Hakuna jambo la kishamba na kiuoga linakera kama hii tabia kutekana watanzania Serikali iko wapi?

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,668
Ni mara chache huwa naandika kuhusu siasa na utawala hasa SERIKALI. Ila inapobidi huwa naandika tena bila uoga wala hofu kuhusu hao watekaji sijui wanatoka kijiji, nchi, au bara gani ni jambo la kishamba, kipuuzi na kijinga.

Nianze na lawama za moja kwa moja kwa serikali kuruhusu na kuvibariki vitendo hivi kuendelea kushika kasi na kushamiri huku wakiendelea kukaa kimya. Serikali na mh. Rais Magufuri huwezi kukwepa lawama maana ukiwa kiongozi wa nchi (Tanzania) na kiongozi wa serikali (amiri jeshi) mkuu unayo dhamana ya kulinda na kutea usala wa nchi na kila raia nchini hapa.

Vitendo vya kutekana vimeanzia Serikali ya awamu ya 4 ya mh. Jakaya Kikwete na kuvuka kuingia serikali ya awamu ya 5 ya mh. Rais Magufuri. Ipo orodha ndefu ya matukio ya watu kutekwa na kurudishwa wakiwa wamepigwa na kuumizwa na wengine kupotea mpaka sasa ila UKIMYA wa serikali ma hasa mh. Rais unashangaza sana.

ORODHA YA WALIOTEKWA NA KUVAMIWA, na wanao sadikika kuwa wasiojulikana, hawa ni wale ninao wajua binafsi.

ULIMBOKA, ROMA, KUBENEA na MWENZAKE, AZORI, DIWANI KIGOMA, KUBANDA, BENI SA8, MOHAMED DEWJI, MWANDISHI WA DW, MDUDE CHADEMA, MFUASI WA CHADEMA KINONDONI aliuawa kabisa, MH. TUNDU LISSU, kimsingi hali ya sintofahamu ni kubwa sana huku tuhuma na kunyosheana vidole na kulaumiana hasa serikali yenye dhamani ya kulinda usalama na uhai wa raia wake kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama km polisi.

Rai yangu, niungane na wanao wanyooshea kidole TAASISI nyeti za vyombo vya usalama nchini vikiwemo POLISI na TISS hii ni kufuatia majibu yasiyotoa majibu kwa matendo haya ya kidharimu na kishamba, kwa mujibu wa sheria za kuanzishwa kwa vyombo hivi vinawajibika kuwalinda raia na usalama wao sasa inapofikia hatua raia wanadhuriwa na hakuna majibu au ufumbuzi wa matukio kama haya tukiwahusisha na haya matukio kufuatia mtiririko nadhani tutakuwa sawa.

Nasema kwa dhati kabisa ba kukemea hii hali ya KUTEKANA ni jambo HASI kabisa na tabia ambayo inatakiwa kupingwa na kila raia mwema wa nchii bila kujali nani anavitekeleza iwe MAJAMBAZI, NCHI ZA JIRANI, MABEBERU au SERIKALI chini ya vyombo vyake vya ulinzi na usalama si SAWA na SI HAKI kutumia vitendo hivi vilivyo kinyume ya misingi ya UTU na HAKI ZA BINADAMU. Nachelea kusema kwa kurudia maneno ya mwl. Nyerere aliwahi kusema akikemea UBAGUZI kwa kuufananisha na DHAMBI ya KULA NYAMA YA MTU, sasa utekaji tunao uona dhidi ya raia ata kama wanaikosoa serikali au kutofautiana kiimani na kiitikadi ipo siku itawageukia WANASIASA na VIONGOZI WA SERIKALI ndiyo chanzo cha mitafaruku ya kisiasa.

Narudia tena kusema ni VITENDO VYA KISHAMBA na KIJINGA, nashauri serikali na watanzania kupambana na utaratibu/utamaduni huu wa KIPUUZI tutofautiane na kudhibitiana kwa MJIBU WA SHERIA NA KATIBA YA NCHI huu mtindo unatunza na kujenga visasi ndani ya mioyo ya watanzania vitakuja kulipwa huko mbeleni, mfano mdogo tu FIKIRIA WATOTO WA MH. TUNDU LISSU wakipata nafasi ya kulipa kisasi kwa aliyefanya kitendo cha kumshambulia baba yao nani atawakataza wamsikie..??

Yakimkini haya maneno yangu wenda yakawa makali masikioni mwa SERIKALI ba VYOMBO vya DOLA ila binafsi natambua ni bora "kuziba ufa kuliko kujenga ukuta" TUJISAHIHISHE AISEI..!

MH. RAIS UNAWEZA UNDA TUME AU KUTOA AMRI ufuatiliahi wa haya matendo ya kidharimu, kijinga na kipuuzi ata kama wanao yafanya wanaweza kuwa na lengo chanya ila nadhani si katika ENZI hizi za dunia inayodhidi kustaarabika kila kukicha kunaichafua Tanzania na serikali yako kwenye ramani ya dunia.
Kwa UNYONGE KABISA NAKIRI KUSIKITISHWA NA MATENDO HAYA MABAYA NA KISHAMBA.
 
Mimi katika sitaki kupepresa macho, SERIKALI inawajibu wa kuwalinda raia wake kwa gharama yeyote..! Nadhani tunahitaji kuhoji sana badala ya kuogopa kutekwa..
kweli kabisa mkuu wanalaumu kunyooshewa vidole lakn kwann hakuna jibu la nani hasa anahusika katika haya
 
Limbukeni mkuu ndio mastermind wa kuteka na kutekwa ,we angekuwa mwingine angemfuata amtafute mpaka mbinguni .
 
Ni mara chache huwa naandika kuhusu siasa na utawala hasa SERIKALI. Ila inapobidi huwa naandika tena bila uoga wala hofu kuhusu hao watekaji sijui wanatoka kijiji, nchi, au bara gani ni jambo la kishamba, kipuuzi na kijinga.

Nianze na lawama za moja kwa moja kwa serikali kuruhusu na kuvibariki vitendo hivi kuendelea kushika kasi na kushamiri huku wakiendelea kukaa kimya. Serikali na mh. Rais Magufuri huwezi kukwepa lawama maana ukiwa kiongozi wa nchi (Tanzania) na kiongozi wa serikali (amiri jeshi) mkuu unayo dhamana ya kulinda na kutea usala wa nchi na kila raia nchini hapa.

Vitendo vya kutekana vimeanzia Serikali ya awamu ya 4 ya mh. Jakaya Kikwete na kuvuka kuingia serikali ya awamu ya 5 ya mh. Rais Magufuri. Ipo orodha ndefu ya matukio ya watu kutekwa na kurudishwa wakiwa wamepigwa na kuumizwa na wengine kupotea mpaka sasa ila UKIMYA wa serikali ma hasa mh. Rais unashangaza sana.

ORODHA YA WALIOTEKWA NA KUVAMIWA, na wanao sadikika kuwa wasiojulikana, hawa ni wale ninao wajua binafsi.

ULIMBOKA, ROMA, KUBENEA na MWENZAKE, AZORI, DIWANI KIGOMA, KUBANDA, BENI SA8, MOHAMED DEWJI, MWANDISHI WA DW, MDUDE CHADEMA, MFUASI WA CHADEMA KINONDONI aliuawa kabisa, MH. TUNDU LISSU, kimsingi hali ya sintofahamu ni kubwa sana huku tuhuma na kunyosheana vidole na kulaumiana hasa serikali yenye dhamani ya kulinda usalama na uhai wa raia wake kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama km polisi.

Rai yangu, niungane na wanao wanyooshea kidole TAASISI nyeti za vyombo vya usalama nchini vikiwemo POLISI na TISS hii ni kufuatia majibu yasiyotoa majibu kwa matendo haya ya kidharimu na kishamba, kwa mujibu wa sheria za kuanzishwa kwa vyombo hivi vinawajibika kuwalinda raia na usalama wao sasa inapofikia hatua raia wanadhuriwa na hakuna majibu au ufumbuzi wa matukio kama haya tukiwahusisha na haya matukio kufuatia mtiririko nadhani tutakuwa sawa.

Nasema kwa dhati kabisa ba kukemea hii hali ya KUTEKANA ni jambo HASI kabisa na tabia ambayo inatakiwa kupingwa na kila raia mwema wa nchii bila kujali nani anavitekeleza iwe MAJAMBAZI, NCHI ZA JIRANI, MABEBERU au SERIKALI chini ya vyombo vyake vya ulinzi na usalama si SAWA na SI HAKI kutumia vitendo hivi vilivyo kinyume ya misingi ya UTU na HAKI ZA BINADAMU. Nachelea kusema kwa kurudia maneno ya mwl. Nyerere aliwahi kusema akikemea UBAGUZI kwa kuufananisha na DHAMBI ya KULA NYAMA YA MTU, sasa utekaji tunao uona dhidi ya raia ata kama wanaikosoa serikali au kutofautiana kiimani na kiitikadi ipo siku itawageukia WANASIASA na VIONGOZI WA SERIKALI ndiyo chanzo cha mitafaruku ya kisiasa.

Narudia tena kusema ni VITENDO VYA KISHAMBA na KIJINGA, nashauri serikali na watanzania kupambana na utaratibu/utamaduni huu wa KIPUUZI tutofautiane na kudhibitiana kwa MJIBU WA SHERIA NA KATIBA YA NCHI huu mtindo unatunza na kujenga visasi ndani ya mioyo ya watanzania vitakuja kulipwa huko mbeleni, mfano mdogo tu FIKIRIA WATOTO WA MH. TUNDU LISSU wakipata nafasi ya kulipa kisasi kwa aliyefanya kitendo cha kumshambulia baba yao nani atawakataza wamsikie..??

Yakimkini haya maneno yangu wenda yakawa makali masikioni mwa SERIKALI ba VYOMBO vya DOLA ila binafsi natambua ni bora "kuziba ufa kuliko kujenga ukuta" TUJISAHIHISHE AISEI..!

MH. RAIS UNAWEZA UNDA TUME AU KUTOA AMRI ufuatiliahi wa haya matendo ya kidharimu, kijinga na kipuuzi ata kama wanao yafanya wanaweza kuwa na lengo chanya ila nadhani si katika ENZI hizi za dunia inayodhidi kustaarabika kila kukicha kunaichafua Tanzania na serikali yako kwenye ramani ya dunia.
Kwa UNYONGE KABISA NAKIRI KUSIKITISHWA NA MATENDO HAYA MABAYA NA KISHAMBA.
Kidnapping or Terrorism USA should check this..
 
Back
Top Bottom