Dindai Ndesi
Member
- Dec 5, 2010
- 16
- 0
Gavana wa Banki Kuu alipokuwa anatangaza kuanza kwa matumizi ya Noti mpya hapo January Mwakani 2011, alisisitiza hakuna mda maalumu wa mwisho kubadilisha matumizi ya hizi Noti zinazotumika sasa, hivyo watu wasikimbilie kwenda kuzibadilisha. Zitabaki ni fedha halali mpaka hapo zitakapo potea katika mzunguko.
Hapa Nyumbani, hasa sehemu za Mijini watu hukimbilia mwanzoni kutaka kuwa na toleo la Noti mpya mapema. Mdani ya Miezi miwili ni dhahiri Noti mpya zitakuwa zimetapakaa sehemu mwingi.
Tatizo (usumbufu), kwa wale wenzangu na Mimi ambao tutakuwa hatujabadilisha Noti zetu, upo uwezekano mkukwa wa kukosa huduma pindi unapotaka kutumia Noti ya zamani. Wengi wa wafanyabiashara wadogo Mitaani ,( e.g chips, Pub, Magenge nk. ) hawatapokea Noti za zamani.
Hapa Sheria Inasemaje?, Mtu ( Mfanyabiashara ) anapokataa kupokea fedha halali kwa mujibu wa tangazo la Gavana wa Bank Kuu. Pia ukiwa mmoja wao wa watu waliokosa huduma kwa kuwa na Noti ya zamani , utatakiwa kufanya nini?