Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina maadui wengi miongoni mwa Wananchi wake

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,032
3,478
Jukwaa la msuguano wa akili na mawazo mbadala kwa kutoa sulushi kwa faida ya wote;

Kwa sasa Tanzania ina maadui wengi sana kutoka miongoni mwa Wananchi wake na viongozi wa kisiasa.

Maadui wa kimkakati ni watatu kama wanarivyorithishwa kila awamu ya uongozi ni Ujinga, Maradhi na Umaskini.

Wanaojitokeza kila baada ya awamu ya uongozi wanatofautiana kwa kulingana na changamoto zinazojitokeza kukabiliana na mahitaji ya kazi, mazingira rafiki ya biashara, ufisadi na rushwa, ukosefu wa haki, uzembe kazini, uzalishaji hafifu, uhujumu uchumi kwa kuficha bidhaa zinazohitajika na washika dau, upendeleo, ubaguzi, dharau za baadhi ya viongozi dhidi ya watu wa chini kwa mambo ya msingi wanayodai kutotendewa ipasavyo hatimaye maadui wafuatao hutokea ili kukuza tatizo ili adui wa nje apate mwaya kupenya ndani kwa sura ya kusaidia kuondoa tatizo huku wakijilipa isivyo halali kwa msaada wa kibinadamu:

1. Watanzania waliotoka vijijini kabisa ama wakiwa wamepata elimu ya kutosha ama hapana lakini ndio wanaotoa taarifa za siri kwa watu wa nje ya nchi ambao walikuwa na maslahi ya sio na vikwazo

2. Baadhi ya wasomi ndio wanaotumika kuvujisha mipango na mikakati ya kitaifa kuhusu uchimi kwa lengo la kuhujumu juhudi hizo kwa kisingizio cha ukiukwaji wa haki za binadamu

3. Baadhi ya wanasiasa wenye mawazo mbadala wanapokwama kutimiza malengo yao wanaamua kushirikiana na watu wa nje wenye malengo ya kuanzisha mgogoro na serikali kutokana na kukwama shughuli zao za uzalishaji

4. Utandawazi lengo lake ni kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi, lakini wasomi wenye malengo rahisi kwa kutumia njia za mkato kufanikisha uongozi wa kisiasa wanaona wanacheleweshwa hivyo huamua kuuza taarifa na nyaraka maalumu za siri kwa maadui wa nchi ndio maana mnasikia kila leo kesi zinafunguliwa kwa madai ya kusababishiwa hasara kwa kukatishiwa mikataba au kurejelewa mazungumzo kwa maslahi ya nchi;

5. Baadhi ya michango ya mawazo kwa watumiaji wa mitandao sio ya kujenga ila ni kubomoa kwa nia ya kumkomoa mtu wanayedhani ndio kikwazo kwao kufikia malengo ya kupata uongozi wa kisiasa katika nchi

6. Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wamezoea kujipatia faida kubwa isiyoathiri gharama za matumizi ya kiutawala na uendeshaji hawalipi kodistahiki kwa mfumo wa elektroniki ipasavyo (thamani halisi kwa kulingana na mteja alivyolipa haiingizwi kwenye risiti ya malipo, kufich bidhaa kwa nia ya kupandisha bei, kuuza bidha bila utaratibu halali kwa kuwapa machinga wenye kitambulisho kilicholipiwa gharama za utengenezaji kisha baada ya mauzo machinga analipwa kamisheni kidogo kwa kufanikisha uuzaji huo usio halali, kuwa na migomo baridi ujengaji na ufufuaji wa viwanda vilivyobinafisishwa kwao miaka kadhaa iliyopita;

7. Baadhi ya wasafirishaji

8. Baadhi ya watumishi wa umma na serikali

Kama Matanzania anajiunga na adui kumkwamisha Mtanzania asifanikiwe kwa wivu, chuki na inda kwamba kkwa kuwa wao sio viongozi wa kufanikisha lengo hilo wanaona ni bora kumkomoa kiongozi huyo bila kufikiri anayekwamishwa ni mwananchi wa kawaida kumudu maisha yake kwa gharama nafuu ili kuonesha nguvu zao za ushawishi za kukubalika katika jamii

Nini kifanyike?

