Hakuna ajira kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna ajira kwa vijana

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Durasco hussein, Mar 24, 2012.

 1. D

  Durasco hussein New Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ajira,tenda kwa vijana sasa hivi hakuna kwa sababu mwananchi kama hakusoma hapati kazi na tujiulize je kwa wale wasiosoma inakuaje.Vijana ndio wanaotakiwa kuendeleza nchi yetu wanapokosa kazi serikalini hujiajili mwenyewe lakini atatakiwa alipe ushuru kwa mfano wauza maji,karanga nk ndio wanaopata vikwazo vingi serikali iangalie namna ya kuwaendeleza vijana.Vijana ndio taifa la kesho bila kuwezeshwa itakuwa kuitia hasara nchi ye2 ya Tz
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  HAYA NI MADHALA YA KUIMBA MABEPARI WALIA KUKATIWA MILIJA! walipotangaziwa Azimio la Arusha! Vijana wetu Hawakujua kabisa wanajitia kitanzi cha moto shingoni. Leo hii kule Nairobi wamejazana vijana wa kilombo wakiuza mitumba na kulala ktk nyumba mbovu kupita hata mabanda ya mbwa!

  Madhala ya kufuata siasa za ujamaa na kujitegemea ni mabaya kupita hata kuishi ktk nchi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ona sasa swala la ajira linavyotutesea vijana wetu! wabunge ndio kwanzaa wanataka kupandisha allowance zao huku 85% ya vijan hawana ajira za maana na hawana uhai. Naomba sana sana serikali imrudishie Lonho mali zake zote ikiwa pamoja na magazeti ya daily News.

  Ujumbe kwa vijana wetu: Usithubutu kumpatia kura mtu wa aina yeyote katika uchaguzi mkuu wa 2015 kama hajakuahidi kazi. Umchague mtu ambaye ankerwa na kero ya kutokuwa na ajira kwa vijana na aseme atafanya nini ili kupunguza daraja kubwa la watu wasio na kazi hapa nchini.
   
 3. J

  John Kangethe Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii topic imenigusa sana.
  Sisi vijana wengi Watanzania hatuna mbele wala nyuma. Ukitutazama vijana tulio wengi unatuhurumia na kutafakari ni lini maisha yatu yataboreka. Maisha mazuri kwetu yanabakia kuwa ni ndoto tu za kufikirika. Kwa wengi wetu inatupasa tujilaumu sisi wenyewe huenda hatukufanya jitihada zozote za ziada ili kuboresha maisha yetu, lakini kwa upande mwingine serikali nayo haikuonyesha jitihada zozote za kutusaidia ili tujikomboe kutoka umasikini huu unatumaliza.

  Mbali ya hayo, elimu bora ambayo ndiyo ingekuwa chanzo cha mitaji yetu tunaikosa, mitaji haipo, na hatima yake ni kufa maskini. Wengi wetu vijana siyo kwa sababu hatukutaka kusoma, ila ni kwa sababu wazazi wetu hawakuwa na vipato vya kutusomesha.

  Chukulia mfano mzuri hizi shule nyingi za kata zimeanzishwa miaka ya hivi karibuni tu. Kabla ya hapo hapakuwa na shule nyingi za kila mwanfunzi kupata nafasi ya kusoma sekondari, na ilikuwa vigumu sana kuchaguliwa kwenda secondary hasa sehemu za vijijini. Hata hivyo hizi shule za kata nazo ni majengo tu, hazina chochote, walimu hakuna, vifaa vya kusomea hakuna, vitabu hakuna, maabara hakuna, yaani ni shiada tu.

  Kibaya zaidi, ni kuona madini yetu yote yanatumika kujenga nchi za Ulaya, America, India, na China, wakati siye hapa Tanzania hatuna mbele wala nyuma.

  Swali ambalo nimekuwa nikijiulizaila kukicha!
  Hivi kweli sisi Watanzania tumeshindwa kabisa kuwachagua viongozi tunaowataka?, viongozi ambao watuletea mapinduzi ya kiuchumi!. Siyo kina Kikwete-style, na mafisadi wenzake. Sidhani kweli sisi wote watanzania tuko mambumbu kwa kiasi hiki wa kushindwa kutambua kuwa tunaibiwa na Benk kuu ya dunia wakishirikiana na kina JK na fisadi wake.

  Issue za kificha mikataba ya madini ndiyo tatizo kubwa la maisha magumu ya maisha ya kijana wa Tanzania. Tumenyonywa vya kutosha, imefika sasa tunasema imetosha. Wazazi wetu hawakuwa makini, lakini siye vijana imefika wakati sasa tuseme imetosha, tuamke na tupiganie maisha na uchumi wetu.

  Hebu angalia jinsi World Bank inavyotumaliza kuhusu mikataba ya madini:-

  World Bank Group (2011): “Increasingly, civil society and other stakeholders are requesting the disclosure of contracts that award companies the right to explore and develop extractive resources. Several countries have already adopted this approach, including Liberia, Timor-Leste, Guinea, Peru and others. As mentioned earlier in the report, IFC has decided under its revised Sustainability Framework, effective January 1, 2012, to also require its EI clients to publish relevant contracts”

  Mikataba ya madini ni haki yetu kuifahamu, na siyo issue ya kuiomba. World Bank inatuambia tu-request. World Bank inapaswa itambue kuwa mikataba yote ifahamike kwa Watanzania, kwa sababu madini haya yote ni yetu. Hii Benki ya dunia inaficha mikataba kwa sababu inashirikiana na mafisadi Watanzania kupora madini yetu. Na hapa ndipo ugumu wa maisha kwa vijana unapoanzia.

  Itafika siku mie nitashika mtutu wa bunduki, ili litakalokuwa na liwe!
   
Loading...