maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,344
Kuna mtoto wa kijijini kwetu huku Serengeti ambaye alipungukiwa sifa ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu mwaka juzi lakini katika uchaguzi wa pili alifanikiwa kuchaguliwa kusoma kozi ya digrii ya kwanza ya Electrical and Electronic Engineering huku akiwa hakukidhi sifa za kusoma kozi hiyo kwa kutokuwa na alama za kutosha katika mtihani wa kidato cha sita.
Mwanafunzi huyo ambaye alisoma shule za kata tangu aanze kusoma kozi hiyo kwa miaka yote miwili amekuwa akifanya vizuri kuliko wenzake wote wa kozi hiyo walioingia kwa kufikia vigezo.
Cha ajabu hivi karibuni amesimamishwa kuendelea na masomo kwa maelezo kwamba alichaguliwa kimakosa kusoma kozi hiyo kwa sababu hakuwa na sifa, na huo ndio ukweli.
Ninachopenda kuuliza ni kwamba hii ni halali na haki kumsimamisha masomo wakati hakudisco ama kusup somo hata moja na ana GPA ya 4.0?