Tundu Lissu unasema CCM haipambani na ufisadi, vipi kuhusu chama chako huoni ufisadi uliofanyika unakutesa?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Tundu Lissu umesikika mara kwa mara ukisema kuwa Ccm haipambani na ufisadi na unatoa mfano kuwa Deodatus Mwanyika alishitakiwa kwa makosa ya kifisadi tisini na mbili na sasa anagombea ubunge kupitia Ccm. Na wewe ndio unasema hii ndio sababu ya wewe kusema kuwa CCM haipambani na ufisadi

Wewe ni mwanasheria tena nguli unayekubalika kwani hatua za Deodatus Mwanyika kukamatwa na kuwekwa ndani kwa kosa la kusaidia Accacia kutolipa kodi sio hatua za kupambana ufisadi? Adhabu aliyopewa na wezanke ya kulipa bil 1.5 au kutumikia kifungo cha miezi minne inamuondolea sifa ya kugombea ubunge?

Kama ni ufisadi umesahau kuwa Chadema ina kashfa kubwa sana ya ufisadi? Mwenyekiti wa Chadema alikwapua pesa zaidi ya bil 8 ambazo zilikuwa zitumike kwa ajili ya uchaguzi mwaka huu. Fedha hizi ni michango ya wabunge waliokuwa bungeni kwa tiketi ya Chadema. Je wewe kama mgombea unayejinasibu kupinga ufisadi umechukua hatua gani kumhoji Mbowe zilipo hizi pesa?

Maana unafanya kampeni kwa tabu,unachangisha watu wakati kumbe wewe mwenyewe unafahamu kuna ufisadi mkubwa uliofanyika ndani ya chama unachokiwalisha kugombea urais. Na kama huu ufisadi usingefanyika ungefanya kampeni kwa urahisi bila kupitisha bakuli na mabeseni kwa watanzania ambao wewe mwenyewe unasema wana hali mbaya ya kiuchumi. Kwa hiyo wakati unaendelea na kampeni jaribu kumuuliza chairman mbowe ziko wapi bil 8 alizochangisha wabunge? Kama zipo zikusaidie kufanya kampeni kwa ufanisi.
 
Chadema wamefanya ufisadi gani? Ni mahakamani ipi iliyothibitisha hayo na kina Nani wamefungwa?
 
Back
Top Bottom