Faiza umebadilika sana awamu hii, ingekuwa enzi ya mkwere bandiko lako lingekuwa na ukakasi!!
Lugha ipo mtu kusema dhaifu ndy katumia lugha mbovu!Hebu fungua kamusi ya kiswahili Angalia neno"dhaifu"ina maana gani....?Uwezo wa kuzisimamia hizo taasisi anao ila siyo kwa lugha ile na jukwaa lile, tukubali tu Asad kakosea
Huogopwi kuitwa na wewe FaizaFoxy na kazi ndugai!
Ila umeongea ukweli mtupu
Goodmorning
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Asaad siyo mwanasiasa wala siyo mwana diplomasia. Kumbuka hilo.Uwezo wa kuzisimamia hizo taasisi anao ila siyo kwa lugha ile na jukwaa lile, tukubali tu Asad kakosea
Kimaadili hairuhusiwi, sheria za maadili huwa hazina mijadala. Kinachoangaliwa hapo, pia ni dharau kw NchiLugha ipo mtu kusema dhaifu ndy katumia lugha mbovu!Hebu fungua kamusi ya kiswahili Angalia neno"dhaifu"ina maana gani....?
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Swadakta kabisa,huu utetezi wake umejificha kwenye udini kwa jicho kali sana japokuwa yupo pamoja na Assad.Kaguswa mwenzie wa middle east!
Mi nimemuona Halima amethubutu naye yupo kwenye kikaango.Wewe na mimi hata tupayuke vipi hapa JF nani wa kutusikiliza?
Nategemea kuna wabunge wachache wajitokeze na kuwa wa kweli wa nafsi zao na kupaza sauti ya wananchi.
Bunge ni dhaifu.
Mkuu FaizaFoxy unarudia rudia hilo neno kwamba Bunge ni ....., naona unataka Spika akuonyeshe kwamba Bunge lake si dhaifu.Assad ni mtu pekee Tanzania hii ambae yupo serikalini lakini anaweza kuikosoa mihimili yote mitatu ya mfumo wa uongozi wa Tanzania.
Anaweza kuukosoa mhimili wa taasisi ya Urais kwa maana ya wizara na idara zote zilizo chini ya taasisi ya Urais. Anaweza kuukosoa mhimili wa bunge ikiwemo ofisi ya spika. Anaweza kuukosoa mhimili wa mahakama. Anaweza kuikosoa mihili yote hiyo kwa kutokusimamia matumizi mazuri, ubadhirifu, uvunjaji wa sheria na kanuni za matumizi na ndiye pekee anaweza kutoa maoni yake ya udhaifu uko wap na akasikika.
Assad majukumu yake hayaishii serikalini tu, ni mtu pekee anaeweza kuyafanya yote hayo juu kwa upinzani pia.
Kwa kutazama hayo kwa uoana wake, Assad ni mtu pekee anaeweza kuikosoa (kwenye usimamizi wa fedha) Jamhuru nzima ya Muungano wa Tanzania.
Hilo ni jukumu kubwa sana na lazima awe na maadui kutoka kila pembe.
Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania matumizi mabovu ni kila pahala.
Ni dhahiri hakuna mhimili usio mchekea usoni tu lakini akigeuka anasonywa.
Kwa hiyo tusitarajie mhimili wowote kumtetea Assad zaidi ya wachache wanaotaka kuona matumizi ya fedha zao yanasimamiwa vizuri.
Hili sakata la Assad ndiyo litatuonesha ukweli wa mambo ulivyo Tanzania.
Hakuna ataepinga kuwa kuna madudu mengi ya kifedha yapo serikalini na inawezekana kabisa kuwa madudu hayo yapo hata ofisi ya spika. Spika ameshindwa kabisa kuliendesha bunge kuwa wasimamizi wa serikali na kwa maana hiyo basi bunge limekuwa dhaifu.
Tutegemee nani wa kuwa upande wa Assad?
Bunge ni dhaifu.
Kibri kimemja ila hata ulipomsikia akiongea na waandishi kuhusu Asad hakutumia kauli nzuri alikuwa anamchukulia Asad kama mtu wa kawaida,eti ataletwa kwa pingu hiyo ni dharau kubwa,Asad ni CAG mtu na professional yake hafanyi mambo kisiasaSasa kuna nini cha kuogopa? Mbona Ndugai haogopi, anatisha watu hadharani?
Lissu alipokuwa anasema kuwa Bunge limegeuka kuwa rubber stamp ya Serikali ulikuwa Kaburini au ndio unafiki uliotukuka plus mihemko ya kidini?Hakuna mwengine yeyote hadi sasa zaidi ya Mdee nae alisema kabla ya tamko la kijinga la Ndugai.