Hakuna Laigwanani Mkuu Afrika Mashariki

sanif

JF-Expert Member
Mar 15, 2016
480
324
MALAIGWANANI wilayani Monduli, mkoani Arusha wametoa rai kwa wenzao wanaoingiza masuala ya siasa kwenye mila za kabila la Kimasai kuacha mara moja. Aidha wamesema hawatambui uteuzi wa Laigwanani, Mepukori Mberekei kuwa Mwenyekiti wa Malaigwanani, wilayani Monduli wala hakuna cheo cha Laigwanani wa Afrika Mashariki.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana wilayani Monduli Juu eneo la Oloponi wakati wa kumsikimika Laigwanani mpya, Kibori Ngilepoi, malaigwanani hao zaidi ya 98 walisema wanamtambua Ngilepoi kama Mwenyekiti wa Malaigwanani.

Alisema hivi sasa kuna baadhi ya Malaigwanani wameunda kikundi kinachoingiza masuala ya siasa katika mila ambazo si rahisi kuingiliwa. Akisoma tamko hilo jana, Sungura Mang’aro alisema siasa hazipaswi kupewa nafasi na kuingizwa katika mila, hivyo Malaigwanani hawatambui cheo cha Laigwanani wa Afrika Mashariki na wala hawana cheo hicho hivyo hawamtambui Mberekei kama Mwenyekiti wa Malaigwanani bali wamemsimika Ngilepoi kuwa Mwenyekiti wao.

“Hatutaki siasa kuingizwa katika mila zetu na hatumtambui Mberekei kama Mwenyekiti wetu ila leo tumempa baraka yote Laigwanani Ngilepoi kuwa Mwenyekiti wetu na tumempitisha kwa kauli moja mbele ya Malaigwanani zaidi ya 98,” alisema.

Malaigwanani hao pia walimuombea Rais John Magufuli Mungu amlinde na kumuepusha na mambo mabaya kwani kazi anayoifanya hivi sasa ni kutetea wanyonge na kuhakikisha kila mtu anamheshimu mwenzake na kumfananisha Magufuli na Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Sokoine kwa kufanya kazi iliyotukuka.
 
Watu wanapenda vyeo hadi wanajiundia vyeo ambavyo havipo,aibu
 
Jamaa kaanza kukataliwa Chimwaga 1995 enzi za Mwl, akakataliwa kwny Cabinet ya kwanza ya Che Nkapa Dec, 1995, akataliwa Bungeni 2007, akataliwa na Mzee wa Msoga rasmi 2011, akataliwa na Kamati ya Maadili July, 2015, akataliwa na Rais wa Mioyo ya Wanachadema Dr Slaa, akakataliwa na Watanzania October 2015 na sasa 2016 anakataliwa Umasaini. Kweli Jamaa ana nyota ya Mkasi
 
Jamaa kaanza kukataliwa Chimwaga 1995 enzi za Mwl, akakataliwa kwny Cabinet ya kwanza ya Che Nkapa Dec, 1995, akataliwa Bungeni 2007, akataliwa na Mzee wa Msoga rasmi 2011, akataliwa na Kamati ya Maadili July, 2015, akataliwa na Rais wa Mioyo ya Wanachadema Dr Slaa, akakataliwa na Watanzania October 2015 na sasa 2016 anakataliwa Umasaini. Kweli Jamaa ana nyota ya Mkasi



Mhhh, kweli, kama Microsoft word art, nimeipenda hiyo ila napita tuu
 
CCM waache kuchochea udini ,ukabila na ukanda.

Tena nimshauri Mh. Magufuli asikubali kabisa kuingizwa kwenye ujinga wa kuwagawa watanzania.

Yanayotokea Zanzibar yanatosha tusianze tena kuleta chokochoko kwenye mambo yasiyo na tija.
Nyerere alifuta huu ujinga wa viongozi wa Makabila lakini naona bado tu kuna watu wanawatumia kufanya chokochoko. Kila jambo CCM inataka lifanyike kwa kuinufaisha tu.
Leo hii hata kikitokea kikundi cha dini kikiisifia CCM na viongozi wake hutasikia matamko ya kusema dini inajiingiza kwenye siasa lakini tamko likamsifu kiongozi wa upinzani basi itakua ni kelele na vitisho vya kila aina.

Kuheshimu mawazo ya watu alimradi hawavunji sheria.
Leo hii Matamko ya wazi ya kusema eti Lowasa sio mmasai ni Mmeru yanaleta ubaguzi wa wazi.
Leo hii ukimwona Mmarekani mweusi huwezi kumwita mwafrika akakuelewa. Wale ni wamarekani weusi. Na sio waafrika wa Marekani.
Tunao Makabila mengi sana ambayo yana watu ambao waliingizwa kwenye makabila hayo kutokana na historia na viapo walivyokua wamefanya na wazee wa mila kwenye makabila hayo na mpaka leo wameingizwa kwenye koo za makabila hayo.
 
Back
Top Bottom