HAKUNA

HAKUNA

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,702
Reaction score
60,336
HAKUNA watoto wa mitaani/
kwa mtaa ukimuona mtoto tambua Ni mtoto wa jirani/
hata akiokota makopo jalalani/
kumbuka changamoto maisha Ni msoto bila Imani/
HAKUNA siku bila mwanga/
usiku bila wanga/
pia HAKUNA jogoo la mjini linalowika shamba/
HAKUNA habari bila mwamba/
hesabu bila namba/
Unabisha?fanya tahmini hakuna sababu ya kusanda/
Skia HAKUNA mkasa bila kisa/
anasa bila maisha/
falsafa bila fikra/
Pia kumbuka HAKUNA mganga asiye na sifa/
Kuna uongo pia ujanja we sio wa kwanza unayefichwa/
HAKUNA anayefanana na MUUMBA/
Sote Ni mfano wake na ndo maana ametuumba/
Mbingu Ni Mali yake,nchi Ni Mali yake,
So HAKUNA Kama yeye kwenye ufahari huu wa kuumba/

HAKUNA furaha bila Hali ya kuridhika/
HAKUNA karaha pasipo Hali ya kughadhibika/
hamasika unayependa kukuza Mambo kuza mipango maana Hali inatisha
HAKUNA mwisho bila mwanzo/mwampamba anapamba mapambo/tokea kitambo HAKUNA kifo bila chanzo/
Wito Bila wazo/ au safari Bila hatua msafiri tambua kuwa ulipo upo hapo/tekeleza dini tambua HAKUNA amani bila matendo/mziki Bila maisha au maisha bila mziki,Bila MAMA tambua mwana hakuna duniani hata kwa skendo/
Duniani uwanja wa Vita na hukumu/ ila HAKUNA anayependa kufa japo maisha magumu/
HAKUNA anayependa kufa japo maisha magumu/na HAKUNA Kama Mimi Ni fikra ndani ya Africa Ni zoom
 
Back
Top Bottom