Hakuna kazi rahisi duniani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Huyu shost mtoto mashalaah kaumbika sura mpaka umbo. Ingawa alizungusha form six lakini baada ya boss kufahamu kuwa ana shida ya ajira ziliachwa division II shost akaingia. Kwa muda mrefu amekuwa small house ya boss mpaka pale best wa boss aliporudi kutoka masomoni Canada. Boss alimkaribisha best mjini na kumtambulisha kwa small house. Boss Alipo kwenda msalani best aliomba digits za shemeji yake.

Best alimpigia mtoto simu akamuweka sawa. Mtoto kama wewe utatokaje na mume wa mtu? Shost mwenyewe alijiona soo. Any way best alikuwa serious na baada ya miezi sita ya weekends nyingi tu za Zenj na Bagamoyo alinunuliwa pete yenye kito cha Tanzanite akawa engaged.

Baada ya kufanikiwa kupata kiwalo safi pale Tandale nilitinga harusini. Bibie aliachishwa kazi mara tu baada ya kuanza kutoa uroda kwa best wa boss. Sasa ni mke wa mtu amefunguliwa biashara ya kuku wa kisasa hao mnao waita wa wanyama na wa mayai.

Mwanzoni shost alikuwa na maneno eti mimi siwezi kuajiriwa kheri nijiajiri mwenyewe. Mmh ni kwakuwa ulizungusha shost!

Basi mauzo ya kwanza aliyafanya jana. Pesa alipata lakini mgongo unauma mbaya. Anasema kuwafuga tangu kifaranga ni kama unalea mtoto mchanga. Hawana maji uongeze, kuna baridi usiku weka taa yenye koti. Shost anatafuta acupuncture ya Kichina atibu mgongo.
 
Mwanzo mgumu, atazoea kazi kidogo kidogo, changamoto zipo lkn zinapungua uzito siku baada ya siku.

Akitaka kufanikiwa zaidi ajitahidi kuipenda kazi yake hii mpya. If you love what you do, you win.
 
Mwanzo mgumu, atazoea kazi kidogo kidogo, changamoto zipo lkn zinapungua uzito siku baada ya siku.

Akitaka kufanikiwa zaidi ajitahidi kuipenda kazi yake hii mpya. If you love what you do, you win.
Aajiri pia mtu wa kuangalia kuku usiku
 
Aajiri pia mtu wa kuangalia kuku usiku
Fact[emoji115]

Bora kazi hii atakuwa na uhuru kwenye kazi yake na uhuru kwenye familia yake kuliko kuishi kama small house.

Maisha mapya ni magumu lkn atazoea, kazi ya mwanzo (ya kutumika) ni NGUMU kuliko kazi ya sasa ni RAHISI ukilinganisha na ya mwanzo.

Option zipo nyingi, ikishindikana kabisa anaweza kuwa house mama tu au akabadili kazi(biashara). At the end Life goes on
 
Huyu msomi wa Canada inaelekea si wa kutoa hela za kununua kiss by Wema (lipstick).
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…