hakuna msamaha wa namna hii katika mapenzi

hakuna msamaha wa namna hii katika mapenzi

fierceman

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
553
Reaction score
758
unagombana na mpenzi wako inafika hatua mnaachana na kisha unamuomba akusamehe pale ulipo mkwaza na kuomba mrudiane lakini yeye anasema amekusamehe lakini hawezi kuwa na wewe tena kwenye mahusiano...ukijibiwa hivyo jua bado haujasamehewa kwa maana hauko nae tena kimapenzi...ndugu tujifunze kusamehe kweli na si kuact umesamehe kumbe hapana...nawasilisha
 
Amesamehe kwa maana ya kuachilia yaani hana kinyongo na wewe ,si kimapenzi
hapo bado hajasamehe kwa maana ni kipi au kwanini sasa asirudiane kimapenzi na mtu wake wakati huyo mpenzi wake anahitajikurudiana tena?
 
hapo bado hajasamehe kwa maana ni kipi au kwanini sasa asirudiane kimapenzi na mtu wake wakati huyo mpenzi wake anahitajikurudiana tena?
Umekosea, ukaomba msamaha kwa kosa ulilofanya. Amekusamehe kosa hilo. Ila hawezi kurudiana nawe, hapo inabidi umuulize sababu za yeye kutotaka kurudiana nawe maana yawezekana isiwe kosa hilo.
 
Umekosea, ukaomba msamaha kwa kosa ulilofanya. Amekusamehe kosa hilo. Ila hawezi kurudiana nawe, hapo inabidi umuulize sababu za yeye kutotaka kurudiana nawe maana yawezekana isiwe kosa hilo.
sasa nitaelewaje kwamba amekataa kurudiana nami kwa kosa lingine na si hilo wakati ameamua kutorudiana nami baada ya hili ambalo kanisemehe? Na kama ni hivyo basi asamehi bali anaweka maumivu moyoni kwa maana msamaha ni kusahau ubaya
 
Pamoja nakwamba, kusamehe ni pamoja na kusahau yalopita.

Bado hakumfani mkosewaji arudiane na mkosaji hata km atakua kakusamehe
 
kuna mambo huwezi lazimisha.....kusahemeh ni kusamehe....kurudiana ni suala lingine .....anza upya blaza...
 
Back
Top Bottom