Hakuna tena ndoa za "vijana" now days

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Kweli mambo huenda yakabadilika, zamani karibu asilimia 90 ya ndoa zote zilizo fungwa zilikuwa ni za watu kati ya miaka 20 hadi 25 na 30 kwa waliochelewa kuoa
Now days mambo ni tofauti kabisa, mwaka jana pekee nimehudhuria ndoa kama 10+ za ndugu, jamaa,marafiki nk karibu zote wanandoa walikuwa na zaidi ya miaka 35 hadi 45

Na kwa ujumla ndoa za sasa zimekuwa na sifa zifuatazo kwa wanandoa
Umri una range 30 to 45
Watakuwa "wanajuana" zaidi ya miaka kadhaa
Zaidi ya nusu walikuwa wanaishi pamoja kama mume na mke
Zaidi ya nusu yao tayari wana watoto wamezaa pamoja

Ukizingatia hivi sasa tafiti zinaonyesha ndoa za sasa hazidumu, mifarakano na kudanganyana zaidi yaani hamna uaminifu katika ndoa hizi, tofauti na ndoa za enzi zile zilikuwa zinadumu na maadili yalikuwa juu kuliko sasa

Je kuna uhusiano wowote wa ndoa hizi na mifarakano ya ndoa hizi?
Je ni nini haswa sababu ya mabadiliko haya
?
 
Nlifikiri ungesema hakuna ndoa za "watoto" siku hizi.

Miaka 30 mpaka 45 ndo ujana wenyewe huo sasa.

Source: CCM
Ushahidi: Wakati JK anagombea uraisi kwa mara ya kwanza walisema mgombea kijana.

Utafiti wa ODM unaonyesha kuwa ndoa zinazofungwa zikihusisha wanandoa ambao wamekwishajuana kwa muda mrefu ndo huwa zinadumu kuliko zile zinazowahusisha wanandoa waliokutana kwenye daladala.

Ushauri: Kabla hamjaoana hakikisheni mnafahamiana kwa kina kuanzia tabia, vikojoleo na hata uzazi wenu ikibidi.

Karibuni Tusker Malt hapa Fyatanga.
 
Mkuu ndio maana kwenye title nikaandika "ujana" kifasihi zaidi....
Lakini mkuu si inasemekana ndoa za sasa ni vimeo kuliko za zamani kwa maana ya kudumu
 
Sijaelewa huo "usasa" unamaanisha nini kiundani.

Lakini uzoefu wangu unaonyesha ndoa zile ambazo wanandoa washajuana saana ndio wakaamua kufunga ndoa huwa zinadumu kuliko zile za kujuana kwa muda mfupi afu mnakimbilia kwenye viapo. Mie mwenyewe nlipanda madhabahuni baada ya kulabuana na bibi yenu kwa zaidi ya miaka saba. Hakuna cha kututenganisha asee! Manake tulijiridhisha kabisa kwamba sisi ni sisi. Hakuna ku-fake hapo tena.
 
NB: Ndoa sio kwenda kanisani/msikitini/Mahakamani(bomani) au kwa wazee wa mila. Hizo ni "formalities" za kuhalalisha ndoa. Ndoa inakamilika pale mme na mke wanaporidhia kuwa kitu kimoja na kuanzisha familia, wakiunganishwa na watoto watakaojaliwa na Mwenyezi Mungu! Ndio maana ukienda kufunga ndoa baada ya kuishi na mwenza wako utasikia minong'ono: "ANAFUNGA NDOA NA MKE/MUME WAKE" na sio "MCHUMBA WAKE"
 
Ha haaaaaa. watoto wa mjini wanaita kupasha moto kiporo.........
Lakini mkuu hiyo tafsiri yako ya ndoa siipingi lakini ipo full utata

upatikanaji wa k umekuwa rahisi sana...zamani k ilikuwa mpaka uwe umeoa ndio wapata lakiini kwa sasa mtu anaweza kuchelewa kuoa huku akiwa ana gf ambaye anapozea chemchem za mwili wake.
na hii sio kitu kipya ilishaonekana toka muda kuwa watu wanao ishi pamoja kabla ya kuoana wana chance kubwa ya ndoa yao kutodumu kwa muda mrefu.
 
NB: Ndoa sio kwenda kanisani/msikitini/Mahakamani(bomani) au kwa wazee wa mila. Hizo ni "formalities" za kuhalalisha ndoa. Ndoa inakamilika pale mme na mke wanaporidhia kuwa kitu kimoja na kuanzisha familia, wakiunganishwa na watoto watakaojaliwa na Mwenyezi Mungu! Ndio maana ukienda kufunga ndoa baada ya kuishi na mwenza wako utasikia minong'ono: "ANAFUNGA NDOA NA MKE/MUME WAKE" na sio "MCHUMBA WAKE"

Uncle unajua unachokisema, 2 wrongs doesn't make it right.
 
