Hali ilivyo ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ilivyo ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPU, Feb 18, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [​IMG][​IMG]

  Sehemu ya Wahanga wa Mabomu ya Gongo la Mboto wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar wakisubiria kujua nini kinaendelea kwa upande wao. Kama vile wanasubili Mechi ya Simba na Yanga

  [​IMG]


  Afisa wa Msalaba Mwekundu,Mama Jane Lweikiza akiwa amembeba mtoto aliekutwa maeneo ya Sitaki Shari,Ukonga mchana huu kutokana na kutojulikana walipo wazazi wake mara baada ya kutokea kwa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto usiku wa kuamkia leo.Wahanga woote waliokumbwa na mkasa huo wapo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar kutokana na hali ya usalama wa maisha yao pamoja na kupatiwa misaada mbali mbali.


  [​IMG]


  Bw. Salum Madaba wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Mwalimu Kiondo wa Shule msingi Tandika wakimnywesha maziwa mmoja wa watoto waliopo katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar ambaye haijulikani wazazi wake walipo mpaka hivi sasa.


  [​IMG]


  Watu Msalaba Mwekundu wakishusha Maji ya Kunywa kwa ajili ya Wahanga hao waliopo ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar hivi sasa.Misaada mbali mbali inaendelea kuleta Uwanjani hapa ili kuweza kuwasaidia watu mbali mbali waliopo uwanjani humu kutokana na kukumbwa kwa tukio hilo la milipuko ya mabomu katika makazi yao huko Gongo la Mboto na maeneo ya jirani na hapo.


  [​IMG]
  Wengine wakiwa nje ya uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kupumzika chini ya vivuli vya miti kutokana na kutolala usiku wa kuamkia leo kwa hali ya milipuko ya Mabomu iliyotokea maeneo ya Gongo la Mboto katika maghala ya silaha ndani ya kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).

  [​IMG]
  Mtoto Gerald Samson akiwa na Mareraha usoni mara baada ya kuumia wakati akijaribu kutaka kujinusuru na milipuko hiyo jana usiku.

  [​IMG]
  [​IMG]


  Kamanda wa Scout akiwapanga vijana wake katika makundi mbali mbali ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar,mchana huu.

  [​IMG]

  Sehemu ya Matenti ya dharula yaliyowekwa ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar.


  [​IMG]

  Hawa ni Watoto ambao waliokotwa huko Gongo la Mboto wakiwa wako peke yako kutokana na wazazi wao kukimbilia sehemu zisizojulikana kutokana na milipuko ya mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto.

  [​IMG]


  Baadhi ya watoto wakiendelea kuletwa uwanjani hapa kwa ajili ya mapumziko na kama kuna ndugu wa karibu aweze kuwatambua.
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kinachoendelea kulundika watu hapo uwanjani ni UVUMI kuwa mabomu yataendelea kulipuka na hasa yale ambayo yamezagaa mitaani. Sababu nyingine ni umasikini tu wa watu wetu. Wanadhani kuna misaada ya pesa itatolewa pale.
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Walifuata maelekezo ya wakubwa
   
 4. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwenye red hapo ndo CCM anapopataka/anapotokea na kuendelea kutawala....umasikini!
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Umeshakuwa mradi wa watu huu. Hapo watu watakula mabilioni, usione kama wanasaidia watu, bajieti yake utaisikia tu. Mimi nimechoka kuwa katika nchi ya namna hii.
   
 6. CPU

  CPU JF Gold Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hehehe kupitia mabaraza ya usalama
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
  KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
  YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


  Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake. Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

  Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

  Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

  Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

  Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
   
 8. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  sasa walivyojaa hivyo usiku wanalalaje? poleni sana wahanga wa mabomu ya gmbt
   
 9. CPU

  CPU JF Gold Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sijui wanalala hivyo hivyo walivyokaa?!!! Yaani nina hasira nyieeeeeeee na hapa paka walio madarakani? aaaaagrrrrrr
   
 10. F

  Felister JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mungu mwenye nguvu na enzi yote awafariji kwa faraja ipitayo ufahamu wa wanadamu, awape ustahimilivu na amani mioyoni mwenu. Ninaomba neema na rehema kwaajili ya watoto wachanga ambao wazazi wao hawajulikani walipo na wote kwakuwa mazingira hayo ni mateso kwao; Mungu si dhalimu machozi yenu na mateso hayata potea bure mkistahimili na kuvumilia atawapa nafasi na pengine maisha haya ni mwanzo wa maisha mengine mazuri zaidi duniani ama hata mbinguni kwawale waliopoteza maisha. It is so touching and painful to think about!

  POLENI NDUGU ZANGU WA GONGO LA MBOTO!
   
 11. CPU

  CPU JF Gold Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Aisee hapa naona kama unasali vile, nilitaka nifumbe macho
   
Loading...