Wana JF! Habari za asubuhi. Nina rafiki yangu amekuja kwangu na tatizo dogo niliona bora nije huku kupata ushauri toka kwa wataalamu maana sijawahi deal na hili swala.
Rafiki na mume wake wamejaaliwa kupata mtoto wa kiume, ana miezi 7. Wote wakristo ila dhehebu tofauti. Baba alipeleka mtoto kwa wazazi (baba na mama wa baba) kuombewa wakati mama yuko kazini. Mama hakushirikishwa wala kuambiwa kuhusu hili jambo. Mama amekasirika. Baba alisema hakujua kwamba angetaka kushiriki, no big deal.
Swali: alifanya haki kutomshirikisha mkewe? Is it really not a big deal? Mimi si mtu wa kanisani sana (spiritual, not religious) kama dada na mmewe kwahiyo nimeona ngoja niwaulize wengine.
Atakua na shaka na hilo neno hapo, kuombewa kwa nani? Mungu? Miungu? Maana imekua kama maombi yalikua ya ghafla sana, tena bila taarifa zozote kwa wahusika wakuu!
Binafsi najiuliza tu;
Miezi 7 ni mingi kiasi, ina maana hao wazazi hawakuwahi kumwona huyo mtoto na kufanya maombi kama inavyohitajika? Mbona inaonekana wanaishi karibu tu kiasi cha kumpeleka mama akiwa kazini? au ni maombi endelevu na kila wanapotamani kumuombea wanamuita nyumbani kwao?
Wazazi (baba na mama wa baba) walishindwa nini kuja kumuombea hapo nyumbani wanapoishi na mkewe?
Kulikuwa na uharaka gani wa hayo maombi kiasi cha kuharakisha katikati ya siku mwenzake akiwa kazini?
Sidhani kama ni sahihi kusema no big deal, kwa sababu huyo mtoto ni wa kwao wawili so mambo mengi hasa haya ya kiimani yanataka maridhiano ya wote, labda kama ni kati ya yale makabila ambayo mtoto akiwa tumboni ni wa mama, ila akishatoka nje tu anakua wa baba!!
Kama alirudi na majivu, nafikiri atakuwa amekwenda kufanyiwa mambo ya mila, lakini si vibaya kama yeye angeshirikishwa, nahisi huyo dada ana wasiwasi kwamba mwanaye amefanyiwa nn wakati yeye hayuko.so he says. Kumbuka dada hakuwepo, mtoto alirudi akiwa na kama majivu kwenye paji la uso. Is this a catholic thing ?
Mi nilifikili alimpeleka kufanyiwa mambo ya mila kumbe maombi?
so he says. Kumbuka dada hakuwepo, mtoto alirudi akiwa na kama majivu kwenye paji la uso. Is this a catholic thing ?
eti! maombi ndo alalamike? shasema huyo mama ana visa tu!
Soma vizuri...Mimi ndo nilisema si mwanamaombi, ila wao (dada na mmewe) ni wakristo ila dhehebu tofauti.
...mtoto alirudi akiwa na kama majivu kwenye paji la uso.
Kwa kuangalia kalenda yangu haraka haraka kwa hakika hiyo siku ilikuwa Jumatano ya majivu...na ni kawaida kwenye misa hiyo kuchorwa alama ya msalaba kipajini kwa kutumia majivu kuashiria kuanza kwa majira ya kwaresma.
Kosa lipo kwa wanandoa hao kutokubaliana juu ya imani zao hasa watakapopata watoto. nadhani ni muda sasa wakae chini ni kukubaliana juu ya jambo hili.
May be walipokuwa wachumba walili-brush off kusema ah dini haitatuzuia ku-enjoy ndoa infact sisi sote si ni wakristo...lakini ts those minute differences zinazoweza kutumiwa na Shetani kuingilia ndoa yao...wakae chini sasa tena ikiwezekana ku-compromise ili waende kanisa moja pamoja...inapendeza!
Alitaka kushiriki yeye pia kama mzazi. Si kwamba mungu ni tofauti.