Mimi nadhani ndoa kuvunjika ni kitu kidogo sana, haijalishi umewai kuishi kwa muda mrefu kabla ya kufuata formalities zote. India ni mmoja kati ya inchi ambayo rate ya divorce iko chini sana ukiliganisha na marekani. wanaoana wakiwa vijana wenye umri mdogo I meam 18+ and still ndoa zao zina dumu ukilinganisha na ndoa za kizungu+ za kibongo.
Zipo sababu za msingi:

1. kuto kufuata maadili yetu
sasa hivi watu wanaiga mambo yanayo onekena kwenye TV, BF and GF aya mambo hayakuwepo siku za nyuma, zamani mtu akitaka kuoa no lazima awashirikize wazazi wazazi walikunafanya BIOSELECTION i.e watatafuta msinchana mwenye tabia nzuru, mtulivu ambaya hana historia ya ugonjwa wa fafa n.k lakini leo hii watu wakikutana disco tayari wameshakua wanandoa.
Okey ukipata mchumba uwashirikishe wazazi wawe washauri basi, yaani uchague mwenyewe ila wazazi wawe washauri. hatuwafanyi hivi, sisi tunalazimisha na tunasema kipenda roho ula nyama ya tembo. matokeo yake ndoa zina vunjika kila kukicha. leo hii mahakamani kesi za ndoa ni kweli kweli. Biblia inasema muheshim baba yako na mama yako ili siku zako zipate kuongezeka. Baba na mama ni miungu wetu hapa duniani

2. watu hawamuogopi Mungu
Katika ndoa nyigi za siku hizi watu hawampi nafasi Mungu atawale ndoa zao, kwanza utakuta Mume ana dini yake na mume anadini yake na inawezekana kabisa wote wakawa hawana dini, hivo inapo tokea matatizo wanashindwa kuomba Mungu au wanashindwa kusameeana kabisa, unakuta wanakua sio waaminifu.

utakuta kwa wale walio makanisani wao wanakua ni hypocrite( wanafki), wakiwa kanisani wanajifanya ni wapole wana mpenda Mungu ila wakiwa manyumbani kwao ni tofauti.

3. wanandoa wengi siyo waaminifu
vijana wengi wanasema kwamba: utakulaje chakula kimoja siku zote?, wengine wameenda mbali zaidi wanasema ratio kati ya wanaume na wanawake TZ ni 1:3 wakimaanisha kwamba kila mwanaume 1 ni lazima awe na wanawake wa 3.
as the result watu wazinzi wakutupwa, simu inakua ni alama mmoja wapo ya kuonyesha kutokuaminia

4. Unafki ata mazabauni,
mnapo funga ndoa, kuna maneno ambayo tunakariri bila hata kujua madhara yake. I will be faithfull tou all the time in sickness or health, in thick and thin etc. untill dealth will separate us . maneno haya ndugu zangu watu ukariri tu, inapo fika wakati wa shida wanandoa wengi ukimbia ndoa zao, watu wanaficha hela zao hawataki kuwaonyesha wakezao, wanawake hawashauriki. kwa hiyo shida mtupu.

5. la mwisho kabisa ni kuto kusamee

Biblia inasema hivi, samee saba mara sabini kwa siku( Matayo 18:22), tunapo omba sala ya baba yetu tunasema utuasamee makosa yetu kama sisi tunavyowasamee waliotukosea.
wanandoa wanaweza kusamee kila kitu isipokua maswala ya uzinzi. wanakimbia andiko linalo sema usamee isipokua uwasharati. sio kweli watu upotosha tafsiri. YESU ANASEMA ATAKAMA MTU NI MZINZI NI LAZIMA USAMEE, usipo samee ata wewe hutosameewa.

"WAABUO ALISI WATAMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI" NA SIYO KWA UNAFKI. Mimi naamini tukimuabudu Mungu katika roho na kweli ata ndoa zetu zitadumu. vinginevyo ni kuishi katika mashaka, kutokuaminiana na kesi kila kukicha.

Source: My own obseravational research
 
upatikanaji wa k umekuwa rahisi sana...zamani k ilikuwa mpaka uwe umeoa ndio wapata lakiini kwa sasa mtu anaweza kuchelewa kuoa huku akiwa ana gf ambaye anapozea chemchem za mwili wake.
na hii sio kitu kipya ilishaonekana toka muda kuwa watu wanao ishi pamoja kabla ya kuoana wana chance kubwa ya ndoa yao kutodumu kwa muda mrefu.
Mkuu comment yako imenifanya nicheke peke yangu, hiyo sababu yako uliyotoa ngoja niifanyie utafiti
Lakini unapingana na mdau mmoja anadai eti ndoa za kujuana muda mrefu ndio zinadumu
 
Nlifikiri ungesema hakuna ndoa za "watoto" siku hizi.

