzima ambayo katika maduka ya dawa inauzwa Sh 3.5 milioni, fedha ambazo alisema hawezi kuzimudu.

Gharama za dawa

Imebainika kuwa dawa zinazotakiwa kwa ajili ya wagonjwa wengi zinapatikana kwenye maduka ya dawa lakini kikwazo ni bei. Katika baadhi ya maduka, bei ya baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa katika hospitali hiyo hazishikiki. Mathalan, tiba ya saratani ya damu kwa watoto kwa dawa iitwayo 1/M asparafinase 20,000IV ni kati ya Sh. 900,000 na milioni moja kwa dozi moja. Kwa mtoto hata kama ni wa mwaka mmoja huhitaji dozi 12 ili apone.

Dawa za bei ya chini kabisa za saratani kwa mfano, Finesteride na Menthotrexate ambazo ni za kutuliza tu maumivu zinagharimu kiasi cha Sh. 20,000 kwa dozi. Kadhalika, imebainika kuwa mbali na uhaba wa dawa, mashine ya mionzi ya ORCI pia imeharibika kutokana na kutumika zaidi ya uwezo wake. Akizungumzia suala hilo Dk Msemo alisema: "Ni kweli mashine ni mbovu. Tunasubiri mafundi kutoka Canada watakuja kuitengeneza, tunawatarajia wakati wowote."

Kauli za wagonjwa

Baadhi ya wagonjwa waliorudishwa nyumbani kwa kukosa huduma ya mionzi walisema wameambiwa watapigiwa simu pindi mashine itakapopona. "Nina saratani ya kizazi, ninatokwa damu kila siku, nimeambiwa mashine mbovu na sijui hatima yangu ni nini kwa sababu naumwa sana, tena sana... Serikali itusaidie jamani tutakufa," alisema Zuhura Kigobe, mkazi wa Nyamagana, Mwanza. Kigobe pamoja na wenzake wenye saratani za aina mbalimbali walirudishwa nyumbani tangu Agosti mwaka huu na hawajui hatima yao hadi sasa.

Takwimu kutoka ORCI zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wa aina hiyo inaongezeka kwa kasi kutoka wagonjwa 2,807 mwaka 2006 hadi 5,384 mwaka jana. Mkurugenzi wa takwimu wa ORCI, Dk Julius Mwaiselage alisema ongezeko kubwa la maradhi ya saratani linatokana na mfumo wa maisha.

Wizara ya Afya

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa dawa katika hospitali nyingi nchini lakini na kwamba Serikali inatafuta fedha... "Lakini inawabidi wasubiri kwa sababu hata Serikali nayo imepungukiwa fedha ndiyo maana hatujapeleka fedha (Bohari Kuu ya Dawa) MSD." Alisema suala la ORCI ni zito na linaitatiza Serikali kwani taasisi hiyo haina chanzo chochote cha fedha na inajiendesha kwa kuitegemea Serikali kwa asilimia 100.

"Pale wagonjwa wanatibiwa bure na tiba yao gharama ni kubwa kwa mfano mgonjwa mmoja wa saratani huweza kutibiwa kwa Sh. 2 milioni, ndiyo maana kuna changamoto kubwa katika suala hilo kwa kweli," alisema Mwamwaja. Hata hivyo, alisema kwa sasa wametoa kipaumbele kwa taasisi hiyo ili ipate mgawo mkubwa zaidi wa dawa kutokana na unyeti wa ugonjwa huo, sambamba na kufungua kanda katika baadhi ya mikoa nchini.

Chanzo: Hali inatisha Ocean Road - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Hii inaumiza Sana wakati mafisi wanachezea mabilioni ya shilingi kujiimarisha kwenye urais MSD inakosa 90 billion huu ni unyama.
 
viongozi wa nchi hii hawajalI kabisa
 
Dah...mimi huwa nawashangaa waTanzania, ni wazuri sana wa kulalamika. Wakati maDaktari walipogoma walikuwa na madai mengi, yakiwemo ya kuboresha mazingira ya kazi (hospitali), upatinakaji wa uhakika wa madawa na vifaa tiba, na motisha kwa wahudumu wa afya (mishahara, alawansi za kuitwa dharura, na mrupurupu ya mazingira hatarishi na magumu)...lakini serikali 'kilaghai' ikawachonganisha maDaktari na wanachi wakaonekana walafi na wenye tama ya mishahara mikubwa. Wananchi walishindwa nini kuwaunga mkono maDaktari kwa hayo madai mengine yanayowahusu kama hakukubaliana na hilo la motisha!? Wananchi hao hao tena wagonjwa maowodini ambao ni mashahidi wa mazingira mabovu ya utoaji huduma za afya hospitalini hapo waliwashutumu maDaktari kwa maneno ya kukera tena kwenye vyombo vya habari...that was 2011! Leo hii wagonjwa wanalamikia kitu kile kile walicholalamikia maDaktari huko nyuma wakitegemea serikali hii itawasikiliza wao..wakati ilishindwa kuwasikiliza maDakatari na kuwaadhibu kidhalimu wakiwang'oa kucha na meno baadhi yao
 
Hii taarifa aje kuisoma mlamba viatu. Pasco wa jf na amtumie baba yake na rizone
 
Last edited by a moderator:
Cha kufanya? Aandaeni basi maandamano watu tujitokezee tuu watue kulikoni ukosefu wa dawa huu..!!
 
Usishangae hii ndo serikali ya ccm inavyotimiza hirani zake ,na bado mpaka kinamama waikatae
 
Back
Top Bottom