Kuna mahitaji kadhaa yanatakiwa yawepo ili mtu, kikundi au nchi ishinde vita inapasaswa angalau yafuatayo yaambatane na mpango huo
1. Uongozi bora, imara na usio yumbayumba kwa maslahi ya nchi
2. Nguvu elndelevu za kiuchumi kufanikisha ghrama za uendeshaji wa vita (rasirilimali watu na vifaa)
3. Nia, hamasa, sababu, uwezo na utashi wa wananchi kuunga mkono vita hiyo kwa gharama za nguvu zao na rasirimali za nchi
4. Eneo la kijiografia la nchi husika
5. Uungwaji mkono na marafiki wa nje ya nchi kiuchumi, kijamii, kwa taarifa za ulinzi na usalama
6. Uwezo na teknolojia ya vifaa na rasirimali watu ya jeshi kukabiliana na maadui kwenye medani za kivita, kidiplomasia na kiusalama
7. Kudhibiti mamluki na wasaliti miongoni mwa jamii na watumishi
8. Kufanya kazi kwa bidii kwa uzalishaji wa bidhaa, huduma na maarifa ili kujitegemea katika nyanja zote za kiuchumi, usalama, jamii nk

NB: Tanzania kwa sasa imo vitani dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nasaba ya Wananchi

i) Adui wa ndani-asiyependa kitu kizuri chenye maendeleo ya jumla na binafsi kifanyike chini ya kiongozi asiyempenda au kuwa na itikadi ya pamoja naye

ii) Adui wa nje-washirika waasi kwenye shighuli za pamoja za kiuchumi baada ya kutofautiana maslahi ambapo upande mmoja unatuhumu kuhujumiwa na mwingine ukidai kunyang'nywa shughuli au huduma yenye maslahi binafsi ndipo mgogoro unapozuka huku kila upande ukidai haki zaidi ya mtindo wa win-lose badala ya win-win situation

KARIBUNI kwa mawazo mchanyato na yenye ujenzi
 
Wanashindana lakini hawatashinda kama yalivyo matokeo ya Uchaguzi Mkuu.

Kuadhibiwa kwao kwenye sanduku la kura kunatoa nafasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, 2020 ya Chama Tawala.

Viongozi wa Serikali kuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa sasa wanawajibika kutekeleza ahadi zao bila viongozi wa kupingapinga.

Waliokatiliwa kwenye sanduku la kura watumie Uhuru na Haki yao kuondoka nchini, kufungua mashtaka au kukaa kimya. Kelele za mitandaoni zitabaki huko huko kwa jinsi ileile ya "debe tupu" au "kelele za chura".
 
Wizi wa Kula na uchaguzi uliovurugwa matokeo yake ndio hayo. Umeandika Fyongo Njingi lakini Unashindwa kutambua ya Kwamba Uchaguzi haukufanyika na Kwamba wazungu waliiona ile dhuluma na wameamua kutusaidia sisis wanyonge. Wazungu wanatoa msaada na Mikopo kwa nchi inayojali utu.. Hii inchi imekuwa kama shurubu za kambale Kuumiza Dagaa...
 
Adui mkubwa wa Taifa letu kwa sasa ni CCM, Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Hawa wamemeng'enyua mpaka mizizi ya Taifa letu. Baadhi ya mambo makubwa maovu waliyoyafanya mpaka sasa:

1) Uongozi wa kibaguzi. CCM, Serikali yake na Rais/Mwenyekiti wake kutamka wazi kuwa maendeleo yatapelekwa mahali kwa kuangalia itikadi ya wananchi

2) Utekaji, uuaji na upotezaji wa raia au wanaohoji au kumkosoa Rais

3) Ubambikaji wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha wanaoikosoa serikali

