Hakuna atakayefanikiwa kuihujumu Tanzania

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi teule na nchi yenye kuonesha njia kwa Africa na Dunia katika nyanja zote.

Wapo maadui wengi dhidi yetu wenye mbinu mbalimbali lakini Tanzania ni babalao.

Haijawahi kushindwa na kamwe haitashindwa.

Tanzania imeshasimama. Tanzania ni wabishi, wababe na wapambanaji.

Tupo hivyo na tutaendelea kuwa hivyo.

Let us watch the big show!

If you plan an attack against Tanzania remember we had a counter attack way back in 59 years ago!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Hizo Propaganda hazisaidii katikati ya matatizo na maumivu ya watu

Chuki inayoonekana machoni mwa watu ni dhahiri tupo eneo baya na la hovyo sana

Sijawahi ona watu wamegawanyika namna hii, Huku kundi kubwa likisubiri kufanya sherehe katikati ya matatizo

Propaganda za kipumbavu kama hizi toka kwa mtu mzima ni aibu Kwa Taifa

Watu wanafanya utafiti wa Astrazeneca, Bion Tech _Pfizer, Johnson and Johnson wewe unaongelea mambo ya hadithi za Abunuasi

Ni kama watu wanasubiri maovu na mabaya kujenga Furaha zao.Jirani zetu sasa wamegeuka watangazaji mambo yetu

Kama sio uzalendo wa watanzania na upendo wa muda mrefu uliojengwa na Mababu zetu, Leo watu wangeongea mengine, Ingawa Wengine wanatumia lakini bado tunapendana mitaani bila kuangalia chama au Dini

Hakika watanzania wazee wetu wamejitahidi sana

Demokrasia yetu imetikiswa, Upendo wetu umetikiswa lakini tupo pamoja

Haya yanayotokea kuombeana mabaya na Propaganda za mleta uzi ni matokeo ya kuvuna tunachopanda

Tuache Propaganda, Tuhubiri Amani na upendo wa kweli, Tumezaliwa Tanzania na hata wengi tutasafirishwa na kuzikwa Tanzania

Hii ni nchi ya Mababu zetu, Baya au zuri yote ni yetu
 
Pumbavu Lao. Kuna majina huwa hayatokei bahati mbaya mtu kujiita au kuitwa. Yanasadifu uhalisia jinsi mtu alivyo. Sawa na mtu kumwita mtoto matatizo, shida . Utashangaa atauvaa uhalisia na uhusika wa hayo majina.

Jingalao na anaandika ujinga hasa.
Jikite kwenye mada, huwa sipost kwa bahati mbaya.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Soko kubwa la mahindi pale Manzese wiki ilyopita mkulima/mfanyabiashara anapata tshs 500 kg leo malori yamejazana bei ni tshs 200
Yawezekana maccm hamjawahi kushindwa lakini mkulima wa Katavi anasjilizia maumivu ya kushindwa baada ya kazi ngumu ya miezi kadhaa.
 
Tatizo leo tunaishia kujidanganya tu. Hatuna cha ajabu hapo Tanzania tofauti na nchi nyingine. Na hao wanaofikiri rasilimali Gas mbona Msumbiji wana Gas zaidi ya mara kumi yetu?

Mbona Uganda wana mafuta? Tumewazidi Congo kwa rasilimali? sasa cha ajabu ni kipi. Tuache ushamba wa kutafuta wachawi tatizo letu ni sisi wenyewe na wala sio wengine. Maneno mengi kumbe watu wanatibiwa Nairobi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom