Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 7,383
- 12,063
Habari za Jumapili,
Nimekaa na kutafakari sana juu ya Bara la Africa na watu wake, Nimegundua, asili yetu sisi africa ni kuishi kwa unyenyekevu na kumpa mgeni kipaumbele pengine kuliko hata sisi wenyewe
Hili linajionyesha wazi kuanzia ngazi za familia, Mfano, imezoeleka mgeni anakuja nyumbani kwako kukutembelea ni lazima umpe kipaumbele kwenye kila kitu, Kama utachinja kuku basi mgeni atapewa paja au kidari, na kuna vyombo maalumu vimenunuliwa kwa ajili ya wageni, Fridge inakua tupu mpaka wageni wakija ndo kunajazwa vinywaji wakiondoka bado watapewa vitu vya kwenda kutumia huko nyumbani kwao, Kwa mwenyeji mgeni akiondoka tuu anarudia maisha yake ya kawaida ya kuishi kwa kujinyima
Hali hii imevuka kutoka ngazi ya familia sasa ipo mpa kwenye mamlaka za nchi, ni kawaida kuona wageni kutoka nchi mbali mbali wakija kutembelea treatments wanazopewa ni hadhi ya juu kuliki mzawa, Tumeshuhudia baadhi ya Ma rais wakija hadi barabara zinafanyiwa usafi na vitu vingine vya kuonyesha kumthamini mgeni, hii inadhihirisha wazi kuwa sisi tumeshajiona hatuna thamani kama waliyonayo ngozi nyeupe, Matokeo yake hata katika fursa za uwekezaji mgeni anapewa masharti rahisi, uhuru na support kubwa pindi anapotaka kufanya jambo lake, huku wazawa wakiendelea kupigika,
Kwa mtazamo huu wala tusishangae kila siku tukiendelea kubaki nyuma, na kuonekana wasindikizaji kwenye kila jambo
Mgeni anapaswa kupewa treatment sawa na mzawa. Ukiona hata nyumbani kwako mgeni akija unampa treatment nzuri zaidi ya wewe mwenyewe basi tambua fika una umasikini wa fikra
Africa ndo sehemu pekee ambayo mgeni ana uhakika wa kupata treatments nzuri kuliko anapokua kwake