Hakuna ajuaye kesho jifunze katika hili ...

Hakuna ajuaye kesho jifunze katika hili ...

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Habari za majukumu waungwana!
Mimi si mpenzi wa mziki ila napenda kujifunza kupitia matukio . Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.
Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.
*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo. Rais wa zamani wa Zimbabwe *Robert Mugabe aliwahi kusema "heshimu kila mtu kama unavyoheshimu taulo lako. Kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio leo, kesho unaweza kuitumia kufutia uso."*

Hakuna chochote kwenye maisha yetu kinachodumu milele. Pia kumbuka hakuna tunu ya kujali wengine inayopotea bure. Jukumu la msingi la uhai tuliopewa na Mungu ni kusaidia wengine. Kwahiyo kama MUNGU amekujalia uwezo wa kifedha, au madaraka vitumie kusaidia wengine.

Na kama huwezi kuwasaidia basi usitumie cheo chako, pesa zako au madaraka yako kuwaumiza. Mahatma Ghandi aliwahi kusema kama huwezi kuwasaidia wengine basi angalau usiwaumize (If you cant help them, atleast do not hurt them).

Kila mtu atavuna alichopanda, kama unapanda ubaya utavuna ubaya; ukipanda wema kumbuka hauozi.
 
Watakaokuelewa in wasioamini ktk ndumba,wengi wangelewa mfano huo waafrica tusingeumizana wenyewe,maana adui Wa mwafrica in mwafrica mwenyewe
 
Kuna profesa alimwapia Dogo lazima takudisco tu sababu ya wivu Wa mapenzi dogo alikuwa akisoma business, akadisco kweli Dogo alishajua akajipanga upya akaenda kusoma udaktari chuo kingine akaajiriwa hospital kubwa ikapita Miaka mingi akaletewa mgonjwa mahututi Wa operations ajitambui,Dogo akamkumbuka akasema tajitahidi niwezavyo apone kweli profesa akapona akarudi kwenye fahamu zake Dogo akajitambulisha unanikumbuka Mimi ndo yule ulienidisco Chuo Fulani Lkn nilikusamehe japo ulisema hatma ya maisha yangu iko kwako ,kama Mimi ilivokuwa hatma ya uhai wako Uko kwangu.
 
In addition ..
Mike tyson aliwahi kumuajir Donald trump kama mshauri wake wa mambo ya kifedha lakini Leo trump ni rais wa nchi anayoish mike...
 
Kuna upande flani unaumiza zaidi.mtu anaumizwa na anayemuumiza anaendelea kuishi kwa amani wakati ambapo mtendwa anaomba aliyemuumiza apate malipo yake kwa baya hilo,ila ndo kwanza mtu mbaya anaendelea na yeye anazidi kuzama.
 
Kuna profesa alimwapia Dogo lazima takudisco tu sababu ya wivu Wa mapenzi dogo alikuwa akisoma business, akadisco kweli Dogo alishajua akajipanga upya akaenda kusoma udaktari chuo kingine akaajiriwa hospital kubwa ikapita Miaka mingi akaletewa mgonjwa mahututi Wa operations ajitambui,Dogo akamkumbuka akasema tajitahidi niwezavyo apone kweli profesa akapona akarudi kwenye fahamu zake Dogo akajitambulisha unanikumbuka Mimi ndo yule ulienidisco Chuo Fulani Lkn nilikusamehe japo ulisema hatma ya maisha yangu iko kwako ,kama Mimi ilivokuwa hatma ya uhai wako Uko kwangu.
Professor pengine alifanya kwa makusudi au hakukusudia ila alimdiscotisha Dogo ili akasome udaktari aje kunusuru maisha ya Professor.
Kwa lugha rahisi maisha ya professor yalikuwa mikonon mwa Dogo akiwa kama Dktari ni si kama mfanya biashara.
Sioni kosa kwa Professor hapa.
 
Ujumbe mzuri Sana. Lakini Bora wanaokukatisha tamaa maana utakuwa na ujasiri kusonga mbele, kuliko kutiwa moyo na wanafiki wanakufumaza kwenye kitu kimoja unasahau kuna maisha zaidi ya hapo ulipo.
 
Ujumbe mzuri Sana. Lakini Bora wanaokukatisha tamaa maana utakuwa na ujasiri kusonga mbele, kuliko kutiwa moyo na wanafiki wanakufumaza kwenye kitu kimoja unasahau kuna maisha zaidi ya hapo ulipo.
Inategemeana wanakukatishaje tamaa. Wakikuweka jera, au kuku-pyuupyu - hapo imekaaje? Jambo la muhimu hapa ni kuimizana tusitendeane mabaya kwa sababu kesho yetu hatuijui.
 
Professor pengine alifanya kwa makusudi au hakukusudia ila alimdiscotisha Dogo ili akasome udaktari aje kunusuru maisha ya Professor.
Kwa lugha rahisi maisha ya professor yalikuwa mikonon mwa Dogo akiwa kama Dktari ni si kama mfanya biashara.
Sioni kosa kwa Professor hapa.
Daima Mungu huwa anatumia njia ambazo kwa macho ya kibinadamu ni ngumu kujua kusudi la Mungu. Umechambua vyema mkuu.
 
Kuna profesa alimwapia Dogo lazima takudisco tu sababu ya wivu Wa mapenzi dogo alikuwa akisoma business, akadisco kweli Dogo alishajua akajipanga upya akaenda kusoma udaktari chuo kingine akaajiriwa hospital kubwa ikapita Miaka mingi akaletewa mgonjwa mahututi Wa operations ajitambui,Dogo akamkumbuka akasema tajitahidi niwezavyo apone kweli profesa akapona akarudi kwenye fahamu zake Dogo akajitambulisha unanikumbuka Mimi ndo yule ulienidisco Chuo Fulani Lkn nilikusamehe japo ulisema hatma ya maisha yangu iko kwako ,kama Mimi ilivokuwa hatma ya uhai wako Uko kwangu.
Mpango wa Mungu hauna makosa ... daima historia huwa zinajirudia.
Hata kwenye Biblia ndugu zake Yusuph walimtenda vibaya lakini huyo huyo ndo akaja kuwaokoa kipindi cha njaa.
 
Back
Top Bottom