Hali duni ya maisha inaweza athiri afya na kupelekea kifo

Chafe

Member
Sep 10, 2021
12
14
Nidhahiri Hali duni ya kimaisha, hasa pale mtu anapougua na hali ya kipato chake cha maisha ni duni. Hii huweza kupelekea kukosa matibabu sahihi kwa wakati na hatimaye kupelekea kupoteza maisha.

Vituo vya afya vya Serikali unaambiwa lipa kwanza upewe huduma, wakati huo mchana MTu hajui atakula nini, anaona Bora akanunue Panadol kutuliza homa, na ndipo baadae anapozidiwa na kuhatarisha maisha yake

Mfano: Sehemu fulani hapa Tanzania siku chache zilizopita mtu ,kapata ajali akaona Bora awahi hospitali akapate msaada ,lakini hakuwa na akiba ya hela, alipewa huduma na baadae wakadai alipe, alishindwa kulipa na wakamtoa nyuzi alizoshonwa.

Tujali utu kwanza na Serikali iangalie namna ya kuwasaidia Watu wanaoshindwa kumudu matibabu yao.
 
Back
Top Bottom