KING ASSENGA
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 929
- 1,500
[emoji120]ni kweli
[emoji120]
HakikaUtu na ubinadamu naona ni mtu mwenyewe anaamua kuishi hivyo.
Dini zilitungwa ili kutawala wanadamu kwa kuwatia hofu na kuachana na maovu - so in this case you are right.Habari ndugu zangu. Wakubwa shkamoo......
Ushawahi kujiuliza maisha yangekuwaje bila Dini?
Leo nimewaza nikawazua na kuangalia mifano iliyohai kuhusu uhusiano uliopo kati ya mtu kuwa na roho ya utu au ubinadamu na Dini. Baada ya uchunguzi wa kina nimegundua bila Dini ubinadamu na utu vita toweka kabisa Duniani na hatutakuwa na tofauti na wanyama .
utu ni ile hali ya kutenda jambo kwa mwingine bila ya kutegemea malipo yoyote kutoka kwake. Hivyo ni jumla ya tabia njema anazopasa kuzionyesha mtu kwa jamii (hulka ya matendo mema). Source Wikipedia
Sasa Kwanini nina amini bila Dini ubinadamu au utu vitatoweka ? .
Sababu ya kwanza. Tumaini la maisha baada ya kifo. Bila dini hakuta kuwa na imani ya kuwa na maisha baada ya kifo.
Hii itaachia wengi walioshika dini kufanya maasi wakijua wote sisi mwisho ni kaburini . Bila shaka tungeuwana hovyo sana na kuumizana . Wengi wanaokamatwa kwa mauaji hukamatwa baada ya kuzubaa kutokana na dhamiri zao kuwa kinyume na walichotenda na hii ni sababu ya imani ya kidini. Bila dini hata sheria zisingeweza kuzuia watu Machafuko yangekuwa mengi sana . Mali zingepiganiwa mara 100 kuliko hivi sasa. Dini ikipotea kabisa ndani ya vichwa vyetu magenge ya mapigano yatakuwa mengi kuliko haiti [emoji1122] na nchi nyinginezo na ndio itakuwa namna ya kujilinda na kuweza kuishi kwa nchi nyingi.
Jiulize kwa hasira zako kama sio kuwa mcha Mungu mangapi mabaya ungetendea wengine haswa waliokukasirisha.
Bila ubinadamu na utu unaoletwa na Dini hakuna ulinzi utakaotosha kukulinda .
Sababu nyingine . Matukio mabaya kwenye jamii zilizo acha Dini. Bila kwenda mbali hebu fanya utafiti wako kwa kulinganisha mikoa ambayo dini imetamalaki sana na sehemu ambazo dini haieleweki imekaaje kwenye eneo hilo . Angalia takwimu za matukio kadiri muda unavyokwenda kutoka nchi za magharibi ata Asia kadiri wanavyozidi kuziacha dini matukio yanaongezeka au yanapungua?. Pia pitia historia kabla hizi dini mbili Ukristo na Uislamu kushika sana Dunia hali ilikuwaje . Mara nyingi vita kupinduana kwa mauaji vilishamiri kuliko hivi sasa na sasa ujuaji unataka kuongezeka tena . Dini zinaanza kuonekana ni ushamba kwa wasomi haina shida wao watapita salama ila ni hatari sana kwa vizazi vijavyo.
Njia salama ya kumwokoa mwanao na tabia hatarishi ni kumnywesha itikadi kali ya Dini.
Ukimwacha aje achague mwenyewe utampoteza kwani bila imani za dini basi hata ushoga na tabia chafu nyinginezo mashiko ya kuzipinga hayatakuwepo .
Maana ukigusia uumbaji tu lazima utagusa Dini. Ukisema tumetokana na sokwe sasa unampangia mtu kuwa unavyotaka wewe ili nini unamzuia asiwe shoga ili nini wakati wote tutaishia kaburini . Bila imani ya maisha baada ya kifo inakuwa sababu nyingine hazina nguvu. Itikadi kali ya dini itamlinda mwanao na kumpa Amani hata anapopitia magumu kiasi gani watu wote wampinge bado ataishi akiamini kuna Mungu.
Mwisho tusiache Dini ni ulinzi wa kizazi chetu na vizazi vijavyo.
Wewe unaonaje Dunia bila Dini ingekuwaje?
Bila Religion tungekuwa vikundi vidogo vidogo ambavyo bado uhasama baina ya vikundi utu na ubinadamu ungeondoshwaJifunze kutofautisha kati ya Spirituality na Religion.
Vita vya dini na dini ndio tatizo lakini kwa sasa tumeunganishwa na Dini zilizobeba idadi kubwa sana ya watu tofauti na miaka ya nyuma . DINI ZILIKUWA NYINGI SANA, MFANO NI KILA KABILA TANZANIA NA MILA ZAKE AU DINI YAKE ALAFU KILA MOJA LIJIONE BORA ZAIDI NA UTU UWE NI NDANI TU YA KABILA VITA SI ITAKUWA KILA SIKU.Historia inatufunza kwamba vita nyingi , mauaji makubwa , ukatili mkubwa katika historia umefanywa kwa mgongo wa dini na imani.
Hata ukisoma vitabu vitakatifu utakubaliana na mimi kuna mauaji mengi sana kwa mgongo wa dini na imani. Sasa ni juu yako kutumia akili kama dini ndio inasababisha mauaji na ukatili au ukosefi wa dini.
Hapana . Dini hazijatungwa . Kwa akili za mwanadamu Uzinzi usingewekwa kuwa ni dhambi maana hakuna uhusiano wa uzinzi na utuDini zilitungwa ili kutawala wanadamu kwa kuwatia hofu na kuachana na maovu - so in this case you are right.