Hakuna experience ya huzuni kuu kama ya kufiwa na mke/life partner

Wakati mwingine mtu ni mbaya ukiwa naye; siku akiondoka ndo utayaona mazuri yake ambayo hukuwahi kuyaona kabla. Huyo mke mbaya kwako; ndo mama mwema na mzuri kwa watoto wake (wenu). Itakuuma kuona watoto wako wamemkosa mama kwenye malezi, kwenye hatua zao za kimaisha etc. Watakapolia utaumia tu na kulia nao. Wewe na wema wako wote, huwezi kuwa mama kwa watoto wako regardless utajitahidi vipi kuziba hilo pengo; kuna kitu tu kitamiss. Wakati mwingine kwenye maisha hauhitaji mtu wa kukufanyia makubwaa: but mtu tu wa kumuita "baba au mama au dada au kaka, mke, mume n.k; ........wa kumuita tu

Kuna hii familia; baba alikuwa anarudi usiku amelewa, anakimbiza nyumba nzima na panga;yaani ilikuwa tafrani. Ikatokea yule baba akafa; yule mama analia hadi leo anasema bora hata mumewe angekuwepo tu pamoja na tabu zote alizokuwa anawapa. Alikuwa na matatizo yake; but angalau familia ilikuwa na uhakika wa kula; watoto kwenda shule, mahali pa kulala, kutibiwa etc. Pumzi ni kitu cha thamani sana
We jidanganye tu hadi ushushiwe gunia la mkaa ndio utajua
 
Siku utakayoacha kulia na kumwacha Apumzike na kukubali hayupo na kujitenga naye kiroho Mambo yatakunyookea au uendelee kulia roho la mauti likuvae uache watoto yatima. Kwenye maisha haya Kuna shida na dhiki nyingi lakini Yesu mwenyewe anasema jipeni moyo nimeushinda ulimwengu, na dunia hii amani ya Kristo yatosha kabisa na kwa mkristo uhai na kuishi kwake ni Kristo na kufa ni faida.
Mtoe moyoni kubali hayupo siku uki relax Mambo yatanyooka uchungu ulio nao moyoni ndo umefunga mengi activate furaha moyoni shukuru Mungu kwa kila jambo, na atakusaidia
Asante nimekuelewa nitakuja pm
 
Wanawake huwa wanapata/wanahamishia nguvu kwa watoto wao. Huyo mjane anayenawiri; subiri afiwe na mtoto wake ndo utaelewa.

Btw nimekaa na wajane wawili watatu; ni kweli wananawiri as maisha lazima yaendelee; lakini deep down kuna uchungu ambao si rahisi mtu wa nje akauona. Mkiwa nyumbani, kuwakuta wamejikunyata wanalia ni kawaida sana tu; ila mgeni akifika anavaa tu tabasamu anatoka. Sio rahisi kwao kama inavyoonekana kwa nje.

Mwanaume umuache tu peke yake na watoto ni shughuli; ndo mke afe kabisa weeeh. Huwa wanachanganyikiwa sana coz most of times mama ndiye analea zaidi watoto nyumbani; as you know kulea si utani.
Ok dear, umenifungua kiupana zaidi
 
Mzazi na Mke au mume Kuna utofauti..mke unashare naye mengi..mke ni zaidi ya rafiki...unashare naye kitanda ...mhh anauma bwana
Inategemea lakin na malez..huwez fananisha jins mim nilivyolelewa na waza wangu na wew.huendaa kuna utofaut mkubwa..inshort mim ni mamaz boy so simwelew mtoa mada hata chembe
 
Kuna watu wanaomba wake zao au waume zao wafe hata leo.

Inategemea na aina ya ndoa uliyonayo. Ndoa nyingine ni JEHANAMU. Umeingia ila kutoka huwezi.
 
Oooh
Mmenifanya nishindwe kulala kabisa mpka natamni hata kuupload picha ya marehemu kipenzi changu. Maisha haya changamoto alizoniachia hua siwezi kuzitatua na nimefeli daima. Hua natamani ata anitokee dakika walau moja tu nimuulize mambo fulani ya msingi but too late
 
Pole Sana ndugu kwa huo mtihani mzito. Ni kweli ni maumivu yasiyoelezeka ila at the end of the day life must go on! Unahitaji upate maombi maalumu yakukutenga na majonzi, vilio, msiba na maombolezo ili uweze kupokea changamko la moyo na MUNGU afanye jambo jipya. Vinginevyo unaweza kupata depression mbaya ukajikuta unastopisha maisha. MUNGU BABA akuvue hilo vazi la maombolezo, huzuni na kuugua!
 
