Hakuna encryption kwenye Website ya PROIN

Indume Yene

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
2,968
Reaction score
728

Ndugu zangu watanzania,

Leo nimejaribu kwenda kwenye Website ya PROIN nikiwa na dhamira ya kununua one movie ili ku-support watanzania wenzetu walioko kwenye hiyo tasnia. Website inadai kuwa transaction inayofanyika kwenye hiyo site iko salama (salama). Mimi as mtalaamu wa Information Security nilikuwa curious kujua kama kweli hiyo Website inaruhusu encrypted transaction nikimaanisha kuwa unapokuwa unaweka information za siri kama password au kadi ya benki na aina yoyote ya information ambayo ni siri kwa mtumiaji wa Website.

Hivyo basi nilianza kuweka movie moja kwenye basket na nikawa nataka ku-check out. Ikanipeleka kwenye page ya ku-login ambapo hapa Website inatakiwa kutumia encryption kuhakikasha hakuna mtu anaweza kunasa information zangu kama vile username and password. Cha ajabu ni kuwa hii Website haikuwa na encryption yoyote kama wanavyodai. Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa ikiwa uta-login in au kununua movie kwenye Website hii, kuna uwezekano mkubwa information za mteja zikanaswa na hackers au sniffers, na wakatumia information zako kufanya unauthorized transactions. Ili kujua Website iko secure, kuna vitu viwili unaweza kutumia ku-make judgement. Cha kwanza ni utumiaji wa
https(Hypertext Transfer Protocol Secure) mwanzoni mwa website address badala ya http ambayo haiko safe (haina S mwishoni). Cha pili ni kuona alama ya kufuli mwanzoni mwa Website address kama ambavyo utaona hapo chini.

Hapa chini nawawekea Website mbili, ya PROIN ambao wana-claim Website yako iko salama (Encrypted) na nyingine ya Ebay ambayo iko encrypted. Communication kwenye PROIN IS NOT SAFE (UNSECURE). Angalia hapo nilipo-highlight.





 

Attachments

  • PROIN.JPG
    47.2 KB · Views: 352
  • Ebay.JPG
    31.9 KB · Views: 332
Proin inamilikiwa na wazee wa EPA kuwa makini nao hao wasije wakapukutisha masimbi yako yote kwenye accounts.
 
Proin inamilikiwa na wazee wa EPA kuwa makini nao hao wasije wakapukutisha masimbi yako yote kwenye accounts.

Sina hakika kama hayo ndiyo malengo yao BUT you never know maana mwanadamu huwa hatosheki. Thanx for crew.
 
Safi umetumia weredi wako vizuri.
Sasa kaka kwann usitumie nafasi hio kupropose uwatengenezeaa encrypted website.???

Ukizingatia tz kuna wataalamu wachache wa weredi kama wako.
 
Safi umetumia weredi wako vizuri.
Sasa kaka kwann usitumie nafasi hio kupropose uwatengenezeaa encrypted website.???

Ukizingatia tz kuna wataalamu wachache wa weredi kama wako.

Kuna kitu kinaitwa Secure Sockets Layer (SSL) ambayo hii inaweka usalama (secure connection) katika mawasiliano kati ya internet browsers pamoja na Websites. Mhusika au mwenye Website anatakiwa kununua SSL certificate kutoka kwa Certificate Authority (CA).

Baada ya hapo CA watatoa instructions jinsi ya ku-install SSL kwenye Website ya mhusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…