Hakuna Serikali inayosimamia Katiba asilimia mia moja duniani

Hakuna Serikali inayosimamia Katiba asilimia mia moja duniani

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Hakuna serikali inayosimamia Katiba yake kwa asilimia mia moja. Hakuna. Haijawahi kutokea na haitakuja kutokea. Kuna watu ambao kila siku ni kuikosoa serikali, yes ni haki yao. Hata wakikosoa mara trillion serikali haiwezi kufanya yote kwa kuwa serikali haiongozwi na Malaika. Binadamu ameumbiwa makosa.

Hata Marekani wanafanya makosa mengi ya kikatiba ndio maana kunakuwa na uchaguzi kila baada ya kiongozi kumaliza mhula wake. Viongozi wangekuwa wanasimamia katiba kwa asilimia mia moja na Ilani kwa asilimia mia moja basi kusingekuwa na uchaguzi. Uchaguzi unafanyika ili kushindanisha mawazo kuwa huyu alishindwa kufanya hiki, mimi mkinipa ridhaa nitafanya.

Tutambue kuwa makosa ndiyo msingi wa Demokrasia. Ukiona chama kinakaa muda mrefu madarakani basi utambue kuwa kwenye midhania ya unafuu, basi chama kinachoshinda kina uafadhali kuliko vilivyoshindwa. Ila kushinda kwa chama haimanishi ni kizuri kwa asilimia mia moja, bali kina ''UAFADHALI'' kuliko vingine.
 
Back
Top Bottom