Hakuna jipya CCM kuhusu ufisadi tuandike tumeumia

Ndugu wanajamvi habari ya mda huu?

Kwa masikitiko makubwa niseme kwa wazalendo wa nchi hii wanaopenda kuona nchi yetu inasonga mbele tuandike tumeumia kwa hakika. Nasema haya kwa hoja kuu mbili

Moja tuanzie bungeni wiki iliyopita wabunge wa ccm wamehongwa mil. 10 kila moja rais alipoulizwa majibu yake tunajua wote alivyojibu

Pili rais amesema hafukui makaburi mana yake kuhusu escrow, epa, lugumi, iptl,tangold, meremeta, richmound nakadhalika hatagusa. Sasa kuna jipya gani?

Kwa muhtasari huu magufuli amedanganya watanzania wakamwamini kumbe yeye hakuwa na nia ya dhati kushughulikia uozo huu mkubwa je nani anafungwa kama ufisadi wote huu hakamatwi mtu

Tuandike tumeumia wenye akili wataelewa maana ya maneno haya watanzania tusitegemee mapya kutoka ccm kwa kuwa ufisadi ni ccm na ccm ni ufisadi ni sawa na mtoto kumkana baba yake ni kitu haiwezekani
Vipi ulipata mgao wa 10bln?
 
"Pili rais amesema hafukui makaburi mana yake kuhusu escrow, epa, lugumi, iptl,tangold, meremeta, richmound nakadhalika hatagusa. Sasa kuna jipya gani?"

Jamaa panda milima aliingia madarakani kwa mbwembwe nyingi, mipasho kedekede, na nguvu ya coca~cola akitumia kibwagizo kikali cha KUTUMBUA MAJIPU. jpm: 'Nitumbue, nisitumbue?' ; walalahoi: 'tumbuaaaaa baba!". Basi walalahoi tukafarijika sana kwamba watu wote tutaisoma namba. Baada ya mwaka mmoja, mtukufu chaguo la Mungu, Rais wa maskini, shujaa asiyejaribiwa amesalimu amri - chezea Lugumi wewe, jipu liloota pabaya!!
 
Tena cdm njaa yao ni mbaya.
Kwa sasa hakuna.atakayedhubutu kutamka neno ufisadi, bosi wao na.mfadhiri wao.atakata mrija
Watanzania tumieni kichwa kufikiria, inasikitisha sana. Tunasikitisha jinsi JPM anavyojiapiza kulinda mafisadi wanaotafuna nchi mpaka sasa na wanaendelea kutafuna nchi kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji wengine mnaleta ushabiki wa ki@#&*%# wa kivyama.
 
ongea hoja iliyopo mezani wew unaona ni siwa wabunge kuhongwa ili mswada upite sio ukiacha cdm mana hao baada ya kujiridhisha kuwa lowasa hakuwa mwizi ila mwizi ni bosi wake ndo wakampokea

Hili la wabunge kama ni kweli hata mimi limeniumiza sana roho...mafisadi ni wajanja sana wakitaka kukufunga mikono na mdomo wanakutafutia washauri then wanakushawishi utende dhambi kama yao ili kupata moral egualness(sp) ukisha ingia king ndiyo hivyo unaanza ku compromize...Lord Jesus let it not be true...
 
But I still hold my promise yeyote atakaye compromize wont stand the test of time...its a convenant I made which none can break mpaka ile njema ipatikane...
 
Mkuu, anayetawala nchi hii ni ccm, tusizoee kuwa kila watawala wanapokosolewa tunakimbilia kujificha nyuma ya vyama ambavyo havijashika dola. Na ni vizuri tukumbuke kuwa mamilioni ya raia wa nchi hii si wanachama wa chama chochote cha siasa. Kwa hiyo kwa mfano nikihoji madudu ya watawala, usiniambie kuhusu NCCR, CHADEMA, CUF, ACT nk. Kwa sababu vyama hivyo havitawali nchi hii. Na pia mimi siyo mwanachama wa vyama hivyo.
Lakini nia yao si ni kushika dola na kutawala? Wanatakiwa wapigwe kurunzi hata kabla hawajashika dola ili tufahamu tusije tukaruka maji tukaenda kukanyaga moto.
 
Lakini nia yao si ni kushika dola na kutawala? Wanatakiwa wapigwe kurunzi hata kabla hawajashika dola ili tufahamu tusije tukaruka maji tukaenda kukanyaga moto.
Mkuu sina tatizo na wao kupigwa kurunzi. Kasoro kubwa ninayoona ni pale kila unapotajwa uovu wa watawala, baadhi humu wanaibuka na porojo za 'hata ACT, CUF, CHADEMA nk.....blah blah blah!!!' Hivi kweli mkuu, watawala ambao wameapa kuilinda nchi yetu halafu wakashindwa ku-deal hata na ESCROW au IPTL ambayo imeitafuna nchi hii kwa zaidi ya miaka ishirini wasihojiwe kwa kisingizio cha CHADEMA au CUF?! Nchi inaporwa wao wako pembeni kama vile haiwahusu halafu kuna watu wanataka wasisemwe! Sheria zinatumika dhidi ya wanyonge lakini ikitokea watawala au ndugu zao wamefanya makosa yaleyale inatumika nguvu kubwa kutetea na kufunika uozo badala ya kuwajibisha wahusika! Wapi LUGUMI???
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?
bora fisadi wa jana au fisadi wa leo?
 
Fisadi mkuu LOWASSA kuondoka tu CCM ni vita moja tosha dhidi ya ufisadi. Waulize Chadema hivi sasa agenda yao kubwa ni nini kama siyo kupinga udikteta wa kufikirika(imaginary dictatorship).
 
IMEFIKIA WAKATI SHERIA YA KUNYONGWA, HASA KWA HAWA MAJAMBAZI(WAHUJUMU UCHUMI), MAJANGILI NA WAUZA MADAWA YA KULEVYA IPITISHWE ILI HESHIMA IRUDI MAHALA PAKE KAMA JAMHURI YA WATU WA CHINA, HAIWEZEKANI BAADHI YA WATANZANIA WANAISHI MAISHA MAGUMU SANA SANA, HALAFU KUNA WATU WANAISHI KAMA MIUNGU KWA UUNGU WALIOUTAFUTA KWA UNYONYAJI NA UJAMBAZI HAIWEZEKANI HII,,HAIWEZEKANI KABISA!!
 
Back
Top Bottom