Hakuna watu wanaongoza kunyima watu rizk za kazi kama Walinzi na Masecretary

Watu wenye nguvu kwenye taasisi yoyote ya umma, na hata za binafsi, wenye nguvu wakati mwingine kuliko hata afisa-masuhuli, ni kwa mpangilio ufuatao:

1. mlinzi, getini na penginepo
2. mesenja,
3. mtunza kumbukumbu,
4. katibu-muhtasi / OMS / msaidizi/ katibu wa bosi

Nguvu yao ni ile inaitwa "soft power", haionekani kirahisi kwa asiyeelewa. Magradueti wengi tunapopeleka bahasha maofisini humo tunawaletea zeleu watu hao tajwa hapo juu. Wakitutunishia misuli yao, ndipo tunapoigundua nguvu kubwa waliyonayo, lakini tukiwa tumechelewa.
 
You said something very great
 
Kwenye orodha yako ongeza wahudumu wa masjala (Registry)

...
Ndio watunza kumbukumbu hao. Ni watu muhimu sana. Na wao wamo mpaka magradueti waliosomea kutunza kumbukumbu.

Tuheshimu kila mtu pasipo kujali kipato tunachodhani wanapata, elimu (vyeti) tunayodhani wanayo, na viashiria vingine vya kibaguzi.
 
Mimi haikuwa inshu ya kazi ila hili swala liliwahi kunikuta. Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuwa na appointment na kiongozi mmoja wa taasisi fulani hapa nchini..Siku ya miadi imefika nikawasiliana nae akaniambia njoo ofisini muda fulani. Kweli, ule muda umefika nikaenda pale ofisini nikiwa na wenzangu (wote kwa pamoja yule kiongozi alikuwa anatujua na alitupa appointment).

Tumefika pale reception tukamkuta secretary ni mama mtu mzima..Alikuwa na 45+ by then. Tukamsalimia na kuweleza shida yetu. Mama akatuambia mkuu hayupo. Tukamwambia tumeongea nae dakika kadhaa zilizopita kasema tuje muda huu, basi kama ametoka kidogo tunaomba tumsubiri (Tulikuwa na uhakika mkuu yupo ila mama alitaka kutufanyia mtimanyongo). Mama akakaza na akawa anapanda juu (anawaka). Kilikuwa ni kitu cha ajabu ikizingatiwa kuwa sisi tulikuwa tunaongea kistaarabu na nafasi za kukaa pale reception kwa wageni zipo kama ilivyo utaratibu kwenye maofisi mengi. Mama aliwaka sana (Naamini alitudharau kwani aliona pengine sisi vijana tusingekuwa na appointment na boss wake)..

Mama alifikia hatua ya kutufukuza kwa maneno makali na kutuambia atatuitia walinzi muda sio mrefu..Nadhani wakuu mnajua maumivu anayoyapata mtu kufokewa kwa kitu ambacho hastahili..Tuliamua kumpa ushindi tukatoka nje kabisa ya ofisi ila hatukuondoka maana tuliamini Mkuu yupo kwahiyo ilibidi tukae nje huku tukiangalia kama tunaweza kumuona maana asingeweza kutuongopea. Tumesubiri kama dk. 10 tukamuona mkuu anakuja maeneo ya ofisi yake..Alipotuona tukasalimiana pale pale nje na akasema karibuni ofisini...

Tukaanza kwenda nae ndani hadi ofisini kwake..Wakati tunapita yule mama alishituka sana kiasi kwamba hakutegemea kuona kuwa Boss wake ni 'rafiki' yetu maana tunatembea huku tukipiga story zinazoonesha tunafahamiana. Tukaingia ofisini, tumeanza mazungumzo yetu na mkuu kama dakika 3 zikapita yule mama akaingia akiwa hajiamini amini..Sijui alihisi sisi 'tutamchoma' kwa boss wake...Akaanza story zake mara eti boss samahani naomba niwaulize hawa vijana hii AC nipunguze au niongeze baridi maana nawahurumia nyie ndio nguvu kazi ya taifa huku akijichekesha kwa boss wake..Sisi tulimwambia asante Mama, tuko sawa tunashukuru...Akatoka zake huku akisema kuweni free sisi (wafanyakazi wa ile ofisi) tupo kwajili yenu...Tulimshukuru kinafki pale na baada ya kumaliza mazungumzo kama nusu saa hivi badae tukatoka tukamuaga na akatukaribisha tena siku nyingine....

Ni muda mrefu umepita ila sijaisahau sura ya yule mama....sitaki kumsema vibaya maana anaweza kuwa mama wa mwana JF mwenzetu au akawa Member kabisa...Ila kama yumo humu nasisi wote tujifunze tu kutokuwa na roho mbaya.