4) Ukanyagaji wa uhuru wa watu, haki zao na ukiukaji wa misingi ya demokrasia unaofanywa na CCM, Rais, Tume ya Uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama

5) Ukiukaji wa wazi wa katiba na sheria unaofanywa na Rais, CCM, serikali na vyombo vya ulinzi na usalama

6) Serikali badala ya kulinda raia, kujigeuza na kuwa genge la maharamia dhidi ya wanaopinga uonevu, mfano mauaji ya wananchi waliokuwa wanataka kuandamana kule Zanzibar

Kwa sasa tunashuhudia taasisi zilizostahili kulinda haki, uhuru na demokrasia, zikigeuzwa kuwa magenge dhidi ya haki za wananchi wanaotaka misingi ya utawala bora, demokrasia, uhuru na haki, ilindwe/kuheshimiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanashindana lakini hawatashinda kama yalivyo matokeo ya Uchaguzi Mkuu.

Kuadhibiwa kwao kwenye sanduku la kura kunatoa nafasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, 2020 ya Chama Tawala.

Viongozi wa Serikali kuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa sasa wanawajibika kutekeleza ahadi zao bila viongozi wa kupingapinga.

Waliokatiliwa kwenye sanduku la kura watumie Uhuru na Haki yao kuondoka nchini, kufungua mashtaka au kukaa kimya. Kelele za mitandaoni zitabaki huko huko kwa jinsi ileile ya "debe tupu" au "kelele za chura".
CCM ipo madarakani toka 1960 unavyoongea kama vile nchi imepata uhuru 2019
 
Umeandika upumbavu wa kiwango cha juu mno!
Unayashutumu matunda ilihali ukiumwagilia mtini maji.
Alafu eti huoni hata aibu kujiita intelligence 😏
 
Mlitoa orodha ndefu ya makundi ambayo yangeinyima kura ccm mkashindwa vibaya sasa mnakuja na orodha nyingine.Ama kweli bongolala
 
Pasi na haki hakuna mshikamano.
Mkuu,

HAKI haipatikani kwenye siasa ni mpaka patokee mgogoro ndipo utoaji wa haki unatafutwa kutoka kwa chombo ambacho sio sehemu ya mgogoro husika. Kuimba haki kwenye jukwaa la kisiasa ni kujidanya tu. Ili madai ya haki yatolwe ni sharti pawepo mgogoro, mwathirika wa mgogoro na msababishaji wa mgogoro kisha chombo kisicho sehemu ya mgogoro kinapewa kazi

i) Haki kwa tafsiri ya kamusi ya Kiswahili ni 'jambo ambalo mtu anastahiki au kitu anachostahili kuwa nacho.'
ii) Haki kwa tafsiri ya kisheria ni 'kile mtu anachostahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mujibu wa sheria’'
iii) Sheria ndio inatoa haki au kutambua haki za watu. Hivyo ili ujue haki yako ni ipi lazima uijue sheria inayotoa haki hiyo kisha unachukua hatua ya kulalamika kwenye chombo kinachokubalika kisheria ili tatizo litatuliwe na wewe kupata kile ambacho unastahili kupata;
iv) Ili uthibitishe uhalali wa haki yako unapaswa pia kwa pamoja kuthibitisha utekelezaji wa wajibu wako kuhakikisha kile unachostahili unakipata kama inavyopaswa na kwa wakati
 
Wizi wa Kula na uchaguzi uliovurugwa matokeo yake ndio hayo. Umeandika Fyongo Njingi lakini Unashindwa kutambua ya Kwamba Uchaguzi haukufanyika na Kwamba wazungu waliiona ile dhuluma na wameamua kutusaidia sisis wanyonge. Wazungu wanatoa msaada na Mikopo kwa nchi inayojali utu.. Hii inchi imekuwa kama shurubu za kambale Kuumiza Dagaa...

Watawala wa kiafrica wanachoweza ni kuumiza watu wao
 
Back
Top Bottom