Hakuna amani kwa waovu na wasiotenda haki

Hakuna amani kwa waovu na wasiotenda haki

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,332
HAKUNA AMANI KWA WAOVU NA WASIOTENDA HAKI​

Tangu zamani za Biblia, watu walihimizwa KUTENDA HAKI ili wapate baraka na kibari kutoka kwa Mungu. AMANI huletwa na Mungu katika jamii au taifa na ni matokeo ya watu KUTENDA HAKI. Watu wakimuasi Mungu na KUACHA KUTENDA HAKI, Mungu huondoa AMANI katikati ya watu. Mungu akishaiondoa AMANI katikati ya watu, hakuna chombo, mamlaka wala Jeshi lo lote duniani ambalo linaweza kuilinda, kuitetea wala kuirejesha.

Mungu peke yake ndiye mtoa AMANI na ndiye mlinzi wa AMANI. Mungu akishaiondoa AMANI katikati ya watu, anaweza kuirejesha tena kama watu wa jamii au nchi husika wataacha UOVU na DHULUMA na kuanza KUTENDA HAKI.

AMANI katika nchi huimarishwa pale ambapo watu wake watajivika vazi la HAKI. Tukitaka kuona AMANI katika nchi wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu sisi sote tunahitaji KUTENDA na KUTETEA HAKI. Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi, Jeshi la Polisi, na Taasisi mbalimbali wakitenda HAKI kutakuwa na Utulivu na AMANI. Tuhimize watu KUTENDA HAKI ili tuone AMANI ikitawala katika nchi. Biblia inasisitiza kuwa HAKUNA AMANI kwa WATENDA MAOVU (Isaya 57:19b - 21)!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Usmsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Hahaha hawa watu wananichosha sana, maneno yao kama kwaya tu.

Tunahitaji kusimamisha uovu kwa vitendo siyo maneno na misamiati mizuri.
 
Back
Top Bottom