HITIMISHO LANGU: 90% ya mabosi au watu wenye nafasi niliokutana nao hawana noma kabisaaa yani....Tatizo ni hawa masekretari....Na huwa inaniumiza sana kuona mama zetu/wanawake (sio wote) amabo ndio 'wamiliki' wakuu kwenye hizo nafasi wakiw wanaongoza kwa chuki.​
Wanawake wenyewe hatupendani we acha tu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye orodha yako ongeza wahudumu wa masjala (Registry)

Wale watu wanaringa balaa alaf salary zao sasa
Sometimes mshahara ni matumizi ya mtu mwenyewe.

Mfano, kama mimi nalipwa laki moja, usiseme tu ni mshahara mdogo kwa kuuweka kwenye matumizi yako. Uweke kwenye matumizi yangu ndio utajua kama ni mdogo au hautoshi siyo yako.

Ndio maana mtu anaweza kuwa analipwa 15M akasema mshahara ni mdogo ( kwa matumizi yake ) lakini wewe ukaona ni pesa nyingi sana ( kwa matumizi yako )
 
Hii naweza sema inasababishwa na chuki tena chuki dhidi ya maisha yao wenyewe binafsi, wengi wanachukia wanavyoishi. Ukiondoa masecretary katika baadhi ya sehemu, walinzi na masecretary wengi wanafanya hiyo kazi si kwa kupenda kiasi kupelekea kuichukia hiyo kazi kutokana na ukweli kwamba wanakutana na masahibu mengi kama kutopata usingizi wa kutosha, mshahara mdogo mnoo, dharau toka kwa wateja, lakini pia wakati mwingine ni utaratibu tu wa Kijinga wa kuiga. Kwahiyo wao kitu cha kwanza mgeni anapokuja wanajijengea mentality ya kuona kuwa wanadharaulika kutokana na kazi anayofanya hata kama huyo mgeni ata play nice, ili kufanya cover up na kujiboost ili uone na yeye ni wa muhimu.

Hali hii pia kama umewahi kuexperience ipo hata kwa maaskari na wajeshi, mara nyingi askari wa kawaida ni wanoko wasumbufu na si waelewa kbs tofauti na maafisa.
 
Mimi ni Graduate na nimefanya sana kazi ya ulinzi.

To be honest, mimi binafsi nimechana sana CV za watu waomba kazi.

Sababu hapa ziko pande zote: Wabongo tunajuana, tunaishi kwa kudharauliana, kila mmoja anajiona yeye ndio mwamba.

Unafika getini, unamuona mlinzi kama takataka kumbe hujui sometimes huyo mlinzi anakuzidi hata CV na uzoefu.

Mimi nimewahi kuwazingua watu wengi tu tena wakubwa kwahiyo haijawahi kutokea nikamwogopa mtu yeyote.

Kuna kipindi cha Makinikia, kuna watu walitumwa kutoka Ikulu wakaja kuchukua sample, baada ya kuchukua wakatukuta getini. Na sisi tuna taratibu zetu za kutoa mizigo wao hawataki kuzifuata ili kuficha Identity zao.

Tuliwasumbua sana, mpaka wakakasirika wakawapiga pingu wenzetu, ila mwisho wa siku wakaamua kusema kweli.

Muhimu ukifika sehemu kuwa mnyenyekevu, fuata taratibu ulizozikuta kama wana nia njema watakusaidia tu.

Hizi mentality kwamba ukiona mtu ni mlinzi unaona hana jipya, kazi yenyewe kazi gani, maisha yamemshinda hakwenda shule zimepitwa na wakati.

Baadhi ya hao walinzi wanawazidi uwezo staff kibao kwenye hizo ofisi wanazolinda.

Hii ni kwa ufupi tu.

Duuhh
 
Mimi haikuwa inshu ya kazi ila hili swala liliwahi kunikuta. Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuwa na appointment na kiongozi mmoja wa taasisi fulani hapa nchini..Siku ya miadi imefika nikawasiliana nae akaniambia njoo ofisini muda fulani. Kweli, ule muda umefika nikaenda pale ofisini nikiwa na wenzangu (wote kwa pamoja yule kiongozi alikuwa anatujua na alitupa appointment).

Tumefika pale reception tukamkuta secretary ni mama mtu mzima..Alikuwa na 45+ by then. Tukamsalimia na kuweleza shida yetu. Mama akatuambia mkuu hayupo. Tukamwambia tumeongea nae dakika kadhaa zilizopita kasema tuje muda huu, basi kama ametoka kidogo tunaomba tumsubiri (Tulikuwa na uhakika mkuu yupo ila mama alitaka kutufanyia mtimanyongo). Mama akakaza na akawa anapanda juu (anawaka). Kilikuwa ni kitu cha ajabu ikizingatiwa kuwa sisi tulikuwa tunaongea kistaarabu na nafasi za kukaa pale reception kwa wageni zipo kama ilivyo utaratibu kwenye maofisi mengi. Mama aliwaka sana (Naamini alitudharau kwani aliona pengine sisi vijana tusingekuwa na appointment na boss wake)..

Mama alifikia hatua ya kutufukuza kwa maneno makali na kutuambia atatuitia walinzi muda sio mrefu..Nadhani wakuu mnajua maumivu anayoyapata mtu kufokewa kwa kitu ambacho hastahili..Tuliamua kumpa ushindi tukatoka nje kabisa ya ofisi ila hatukuondoka maana tuliamini Mkuu yupo kwahiyo ilibidi tukae nje huku tukiangalia kama tunaweza kumuona maana asingeweza kutuongopea. Tumesubiri kama dk. 10 tukamuona mkuu anakuja maeneo ya ofisi yake..Alipotuona tukasalimiana pale pale nje na akasema karibuni ofisini...

Tukaanza kwenda nae ndani hadi ofisini kwake..Wakati tunapita yule mama alishituka sana kiasi kwamba hakutegemea kuona kuwa Boss wake ni 'rafiki' yetu maana tunatembea huku tukipiga story zinazoonesha tunafahamiana. Tukaingia ofisini, tumeanza mazungumzo yetu na mkuu kama dakika 3 zikapita yule mama akaingia akiwa hajiamini amini..Sijui alihisi sisi 'tutamchoma' kwa boss wake...Akaanza story zake mara eti boss samahani naomba niwaulize hawa vijana hii AC nipunguze au niongeze baridi maana nawahurumia nyie ndio nguvu kazi ya taifa huku akijichekesha kwa boss wake..Sisi tulimwambia asante Mama, tuko sawa tunashukuru...Akatoka zake huku akisema kuweni free sisi (wafanyakazi wa ile ofisi) tupo kwajili yenu...Tulimshukuru kinafki pale na baada ya kumaliza mazungumzo kama nusu saa hivi badae tukatoka tukamuaga na akatukaribisha tena siku nyingine....

Ni muda mrefu umepita ila sijaisahau sura ya yule mama....sitaki kumsema vibaya maana anaweza kuwa mama wa mwana JF mwenzetu au akawa Member kabisa...Ila kama yumo humu nasisi wote tujifunze tu kutokuwa na roho mbaya.

HITIMISHO LANGU: 90% ya mabosi au watu wenye nafasi niliokutana nao hawana noma kabisaaa yani....Tatizo ni hawa masekretari....Na huwa inaniumiza sana kuona mama zetu/wanawake (sio wote) amabo ndio 'wamiliki' wakuu kwenye hizo nafasi wakiw wanaongoza kwa chuki.​

Pole sana mkuu na hongeren kwa kuwa na mioyo ya uvumilivu
 
Jiwe mmetupa gizani, Mimi ni sekretary, nitajifunza kutenda Kama mafunzo ya kozi zetu, na tunaambiwa Sana kuhusu maringo na nyodo, Tabia za kuchana barua kubania watu kumwona boss, tunafundishwa na wakufunzi, katika somo la office practical, na sekretary duty, Ila tukitoka vyuoni tukiwa kwenye kitu tunajisahau tu wapendwa.

Mola akujalie uwe na moyo wa upendo kweli na sio maneno ukiwa mtiifu na mwenye upendo hata kazi yako itabarikiwa
 
Mm mwenyewe nilishawahi kuwa mlinzi, na elimu yangu ya bachelor degree kabisa.

Mlinzi anafuata orders au maelekezo anayo pewa na boss wake, ukiona amekwambia kitu Fulani, ujue hiyo Order kutoka juu .

Kitu kingene, utakuta anakuja mtu getini, anatanguliza dharau na jeuri, kwasababu wewe ni mlinzi,

Kifuatacho, nikukomoana,

Sawa mkuu
 
Binafsi Mimi huwa ni mstaarabu sana ila nikifika peak, huwa nina kiburi gunia 10 bila kujali naongea na nani.

Mimi kwenye kwenye hizo ofisi nimewahi kuwafungia sana nje staff kibao tena wenye nafasi zao kama Wahasibu, Procurement etc hadi wanapiga kelele

Unajua sometimes, kuna watu huwa wanadhani wanaweza kuwa maboss wa kila mtu.
 
Watu wenye nguvu kwenye taasisi yoyote ya umma, na hata za binafsi, wenye nguvu wakati mwingine kuliko hata afisa-masuhuli, ni kwa mpangilio ufuatao:

1. mlinzi, getini na penginepo
2. mesenja,
3. mtunza kumbukumbu,
4. katibu-muhtasi / OMS / msaidizi/ katibu wa bosi

Nguvu yao ni ile inaitwa "soft power", haionekani kirahisi kwa asiyeelewa. Magradueti wengi tunapopeleka bahasha maofisini humo tunawaletea zeleu watu hao tajwa hapo juu. Wakitutunishia misuli yao, ndipo tunapoigundua nguvu kubwa waliyonayo, lakini tukiwa tumechelewa.

Wengine ni hulka za roho mbaya ht km ukiwa mnyenyekevu kwake
 
Back
Top Bottom