Hali hii nnanifanya Nijiingize kwenye Siasa

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
362
This place is turning me into a politician. Kwa kweli, nilikuwa sina interest kabisa na mambo ya siasa, but I can feel something burning inside me. Natamani kila Mtanzania anayejua kusoma angeweza kuingia humu akasoma uchafu unaoendelea serikalini. Naamini kama wenzetu wa vijijini wangekuwa wanapata hizi nyeti kama mimi leo, kungekuwa na machafuko makubwa nchi nzima! Hivi haiwezekani tukaipromote hii site kwa Watanzania wote? Tuwe na matangazo redioni na mabango mitaani? Kama ni fedha, naamini wengi tutakuwa tayari kuchangia. Nimeamshwa na haka kamtandao na naamini kila atakayeingia humu ataamka tu.

Selfishness of our leaders is the main issue here. Wao na familia zao ndio wanaendesha magari mazuri huko barabarani, majumba mazuri ya kwenye fukwe za bahari, yote yao. Wakiumwa mafua tu wanakimbilia Ulaya - bila haya kabisa. Kazi zote nzuri wanawapa watoto wao kwa vijinote tu! On a personal note, I have never felt so low in my life (was almost in tears!) because of any political-related issues, na sijawahi kupost article wala comment yoyote kuhusu politics hapa - but I'm being turned into a politician (if not a fighter) now.

Post ya Kapuya kurejea toka India akiwa mzima wakati mwenyekiti wa CCM wilaya aliyepata naye ajali anakufa Muhimbili imenitia huzuni kubwa, najuta hata kwanini niliisoma. Kama tungekuwa na serikali makini, ingekuwa ni very possible kwa kila Mtanzania anayekuwa involved kwenye critical accident kuwa airlifted toka popote pale alipo na kuletwa Dar - why should it be kwa vingunge tu? Si wote tuna roho moja tu? Naamini kila kanda, kama sio mkoa, ina uwezo wa kuwa na helikopta for accidents and emergencies, ni mipango tu. Kuwa makini kwenye kusaini mikataba ya madini, hakikisha mabilioni ya fedha hayachotwi BOT. Utaona kuwa ninachosema sio ndoto.

Hii ya story ya wapinzani leo huko Urafiki ndo imenimaliza kabisa, inatia kinyaa, I felt like puking at the end of it. Kwanini watu hawana aibu kiasi hiki? What on earth were they thinking? Kwamba Watanzania tutaendelea kulala tu na hakuna kitakachojulikana? Kuna msitari wa wimbo mmoja wa Hayati Bob Marley anakosema "You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time..." and this is proving to be very true. Someone, somewhere needs to do something - we can't let this rot go on like this. Cha kushangaza ni kwamba uchaguzi mwingine ukifanyika watu bado wataichagua CCM (kama sio CCM kuiba kura!)

Sorry, have to go and get some antidepressants, I need them today. So pi...d off at the moment.
 
Watu wanasubiri kwa hamu kubwa sana pale watakapopata pa kuanzia basi kumalizia ni rahisi.mengi yanatia uchungu lakini hakuna jinsi.
 
Kama huyu mwenyekiti ni wa CCM basi safi sana. haya ndiyo wanayoyataka tukiwaambia wanatuona wajinga wache wafe kwa njaa zao
 
Na talkin about that ajali, sina uhakika ila kwa mawazo na fikra duni zangu yawezekana kabsaa wakati waziri kapuya akiletwa Bongo kwa ndege, kupelekwa India kwa pipa if not ndege... yule marehemu ilibidi asubiri aina nyingine ya usafiri kumfikisha Dar na sina shaka kama ilikua ni siku ile ile but it took time... jamani nimesema ni fikra zangu tuu na nionavyo jinsi kakampuni ketu ka kutapeli watz kwa speed kubwa kaitwacho CCM kinavyojua set priorities...
 
yaani sie wa tz na haka ka kampuni ketu ka mafisadi if not matapeli tulie tuu laaaaaabda tungojee danganywa tena kama kawa mwaka 2010 kwa sasa tuendeleee funga mkanda na kutulia kama twanyolewa wakati ndege yetu ikipaaa
 
What happened kwa huyo M'kiti wa CCM wilaya is very sad na kilitushangaza wengi tu. Lakini bwana, sote tunajua viongozi wetu ni selfish kupita kiasi, kama wewe ni "small fish" basi huangaliwi na hupewi consideration hata kidogo. Anayeangaliwa ni the "big fish"! Huyo kapuya angeweza ku-insist kwamba yeye hajambo lakini badala yake apelekwe huyo anayeumwa zaidi, ninaamini wangepelekwa wote wawili. Unafahamu wakati mwingine kinachohitajika ni mtu mmoja tu aonyeshe kwamba "hivi siyo sawa", na kitu kibaya kinarekebishwa

On the other hand, viongozi wetu nadhani ni washamba pia....kama JK anaona uroda kupanda pipa, sembuse hao wa chini yake? ushamba na ignorance ndivyo vinavyowasumbua!
 
Pole Kana
Kwa mwendo huo wa kuchota mabilions basi wangetuachia basi hizo kazi za BOT sie walalahoi au wangewapa watoto wao ajira kwenye makampuni yao.Si wameshatubrainwash kwamba "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe"? sasa mbona hatupewi mahali pa kuzitumia nguvu zetu? najua kwa kautaratibu ka 'special clearance'-wala hutumii nguvu!!...yes! they dont need nguvu like us. Sasa sisi makapuku tukimbilie wapi? kila kitu wanachukua wao tu, inauma sana hakyanani. Lakini naona mwisho wa haya yote hauko mbali, itafikia kipindi kila mlala hoi atasema-"BORA TUKOSE WOTE, LIWALO NA LIWE!!"
 
Post ya Kapuya kurejea toka India akiwa mzima wakati mwenyekiti wa CCM wilaya aliepata nae ajali anakufa Muhimbili imenitia huzuni kubwa, najuta hata kwanini niliisoma.

This is very sad indeed!
 
Katika serikali hii, hasa baada ya Azimio la Arusha kuvunjwa, ni kwamba sasa CCM imegawa watu na viatu! Watu ni kama kapuya, viatu ni kama huyo marehemu na wengineo! Hapo ndipo mjue kuwa pamoja na wao kuchota hela na kuwa mabilionea wakati hizo hela zilipaswa kuboresha huduma za afya, elimu, n.k.

Lakini bado hao hao wakiugua huzikimbilia hizi hospitali zetu mbovu choka mbaya, Muhimbili wodi ya wazazi wanalala wazazi wawili na wengine hulala chini ya safafu (ila huweka magogoro yao yaliyochoka!). Si mmesikia Karamavi na TISCS yake anabishana na TRA kuhusu kuchelewesha makontena bandarini!

Ninakuambia leo hii Karamavi akiugua hatatibiwa nchini atapelekwa Ulaya tena kwa gharama/kodi yetu!

Lakini cha ajabu humu, akina so and so, mtazama pande mia, n.k., au masamaki, n.k., kila linalosemwa hata kama ni baya wao hupinga tu! Sijui! Anyway, si mnaona makala humu kuhusu mafisadi na watetezi wao humu!
 
Back
Top Bottom