Msiba wa mke/mume au mzazi unauma sana lakini tunakosea tunapo fananisha uchungu wa kufiwa na watu wawili tofauti ambao ni wa muhimu sana maishani. Poleni wote ambao mmefiwa na wapendwa wenu.
 
Asante nimepitia yote kama ulivyo sema now naugumia maradhi tu na nimeanza kurecover
Pole. Hayo maradhi tafuta spiritual healing ukae sawa. Nitext ukihitaji mtumishi wakuongea naye hata kwa simu akushauri na maombi. Nicholas bure hakuna malipo.
 
Jaman mimi machungu ninayapitia mpaka leo nalia
Nilikua na mpenzi tulipendana sana mimi nilipata kazi mkoa tofauti na wake nikafanya kazi kama mwaka mmoja baadae akanitafutia kazi mkoa alipokua anaishi ili tuwe pamoja nikafanya kazi kama mwaka mmoja na nusu baadae nilipata changamoto ya kifamilia iliyohitaji muda wangu sana nikaacha ile kazi na ndo mapenz yakaishia hapo akasema simuheshimu wala kumsikiliza nilijitajid kumuomba msamaha lakin wapi
Jamn kila siku nalia mbya zaid alinitamkia kua alizaa na mtu mwingine tukiwa kwenye mahusiano Kwa hiyo aumii saana kuniacha jamn bora ningefiwa
 
My dear kuachwa kunauma sanaaa; lakini kufiwa ni habari nyingine kabisaaaa. Time heals; kesho na kesho kutwa Mungu atakupa wa kwako ambaye atakufuta machozi. Huyo wa kukwambia haumii kukuacha + kuzaa akiwa kwenye mahusiano na wewe: girl pleaseeeee

Jaman mimi machungu ninayapitia mpaka leo nalia
Nilikua na mpenzi tulipendana sana mimi nilipata kazi mkoa tofauti na wake nikafanya kazi kama mwaka mmoja baadae akanitafutia kazi mkoa alipokua anaishi ili tuwe pamoja nikafanya kazi kama mwaka mmoja na nusu baadae nilipata changamoto ya kifamilia iliyohitaji muda wangu sana nikaacha ile kazi na ndo mapenz yakaishia hapo akasema simuheshimu wala kumsikiliza nilijitajid kumuomba msamaha lakin wapi
Jamn kila siku nalia mbya zaid alinitamkia kua alizaa na mtu mwingine tukiwa kwenye mahusiano Kwa hiyo aumii saana kuniacha jamn bora ningefiwa
 
Mtu yeyote ambae alikuwa anaonyesha upendo wake kwako na anakujali, siku akifa lazima utaumia.
Iwe ni dada au kaka
Shangazi au mjomba

Ilaa, nasema ilaa, hata kama ni mkeo, lakini matendo yake yalikuwa huyaelewi, alishaacha kukuheshimu, tunda akikupa kama kalazimishwa, majibu ya mkato ndio salamu yake, ulikuwa nae kwasababu mmezaa na mmejenga wote, bwana hata akitangulia, mume msibani ndio kwanza anabeti mechi ya usiku, na mkeka unatiki.

Hata kwa mwanamke my dear ni hivyo hivyo tu. Kwamba mume jina. .mume bachelor mume mwanachuo siku ya siku Israel akiamua kufanya yake hata kma Kuna kikoba mke unahudhuria Safi kbs!
 
Jaman mimi machungu ninayapitia mpaka leo nalia
Nilikua na mpenzi tulipendana sana mimi nilipata kazi mkoa tofauti na wake nikafanya kazi kama mwaka mmoja baadae akanitafutia kazi mkoa alipokua anaishi ili tuwe pamoja nikafanya kazi kama mwaka mmoja na nusu baadae nilipata changamoto ya kifamilia iliyohitaji muda wangu sana nikaacha ile kazi na ndo mapenz yakaishia hapo akasema simuheshimu wala kumsikiliza nilijitajid kumuomba msamaha lakin wapi
Jamn kila siku nalia mbya zaid alinitamkia kua alizaa na mtu mwingine tukiwa kwenye mahusiano Kwa hiyo aumii saana kuniacha jamn bora ningefiwa
Hapo tu hujaolewa umeanza kuoneshwa rangi rangi ..! Kuna watu mnavipaji vya kupenda aise
 
Back
Top Bottom