Miaka 30 mpaka 45 ndo ujana wenyewe huo sasa.

Source: CCM
Ushahidi: Wakati JK anagombea uraisi kwa mara ya kwanza walisema mgombea kijana.

Utafiti wa ODM unaonyesha kuwa ndoa zinazofungwa zikihusisha wanandoa ambao wamekwishajuana kwa muda mrefu ndo huwa zinadumu kuliko zile zinazowahusisha wanandoa waliokutana kwenye daladala.

Ushauri: Kabla hamjaoana hakikisheni mnafahamiana kwa kina kuanzia tabia, vikojoleo na hata uzazi wenu ikibidi.

Karibuni Tusker Malt hapa Fyatanga.

Duh vp kuhusu vinyeo......
 
siku hizi,wanawake nao wana vipato vyao.ukileta za kuleta,na wao wanaweza.zamani mwanamme aki cheat,na kama akicheat inakuwa siri mno.siku hizi,wanaume wanafanya mambo hadharani.m.ke unavumilia,mwisho unashindwa
 
NB: Ndoa sio kwenda kanisani/msikitini/Mahakamani(bomani) au kwa wazee wa mila. Hizo ni "formalities" za kuhalalisha ndoa. Ndoa inakamilika pale mme na mke wanaporidhia kuwa kitu kimoja na kuanzisha familia, wakiunganishwa na watoto watakaojaliwa na Mwenyezi Mungu! Ndio maana ukienda kufunga ndoa baada ya kuishi na mwenza wako utasikia minong'ono: "ANAFUNGA NDOA NA MKE/MUME WAKE" na sio "MCHUMBA WAKE"
I totaly agree. Kumekua na uelewa mdogo kuhusu ndoa miongoni mwetu. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili wa jinsia tofauti, kuishi pamoja. Baada ya makubaliano hayo huishi pamoja na kuwa mume na mke na huzaa watoto na kutengeneza familia.

Hivyo basi, waweza kuitisha watu kushuhudia ambayo mnaita harusi au usite watu. Kwenda kanisani ni swala la imani na utamaduni. Pia waweza kusajili ndoa yenu mkuu wa wilaya ili kupata uthibitisho wa kidunia.

So kimsingi padre au shehe au mchungaji hafungishi wa kuhalalisha ndoa ila anasajili tu kama anavyofanya mkuu wa wilaya.
 
siku hizi,wanawake nao wana vipato vyao.ukileta za kuleta,na wao wanaweza.zamani mwanamme aki cheat,na kama akicheat inakuwa siri mno.siku hizi,wanaume wanafanya mambo hadharani.m.ke unavumilia,mwisho unashindwa
Mkuu inamaana akidada wa zamani walikuwa "maboya"
 
I totaly agree. Kumekua na uelewa mdogo kuhusu ndoa miongoni mwetu. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili wa jinsia tofauti, kuishi pamoja. Baada ya makubaliano hayo huishi pamoja na kuwa mume na mke na huzaa watoto na kutengeneza familia.

Hivyo basi, waweza kuitisha watu kushuhudia ambayo mnaita harusi au usite watu. Kwenda kanisani ni swala la imani na utamaduni. Pia waweza kusajili ndoa yenu mkuu wa wilaya ili kupata uthibitisho wa kidunia.

So kimsingi padre au shehe au mchungaji hafungishi wa kuhalalisha ndoa ila anasajili tu kama anavyofanya mkuu wa wilaya.

Mkuu ndoa ni tendo la kisheria, iwe madhabahuni,kwa mkuu wa wilaya au kimila zote ni ndoa
Ninachouliza mimi ni kwanini kitendo hicho miaka imepanda kuzingatia factors nilizotoa?
yaani kwanini mkae miaka 10 mpate na watoto ndio mkumbuke kuna padri au mkuu wa wilaya?
 
.
SI unit like this
 
Ok! Kama swali ni kukaa ten years, sababu ni nyingi ikiwemo ile ya kutaka kufanya sherehe kubwa ya kifahari, that is to say, kitchen party, send off, and wedding itself. Wengine wanachelea (sio kuchelewa) kwa sababu hiyo. But my poit should be the same, ndoa inakua imesha"takeplace" (coz tayari mshafanya tendo la ndoa, yamkini mmeshajaliwa na watoto) kinachobaki ni sherehe ya kushuhudiwa na watu wengi (harusi) kuthibitisha huo muungano wa mume na mke. Over!
 
Got you dude........ kwa hiyo sikuhizi harusi(sherehe) nikama fasion fulani hivi aka show
 
Back
Top Bottom