Hakuna furaha ya Kweli katika mapenzi

Hakuna furaha ya Kweli katika mapenzi

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
::
Binadamu tumeumbiwa kutafuta furaha katika maisha.
Tutajaribu hili na lile ilimradi tu tupate furaha.Je ni rahisi furaha kuipata?
::
Washairi huitukuza,Waandishi huielezea,Wanafalsafa hujenga hoja tu lakini wote hao na sisi huishia kujifariji tu maana baada ya muda tunajua hatuna furaha.
::
Wapo waliodhani utawala utawapa furaha lakini wapi,,matajiri wamejaribu kununua furaha lakini furaha haiuzwi,wasomi wamejitahidi kuielewa lakini wameambulia kuchanganyikiwa tu,umaarufu pia hauna furaha ya kweli.
::
Msomi wa kale Sigmund Freud nae alidhani kama wengi wanavyodhani kuwa Furaha ipo katika mapenzi.
Kwamba kule kubadilisha hisia,joto,mahaba,maneno matamu,ujuzi wa mitindo mingi ya mapenzi huleta furaha LAKINI baada ya tendo hilo kuisha tunajua kuwa ilikuwa msisimko tu wa mwili na si furaha.
::
JE FURAHA IKO WAPI?
Furaha ya kweli ni jinsi "tunavyowaza"
Ni mawazo ya aina gani tumeweka akilini,,tumeumbwa kufikiri,,tunafikiri kila siku,tunafikiri juu ya jana,leo,kesho, juu ya mke,mtoto,mume n.k
Tunapaswa kuyaongoza mawazo yetu Kamwe kukimbilia ngono toka mwili huu kwenda huu hautufanyi kupata furaha.Ni kujiletea majuto baadae.
FURAHA YA KWELI HAIPO KATIKA MAPENZI bali katika namna tunavyowaza.
=
 
Back
Top Bottom