Hakuna mtu aliye juu ya Taifa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,243
2,000
"(MKAPA: HATA WABAYA HUOMBWA KUENDELEA"

Tunaendelea na maombolezo ya kifo cha Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa. Yamesemwa mengi na kuandikwa mengi. Yeye hasikii kinachoendelea. Lolote laweza kusemwa na hawezi kukanusha. Hata mimi nimesema na kuandika. Katika kila msiba kuna "kulia vibaya na kulia vizuri".

Katika fursa adimu nilizopata kujadiliana na hayati Mkapa, tulijadili mambo mawili ambayo napenda niwamegee.

1. Jaribu la kuongeza muda wa urais: Tulichambua jambo hili kwa mifano kadhaa. Nilijaribu kumshawishi kwa hoja kuwa maono huanza na mtu. Akakubali. Kisha nikampeleka kwenye kona kuwa kwa kuwa maono huanza na mtu, kwa nini mtu huyo asiachwe ofisini hadi akamilishe maono yake bila kujali ukomo wa kikatiba? Alinijibu kuwa "hata marais wabaya huwa wanaombwa kuongeza muda". Aliendelea kutetea hoja yake kuwa, wanaomuomba rais aongeze muda huwa hawawezi kumwomba aondoke endapo anafanya vibaya. Akanieleza kuwa marais wa awamu zote hapa nchini waliombwa waendelee hata baada ya muda kukaribia kwisha. Alimalizia kwa kusema, "uzuri wa rais huonekane kwa kuheshimu katiba".

2. Ukuu wa serikali: Rais Mkapa aliheshimu kwa kina ukuu wa dola (muunganiko wa mihimili mitatu). Naweza kusema, baada ya Mungu, aliiheshimu serikali. Alikuwa mtiifu, msikivu na mfuasi wa dola. Hata alipooona sababu ya kutofautiana nayo (kama ilikuwa lazima), alilazimika awaone wahusika kuwaambia maoni yake. Yako mambo aliyokuwa akinung'unikia kwa hoja nzito. Lakini kwa uchaji (devotion) wake kwa dola alikuwa anaweza kuyasema ama akakatisha asimalize, au akayasema lakini akayapuuza kuwa ni fikra zake za "kizee". Alifanya hivyo wakati wote kuonyesha utii wake kwa dola.

Katika kusisitiza msimamo huu, siku moja alituambia na "wenzangu" tukiwa meza ya chakula kuwa "ukiri" wa kila siku wa Ikulu unasema, "hakuna mtu aliye bora kuliko taifa" (No person is so more important than a nation). Alipinga kwa nguvu zote mtu aliyekuwa anatishia kuhujumu (blackmail) nchi kwa sharti la yeye kupewa heshima au kusikilizwa ili asitoe siri inayoweza kudhalilisha nchi.

Aliyasema haya akilishauri kanisa lisikubali kumdekeza mtu aliyetishia kanisa kuwa atatoa siri za kanisa hadharani endapo matakwa yake hayatasikilizwa. Mzee Mkapa alitushauri kwa kusema " mwache aseme kwanza ndipo mpatane naye". Kisha akahitimisha, "msipofanya hivyo tutajua kuna mambo huwa mnafanya huko kanisani".

Katika mjadala ulioendelea siku nyingine, Mzee Mkapa alisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya taifa. Alitoa mifano ambayo si busara kuisema hapa. Natamani ukuu wa taifa ungekuwa wa kwanza kuliko ukuu wa dola. Naelewa wapo wanaotofautiana nami katika hili. Ni ruksa. Historia itaamua siku moja.

Kutoka kwa Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza
 

Sauti ya Mamlaka

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,316
2,000
We will miss him so much ila hapo kwnye kuongeza mda ngja tusubiri muda utaongea kama wataheshim katiba au la muda ni shahid mzur
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,997
2,000
Zambia walimzuia raisi wao kujiongezea muda. Hivyo kama watanzania wataacha ukondoo wao hilo linawezekana kushikilia katiba ifuatwe.
La mtu kuwa juu ya taifa kwa Tanzania hali hiyo ipo na inaletwa na katiba mbovu mpaka tunatakiwa kuwa na sauti moja tu ambayo ikipenda inavunja katiba kwa kutumia vyombo vya dola na wengi wetu tunafukia vichwa vyetu ardhini misili ya yule ngamia. Ukondoo wa Nyerere hapa unatutesa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom