AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 222
- 695
HAKUNA HARUSI INAYOKOSA WASINDIKIZAJI NA WATANI
Ni kawaida Harusi yoyote inapofungwa lazima kuwe na wasindikizaji na watani wanaohanikiza na kuchangamsha sherehe nzima.
Hii ndio ni desturi nzuri ya Watanzania. Bwana Harusi aoae ni mmoja tu nae anajlikana, hawa wengine ni wasindikizaji na watani ambao wanacheza, kufika, kuimba na kuongea kila aina ya maneno ili kuchangamsha genge.
Wasindikizaji wengine mahiri kweli kweli na wana upendo wa dhati kwa Bwana Harusi kwa maana wameamua kutoka hata nga'mbo ya nchi kuja kumsindikiza kaka yao anayeoa siku ya Jumatano Oktoba 28.
Kinachofurahisha zaidi kwa wasindikizaji hawa ni rangi za sare ya mavazi zao, wengine wameshona sare za rangi nyekundu, huku zikiwa na fito za buluu na nyeusi kwa mbalii hana na hawa wengine wameshona sare za rangi ya zambarau, hakika wamependeza sana.
Chereko chereko asie na mwana aeleke jiwe.