FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,776
Assad ni mtu pekee Tanzania hii ambae yupo serikalini lakini anaweza kuikosoa mihimili yote mitatu ya mfumo wa uongozi wa Tanzania.
Anaweza kuukosoa mhimili wa taasisi ya Urais kwa maana ya wizara na idara zote zilizo chini ya taasisi ya Urais. Anaweza kuukosoa mhimili wa bunge ikiwemo ofisi ya spika. Anaweza kuukosoa mhimili wa mahakama. Anaweza kuikosoa mihili yote hiyo kwa kutokusimamia matumizi mazuri, ubadhirifu, uvunjaji wa sheria na kanuni za matumizi na ndiye pekee anaweza kutoa maoni yake ya udhaifu uko wap na akasikika.
Assad majukumu yake hayaishii serikalini tu, ni mtu pekee anaeweza kuyafanya yote hayo juu kwa upinzani pia.
Kwa kutazama hayo kwa uoana wake, Assad ni mtu pekee anaeweza kuikosoa (kwenye usimamizi wa fedha) Jamhuru nzima ya Muungano wa Tanzania.
Hilo ni jukumu kubwa sana na lazima awe na maadui kutoka kila pembe.
Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania matumizi mabovu ni kila pahala.
Ni dhahiri hakuna mhimili usio mchekea usoni tu lakini akigeuka anasonywa.
Kwa hiyo tusitarajie mhimili wowote kumtetea Assad zaidi ya wachache wanaotaka kuona matumizi ya fedha zao yanasimamiwa vizuri.
Hili sakata la Assad ndiyo litatuonesha ukweli wa mambo ulivyo Tanzania.
Hakuna ataepinga kuwa kuna madudu mengi ya kifedha yapo serikalini na inawezekana kabisa kuwa madudu hayo yapo hata ofisi ya spika. Spika ameshindwa kabisa kuliendesha bunge kuwa wasimamizi wa serikali na kwa maana hiyo basi bunge limekuwa dhaifu.
Tutegemee nani wa kuwa upande wa Assad?
Bunge ni dhaifu.