mary mary
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 869
- 287
Zitto Kabwe
"Kaliua-Tabora imetupa heshima kubwa sana CHADEMA. Tumefanya mkutano mkubwa na wa kihistoria. Tumezungumzia masuala ya kero za wakulima wa tumbaku na hasa dhuluma wanayopata. Tumezungumzia umuhimu na uharaka wa wao kujiunga na hifadhi ya jamii ili kujikomboa, kupata mafao ikiwemo mikopo nafuu ya pembejeo na kujiwekea akiba. Tumewapata taarifa fupi ya ziara yangu katika nchi za Ulaya kufuatilia sakata la wanaotorosha na kuficha fedha nje.
Tumewahakikishia wananchi kuwa CHADEMA hakuna mgogoro wowote ukiachana na makundi ya wahuni wanaotumwa kwa malengo maalumu ya kutuondoa kwenye reli ya kazi za ujenzi wa chama na kupambana na CCM. Watu wanaosambaza kashfa za uzushi na kutunga hekaya za abunuwasi wana malengo maalumu tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa chama.
Nimewaambia watu wa Kaliua "ukiona kifaranga kipo juu ya chungu ujue chini kuna mama yake"
Chanzo: FB
-----------------

Akiwahutubia Wananchi wa Kaliua leo Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe ameonyesha kushangazwa kwake na kusikitishwa na uongo na uzushi unaofanywa dhidi yake na zaidi na watu wanaojidai kuwa ni Wanachadema pia.
Zitto amesema wakati huu ambao yeye amekuwa akihangaika kufuatilia watu na makampuni yaliyoficha fedha nje ya nchi vita ya kisiasa dhidi yake imezidi kuwa kubwa ambapo CCM, Matajiri hao na hata wanaCHADEMA wamekuwa wakimpiga mishale mingi ili kummaliza nguvu. "Mimi ni binadamu nikifinywa naumia, nikipigwa mishale pia naumia tusiruhusu watu waturudishe nyuma katika mapambano kwasababu ya maslahi yao" Alisema Zitto
Zitto aliongeza demokrasia ndani ya CHADEMA iko tangu siku nyingi ambapo mwaka 1995 Mzee Mtei alishindana na Mzee Bob Makani katika kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA lakini baadae waliamua kumuunga mkono Mrema. Mwaka 2000 Mzee Makani aligombea Uenyekiti akichuana na Mzee Ndesamburo na Makani kushinda lakini Chama kilikuwa pamoja. Kwanini yeye kugombea Uenyekiti 2009 iwe nongwa?? Alihoji!
Mnakumbuka Marando alivyoitwa Shushushu? Marando alinuka nchi nzima lakini leo Marando yuko wapi? si CHADEMA? Na ni Mwanasheria wetu kwa sasa.