Hakutakuwa na mgao wa umeme-Wizara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,355
33,194
WIZARA ya Nishati na Madini imewahakikishia Watanzania kwamba hakutakuwa na mgao wa umeme kwani kiasi cha upatikanaji wa umeme kwa sasa kinakidhi mahitaji.
Jana Katibu Mkuu wa wizara ya nishati, Eliackim Maswi, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

“Napenda kuwahakikishia Watanzania kwamba serikali imejizatiti katika kuhakikisha kwamba hapatakuwepo na mgawo wa umeme kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza,” alisema


Alisema sababu ambazo zinasababisha umeme kukosekana hazipo kwani vyanzo vyote vya umeme vimejitosheleza na hakuna sababu itakayofanya kukosekana kwa umeme kwa sasa

Alisema mahitaji ya umeme kwa sasa ni kati ya megawati 650 hadi 720 na uwezo wa ufuaji umeme utokanao na maji, gesi asili na mafuta ni megawati 720.

Aliongeza kuwa mitambo ya gesi ya asili itakuwa na wastani wa megawati 348 kati ya hizo 180 za Songas, Ubungo Plamt I(Wartsilla) megawati 77, Tegeta 41, Ubungo Plant II (Jacobsen) megawati 50.

Aliendelea kufafanua kuwa, mitambo ya mafuta itakuwa na wastani wa megawati 240 kwa mchanganuo ufuatao - IPTL (megawati 100), Symbion Dodoma (megawati40), Symbion Arusha (40) na Symbion Ubungo (Jet A1) megawati 60.
Hakutakuwa na mgao wa umeme-Wizara
 
Hata muda sisi hatuna umeme! Halafu kama vile kuna mtu huko Tanesco anataka kutuingiza kwenye umaskini!
Anawasha na kuzima, matokeo yake vitu vya thamani vyaweza kuungua au nyumba kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom