Huwa siamini uganga aka uchawi hata siku moja, waganga ni watu wajanja saana, wanacheza na akili za watu tu, hakuna lolote.
Yaani wanachofanya ni kukuhoji tena kwa undani juu ya tatizo lako, mfano kuna jamaa yangu aliojiwa ye shida yake ni kupata utajiri, uone waganga walivyowajanja, alichofanya ni kumpa dawa na masharti tena ya ovyo tu.
Lkn akamwambia asafiri aende maeneo fulani anunue plot na alime vitunguu,jamaa akalima vitunguu vikakubali, akauza na kupata hela za kutosha, mambo yakawa mazuri akatajirika. Sasa ukiangalia hapa ni kwamba mganga alisoma tu mazingira na jamaa aka practice mambo yakawa lkn si kwasababu ya yale masharti au dawa alompa bali ni ule ushauri wa kumtaka akalime, ushauri ambao hata mtu mwingine angempa tena bila masharti, lkn wasiochanganya na za kwao wataamini ni dawa ndo imesaidia.