Hakuna ndoa ya siri

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
Acha tufunge maneno vizuri leo.

Hivi unajua kuna watu wanaoa kama vile wanafanya biashara ya madawa ya kulevya? Yaani, kimyakimya, bila mashahidi, bila kujulisha hata mbwa wa jirani. "ndoa ya siri."

Sasa hivi bwana, kuna mtu anaweza kupata ndoa nyuma ya pazia alafu kesho anaanza kusema "Nimeoa," huku hata dada zake hawajui kama alitoa mahari au alienda kanisani/msikitini. Ukimuuliza anasema, "tulielewana, ndoa ni kati ya watu wawili." Hapo ndo unajua ulimwengu umeharibika.

Ndoa si kamchezo ka bahati nasibu. Ndoa ni heshima, inataka uiheshimu na uiheshimishe. Siri ni kwa mapenzi, si kwa ndoa. Ukioa kimya kimya, kesho utalia kimya kimya. Ukiolewa kwa siri, kesho ukiachwa huwezi hata kuandikwa WhatsApp status.

Jamii yetu inahitaji uwazi. Utu, siyo ughost.
Hakuna ndoa ya siri. Kama huna ujasiri, usiingie kwenye ndoa.

🖋️ Abuuabdillah
#Mahusianoseason
 
Kwamba ili ndoa itimie lazima dada zangu wajue?
Dada wanaingiaje katika misingi ya ndoa kutimia?
Au kwamba ndoa kutimia lazima iwe na makelele?
Tafsiri ya ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi(kwa wale.wanaofanya mitala).
 
tofautisha harusi na NDOA,.. ndoa ni ya watu wawili, heshima ya ndoa inatoka kwa watu wawili waliopo kwenye ndoa na sio walio nje,.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…