Hali ngumu ya kimaisha, vyakula bei juu, mtu anaandaa bajeti ya kula yeye na familia yake tu. Tena anataka ale mpaka abakishe na baade ale na kesho asubuhi ale kiporo chake kwa chai siku ipite. Hicho chakula cha kugawa mpaka kwa jirani atakipata wapi? Siku hizi hakuna kualikana kama zamani, hata ndugu yako wa karibu hakualiki. Ubinafsi nao umetawala, cha mtu, cha mtu tu. Maisha yamebadilika ndio maana hata hizi sikukuu wengi wameanza kuzipuuzia na kuziona ni kero tu za kuvuruga fedha za maendeleo yao ya maana na kujitakia stress bure.