Hali bado tete Uturuki: Polisi 8,000 na Wanajeshi 6,000 wakamatwa na kushtakiwa

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,195
2,000
Vikosi vya usalama nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki iliyopita.
Runinga rasmi ya serikali nchini Uturuki- Anadolu, inasema kuwa maafisa wengine waliokamatwa ni pamoja na majenerali wakuu wa kijeshi.
Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.
Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa hao wanalaumiwa kwa kuwa na uhusiano na mapinduzi hayo ambayo serikali inadai kuwa yalipangwa na kiongozi wa dini aliyeko uhamishoni nchini Marekani- Fethullah Gulen.
Msako dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika na mipango ya kuipindua serikali juma lililopita nchini Uturuki, unaendelea.
Usiku wa kuamkia leo na mapema Jumatatu alfajiri, zaidi ya maafisa elfu nane 8,000 wa polisi walikamatwa kushauriwa kuwasilisha bunduki zao na kusimamishwa kazi.
Kituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa hao kukamatwa.
Waendesha mashtaka wameanza kuwahoji kinara mkuu wa jaribio hilo la mapinduzi ambaye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la angani Akin Ozturk, ambaye ni miongoni mwa makamanda wakuu 100 waliokamatwa.
Maafisa wanane wa kijeshi walioingia nchini Ugiriki kwa kutumia Helikopta, wamefikishwa mahakamani katika mji ulioko mpakani wa Alexandrou-poli, ili kushtakiwa kwa kuingia nchini humo bila idhini.
Uturuki imeomba Ugiriki kuwarejesha nyumbani ili kushtakiwa, lakini mawakili wao wameomba idhini ya uhamiaji.

: Naona hali bado sio shwari na mwenendo huu wa kamata kamata inayowakumba hadi maofsa wa jeshi na polisi itazidisha hasira na hamasa ya kutokea kwa mapinduzi mengine
 
Prof

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,578
2,000
jamaa lazima ata-retaliate na atakuwa mkatili sana this time...Kushindwa kumpindua jamaa ilikuwa ni grave mistakes..
 
BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
7,891
2,000
Akamate wote wanaohusika pumbavu kabisa, na ikiwezekana wanyongwe asibaki hata mmoja..raisi kama huyo kumpata ni nadra mnoo,ni mtu mwenye uchungu sana na nchi yske na wananchi wake,Big up Ordogan wewe ni jembe la uhakika
 
Prof

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,578
2,000
Ila hao wanajeshi hawajui kujiongeza, ilitakiwa wakimbilie syria-kwa Assad, then wana form Rebel group na hapohapo Russia atatia mguu kuwapa silaha na training, then wanalianzisha kuelekea mji mkuu wa Uturuki....lazima kingeeleweka tu
 
Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
6,892

duh! we nawe umenifungua macho, kumbe russia ndo mfadhili wa waasi?!
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,195
2,000
Akamate wote wanaohusika pumbavu kabisa, na ikiwezekana wanyongwe asibaki hata mmoja..raisi kama huyo kumpata ni nadra mnoo,ni mtu mwenye uchungu sana na nchi yske na wananchi wake,Big up Ordogan wewe ni jembe la uhakika
anatengeneza mapinduzi mengine
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,250
2,000
Jamaa yaelekea anavisasi na wengi sasa hivi kahamia kwenye Tasisi ya Elimu keshatimua zaidi ya mamia... Sasa walimu wanaweza vipi kupindua nchi??? Keshaambiwa akiua mtu asahau kujiunga na ulaya
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,564
2,000
Ila hao wanajeshi hawajui kujiongeza, ilitakiwa wakimbilie syria-kwa Assad, then wana form Rebel group na hapohapo Russia atatia mguu kuwapa silaha na training, then wanalianzisha kuelekea mji mkuu wa Uturuki....lazima kingeeleweka tu
mapinduzi ya kuanzisha civil war ni kazi sana na uturuki ni nchi kubwa sana.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,564
2,000
Jamaa yaelekea anavisasi na wengi sasa hivi kahamia kwenye Tasisi ya Elimu keshatimua zaidi ya mamia... Sasa walimu wanaweza vipi kupindua nchi??? Keshaambiwa akiua mtu asahau kujiunga na ulaya
alisema mampinduzi yalikuwa kama baraka. yamempa nafasi ya kuclean/purge wapinzani wake.
 
concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,299
2,000
Kwa jinsi ninavoona hapa ndo anachochechea mapinduzi. Na inasemekana hii ishu aliifanya mwenyewe ili apate nguvu ya kuwamaliza wapinzan wake. Fikiria ndege za kivita ziliscramble ndege yake lakin hazikumlipua. Kama kweliwalikuwa na nia ya kummaliza wangeshusha ndege yake. Yasije kuwa kam yale ya russia baadae akapiga goti mwenyewe. Kumbuken kuna allegation warusi walitoa kuhusu yeye kuhusika luuza mafuta ya isis
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,195
2,000
Jamaa yaelekea anavisasi na wengi sasa hivi kahamia kwenye Tasisi ya Elimu keshatimua zaidi ya mamia... Sasa walimu wanaweza vipi kupindua nchi??? Keshaambiwa akiua mtu asahau kujiunga na ulaya
Anazidisha chuki pasi yeye kujua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom