Hakuna mwanaume mbahiri mbele ya mwanamke ampendaye

Hakuna mwanaume mbahiri mbele ya mwanamke ampendaye

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,996
Reaction score
189,582
Habari za siku nyingi ni muda kidogo toka nipotee Jamii Forums. Na imani wote ni wenye afya njema.

Wanawake wengi wamekuwa wakisahau na kuona kama mwanaume fulani si mpambanaji au ameridhika na maisha ya kila siku kumbe hakuna kitu kama hicho.

Mwanaume anayejitambua kila siku hupambana kuweka misingi mizuri ya kimaisha kwa watu wote wanaomzunguka (familia, wazazi, rafiki, jamaa, nk)

Hakuna mwanaume anafurahia mwanamke ampendaye ahangaike kwa kitu chochote kile. (Mwanamke hajaumbiwa shida). Kama ni usafiri basi usidhani kama anafurahi wewe kila siku uangaike na Uber au daladala watu wakusumbue-sumbue, kukushika-shika, kukubambia-bambia kama zilivyo route za Mbagala - Buza.

Wanaume wanaumia moyoni kukuona ukiteseka hivyo ila huku wakipambana. Pia unaweza kuona mbona kama anaweza kukununulia hata ki-IST ila yeye hawazi hapo anawaza kuweka misingi mizuri upate hata ki-crown /x3 cha kutembelea suala tu baadae utoke katika hatua hiyo ya sasa.

Kama amepanga basi mwanaume anapambana atoke kwenye hiyo hali kila kuitwapo leo. Mwanaume hapendi hata kidogo kuona unanyanyasika. Maana kero za nyumba za kupanga kila mtu anafahamu vizuri.

Kwa wale wa uswahilini hapendi kuona unahangaika na zamu za kudeki vyoo mara hii mara lile. Wenye nyumba wanaizingatia sana nahau hii 'cha mtu mavi' sasa hapa wanaona wapangaji wote ni waharibifu.

Hivyo basi kimya cha mwanaume si amekubali hayo maisha ila nakuhakikishia kila siku anapambana mtoke kwenye hiyo hatua usilazimishe sana ukamuharibia malengo.

Hakuna mwanaume anapenda wewe mwanamke siku ya harusi yako usifurahi. Kila mwanaume anataka kwenye siku yako special ya ndoa ufeel kweli ni harusi. Mwanzo na haraka haraka unaweza kuhisi kama anataka kukuchezea na hataki kukuoa ila nakuhakikishia kama anakupenda kweli anatengeneza mazingira mazuri ya hiyo harusi nakupa moyo we endelea kuwa mvumilivu.

Hakuna mwanaume anapenda watoto wake waje wateseke kwa kukosa elimu iliyo bora. Unaweza kuona kila siku kama anakwepa majukumu ila nakuhakikishia yupo anapambana kuweka mazingira ambayo watoto wakipatikana waishi mazingira bora.

Mwisho kwako wewe mwanamke usiwe mpumbavu (Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe) jua kusoma nyakati usiwe mfuata upepo usikiapo kupiga vizinga ndio habari ya mjini ukaangukia kuharibu mipango yote ya mwanaume akupendae na kuambulia patupu ukusubiri upepo wa kisulisuli kuona mwanaume huyo hafai. Wengine wanaona kama mwanaume ni mbahiri au hamjali.

Ila ukweli ni hakuna mwanaume mbahiri.

Kila kwenye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke.

Sasa jiulize huyo mwanamke ni wewe?

Nawasilisha.


Cc. Kichwa Kichafu
 
(Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe)

Kila kwenye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke.

Ukweli mtupu/ukweli pekee bila uongo.

TAHADHARI: Mabaharia mnaohustle mkiwa sambamba na wake zenu, baadae mkafanikiwa halafu ukaamua kumuacha huyo mke wako kisa umepata jeuri ya pesa na ukaamua kutafuta mwingine. MUACHE HIYO TABIA.
 
Kumbuka: Pata pesa tujue tabia yako!
Ukweli mtupu/ukweli pekee bila uongo.

TAHADHARI: Mabaharia mnaohustle mkiwa sambamba na wake zenu, baadae mkafanikiwa halafu ukaamua kumuacha huyo mke wako kisa umepata jeuri ya pesa na ukaamua kutafuta mwingine. MUACHE HIYO TABIA.
 
Daaaaaah we jamaa umetoa madini mazito sana ambayo wengi huwa tunashindwa kuwaambia hawa warembo.

Yani tatizo tu ni kwamba wengi wao wanataka yani ile upo kwenye hatua za kumtongoza basi mkononi uwe na ufunguo wa gari mkononi,

yani wanawake wanafeli mahali padogo sana mpaka ipelekea wengi kujikuta wanaharibu jumla jumla mipango na mitiririko ya maisha yao kwa kuhutaji maisha mazuri kwa haraka na kwa kuiga marafiki zao......
 
Teh teh teh ni msemo tu mkuu. Popote pale mwanaume unapokuwa jua wewe ndio mtatuzi wa changamoto yeyote ile.
Usitegemee kama kwenye familia/mahusiano mwanamke ndio awe mtatuzi kwako utaishia pabaya.

Mwanamke uhitaji mazingira mazuri na sio karaha(shida).
"Mwanamke hajaumbiwa shida? " Sijaelewa una maan ipi
 
Wanahisi kama kila siku utakuwa na maisha hayo hayo.

Daaaaaah we jamaa umetoa madini mazito sana ambayo wengi huwa tunashindwa kuwaambia hawa warembo.

Yani tatizo tu ni kwamba wengi wao wanataka yani ile upo kwenye hatua za kumtongoza basi mkononi uwe na ufunguo wa gari mkononi,

yani wanawake wanafeli mahali padogo sana mpaka ipelekea wengi kujikuta wanaharibu jumla jumla mipango na mitiririko ya maisha yao kwa kuhutaji maisha mazuri kwa haraka na kwa kuiga marafiki zao......
 
Natamani nioe mwanamke mwenye kigugumizi, ili Kabla hajaniambia "baby naomba hela nikasuke", Huyoo nishakimbia kwenda kazini.


Ubahili duuuh.
Aisee. Kwenye pesa hata vigugumizi vinajificha mkuu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom