Hakuna jipya CCM kuhusu ufisadi tuandike tumeumia

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Ndugu wanajamvi habari ya mda huu?

Kwa masikitiko makubwa niseme kwa wazalendo wa nchi hii wanaopenda kuona nchi yetu inasonga mbele tuandike tumeumia kwa hakika. Nasema haya kwa hoja kuu mbili

Moja tuanzie bungeni wiki iliyopita wabunge wa ccm wamehongwa mil. 10 kila moja rais alipoulizwa majibu yake tunajua wote alivyojibu

Pili rais amesema hafukui makaburi mana yake kuhusu escrow, epa, lugumi, iptl,tangold, meremeta, richmound nakadhalika hatagusa. Sasa kuna jipya gani?

Kwa muhtasari huu magufuli amedanganya watanzania wakamwamini kumbe yeye hakuwa na nia ya dhati kushughulikia uozo huu mkubwa je nani anafungwa kama ufisadi wote huu hakamatwi mtu

Tuandike tumeumia wenye akili wataelewa maana ya maneno haya watanzania tusitegemee mapya kutoka ccm kwa kuwa ufisadi ni ccm na ccm ni ufisadi ni sawa na mtoto kumkana baba yake ni kitu haiwezekani
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?
 
ongea hoja iliyopo mezani wew unaona ni siwa wabunge kuhongwa ili mswada upite sio ukiacha cdm mana hao baada ya kujiridhisha kuwa lowasa hakuwa mwizi ila mwizi ni bosi wake ndo wakampokea
 
Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?

Sasa hivi wapinzani wanacheza ngoma ya utawala ulioko madarakani. Wnachezeshwa kisawasawa hadi bungeni ni kama wameziba midomo, mh!
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?

Tena cdm njaa yao ni mbaya.
Kwa sasa hakuna.atakayedhubutu kutamka neno ufisadi, bosi wao na.mfadhiri wao.atakata mrija
 
Nawahurumia sana wanaotegemea kuwa serikali yoyote ya ccm inaweza kuwa na nia ya dhati ya kupambana, kuwajibisha na kuadhibu wale wote walio/wanaohusika na ufisadi mkubwa unaoididimiza nchi yetu. Anayebisha aseme hapa kwa uwazi ccm na serikali zake wamefanya nini au wanasema nini kuhusu ESCROW, LUGUMI, IPTL, RICHMOND, EPA, HELA ZA BUNGE LA KATIBA, KIVUKO FEKI CHA DAR-BAGAMOYO, HAYA MABARABARA MABOVU WANAYOJENGA KILA MAHALI (anayebisha aende kwa mfano kipande cha Mwenge Tegeta, halafu atuambie kimejengwa lini) Nchi hii kuna kundi la waovu ambao nyakati za uchaguzi wanatumia hila na nguvu zote ili watu wao watangazwe washindi, kwa sababu wanajua kuwa watu wao wakichaguliwa hawatawagusa kuhusiana na maovu waliyolifanyia taifa hili! Hivi kwa taifa linalojitambua itawezekana watawala kushughulishwa zaidi kuhusu kuwalinda watangulizi wao badala ya kushughulika kukomesha kuadhibu wahusika wa uhuni kama wa IPTL, EPA, RICHMOND, ESCROW, LUGUMI na madudu yanayofanana na hayo??? Nchi hii ina mkosi....
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?
Kwakua chadema wapo na fisadi, basi ufisadi usiongelewe?
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?
Mkuu, anayetawala nchi hii ni ccm, tusizoee kuwa kila watawala wanapokosolewa tunakimbilia kujificha nyuma ya vyama ambavyo havijashika dola. Na ni vizuri tukumbuke kuwa mamilioni ya raia wa nchi hii si wanachama wa chama chochote cha siasa. Kwa hiyo kwa mfano nikihoji madudu ya watawala, usiniambie kuhusu NCCR, CHADEMA, CUF, ACT nk. Kwa sababu vyama hivyo havitawali nchi hii. Na pia mimi siyo mwanachama wa vyama hivyo.
 
Anasema hawezi kufukua makaburi kwa kuwa anajua hawezi kumshtaki Lowassa.
Atakuwa amemshtaki JK na serikali yake.
huo ndo ukweli na kama kuna watu wanaamini lowasa anashtakiwa hakuna kitu ksma hicho na 2020 ndani ya nyumba sijui watasema nini lumumba
 
Inasikitisha sana pale wanaposema ipo mahakama ya mafisadi...halikuwa watu hawapandishwi kortini
 
Ndugu wanajamvi habari ya mda huu?

Kwa masikitiko makubwa niseme kwa wazalendo wa nchi hii wanaopenda kuona nchi yetu inasonga mbele tuandike tumeumia kwa hakika. Nasema haya kwa hoja kuu mbili

Moja tuanzie bungeni wiki iliyopita wabunge wa ccm wamehongwa mil. 10 kila moja rais alipoulizwa majibu yake tunajua wote alivyojibu

Pili rais amesema hafukui makaburi mana yake kuhusu escrow, epa, lugumi, iptl,tangold, meremeta, richmound nakadhalika hatagusa. Sasa kuna jipya gani?

Kwa muhtasari huu magufuli amedanganya watanzania wakamwamini kumbe yeye hakuwa na nia ya dhati kushughulikia uozo huu mkubwa je nani anafungwa kama ufisadi wote huu hakamatwi mtu

Tuandike tumeumia wenye akili wataelewa maana ya maneno haya watanzania tusitegemee mapya kutoka ccm kwa kuwa ufisadi ni ccm na ccm ni ufisadi ni sawa na mtoto kumkana baba yake ni kitu haiwezekani
Lakini kama hafukui itakuwaje wakati kila kuchako kuna watu wanavuta hundreds of millions through iptl? Au ni kwa kuwa haimhusu mzee EL?
Namna hii tutafika kweli?
 
Hata CHADEMA na UKAWA yao ndo walewale tu.

Waliyemwita fisadi miaka nenda rudi leo hii ndo kiongozi wao [de facto].

Sasa hivi wapinzani wana mamlaka yepi ya kimaadili ya kuwasema CCM kuhusu ufisadi wao?
we mzee kichwa yako ina ubongo wa nguruwe! hivi uovu wa ccm unahalalishwa na uovu wa chadema???,

ccm ina wanachama mil. 5, chadema ina wanachama mil 3, watz tuko mil 50, tunaohoji ufisadi sio wanachama chadema wala wanachama wa ccm.

ni sisi wananchi wazalendo tusiokuwa na vyama takriban mil.42, kwa hiyo hoja zako ni ya kipuuzi
 
Mkuu, anayetawala nchi hii ni ccm, tusizoee kuwa kila watawala wanapokosolewa tunakimbilia kujificha nyuma ya vyama ambavyo havijashika dola. Na ni vizuri tukumbuke kuwa mamilioni ya raia wa nchi hii si wanachama wa chama chochote cha siasa. Kwa hiyo kwa mfano nikihoji madudu ya watawala, usiniambie kuhusu NCCR, CHADEMA, CUF, ACT nk. Kwa sababu vyama hivyo havitawali nchi hii. Na pia mimi siyo mwanachama wa vyama hivyo.
Tatizo watakuelewa hawa jamaa? Hakuna kitu kinachonikera kwa mtu kukosoa serikali yake kwa nia nzuri tu, halafu anaibuka kada fulani eti na CDM au CUF au NCCR ni hivyohivyo. Serikali ni yetu sote, hivyo kila mtu ana haki ya kupongeza au kukosoa inapobidi.
 
CCM inakera lakini hatuna alternative.
Kuliko nimpe kura Lowassa bora CCM itawale milele.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom