Hakuna binadamu ambaye hajawahi kukutana na hiki kitu

Hakuna binadamu ambaye hajawahi kukutana na hiki kitu

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,265
Kuna wakati unatamani kila text inayoingia kwenye simu yako itoke kwake, bahati mbaya inaingia text na unairukia simu kutaka kuisoma, unakuta ni text
ya yule usiye na feelings naye akikwambia " I love you", unatamani kubamiza simu chini kwa hasira.

Aliyesema mapenzi upofu hakukosea, unayempenda anampenda mtu mwingine na yule usiyempenda anakupenda mpaka unajisikia vibaya, unatamani mapenzi aliyonayo huyu kwako angekuwa nayo yule mwingine, unatamani abadilike na kuona unavyohangaika juu yake.

Kuna wakati unaona kabisa kule alipo naye hastahili, yule aliyenaye anamtumia tu lakini huwezi kumwambia, ataona una wivu naye, ataona kama ni mbinu zako za kutaka kuharibu ili aje kwako, hataweza kukusikiliza kwa kuwa amezama kule na hasikii lolote.

Ngoja niendelee kumwacha kule alipo, labda ipo siku atagundua na kubadili njia, labda ipo siku atageuka na kuniangalia na labda ipo siku ataenda
moja kwa moja pia, naendelea kusali na kujipa tumaini labda pia ipo siku nitamsahau na kusonga mbele.
 
1469133076195.jpg
 
Hakuna text nazozipenda Kama za Tigo pesa na M-PESA, huwa natamani kila dakika zinaingia tu.
Hahaaa jaman really text za imethibtshwa umepokea......huwa hata Mimi nazipenda sana...hizo nyingine chenga tuuuuuu
 
Nitakukumbuka Daima Zawadi wangu, nilikupenda sana saana na najua ulinipenda pia ila yule jamaa ndio alikuharibu. Alikutia mimba na akakuacha na mapacha wawili, hakika ujana ni maji ya moto.
 
Back
Top Bottom