Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,018
- 144,375
Changamoto kubwa itakayoikabili Aviation Industry hapa nchini kwa sasa ni uchache wa abiria utakaosababishwa na mambo kadhaa nitakayoyaanisha hapa chini kulingana na mtazamo wangu huku mashirika ya ndege yakiendelea kuongezeka kila kukicha.
Sababu ni hizi:
Utamaduni wa mtanzania
Watanzania wengi bado wanakasumba ya kishamba sana na ya kizamani kuwa usafiri wa ndege ni anasa na ni usafiri wa watu matajiri tu.
Leo hii mwananchi wa kawaida mwenye kipato cha wastani ukikata ticket ya ndege kutoka Tabora kwenda Dar watu hawakuelewi na wataanza kuulizana hivi huyu hata kiwanja anacho,wengine watasema unapanda ndege wakati unaishi nyumba ya kupanga,n.k
Hata vigogo wa serikali wengi ukiona wamepanda ndege basi ujue hiyo ni safari ya kikazi lakini safari binafsi atachukua basi na wengine hata mabasi ya bei chee na sio luxury.
Wakati mwingine hata mtu akichukua likizo na akaamua kupanda ndege kuelekea mikoa ya pembezoni kusalimia ndugu na jamaa kijijina kwao basi hufanya hata siri maana ndugu/wazazi hawatamuelewa na badala yake watamuona anafanya anasa kwa kupoteza fedha ambazo angeweza kusaidia wazazi au ndugu zake huko kijijini aendako.
Serikali kubana matumizi
Hivi sasa serikali imeamua kubana matumizi kiasi cha kupunguza OC katika Mashirika na Taasisi nyingi za serikali.
Athari ya sera hii ya kubana matumizi kwa biashara ya usafiri wa anga hapa nchini ni kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watumishi wa serikali waliokuwa wanapanda ndege kwa safari za kikazi za ndani ya nchi.
Kwa mfano,siku za nyuma CEO wa Taasisi ya umma yeye na maafisa wake kadha walikuwa wakikata ticket za ATCL kwenda mikoani kuhudhuria maafali katika chuo kinachoendeshwa na taasisi anayoingoza,kufanya uzinduzi,kukagua utendaji kazi mikoani n.k. Hivi sasa wengi bila shaka wanalazimika kutumia magari ya ofisi au hata public transport.
Kipato kidogo cha watanzania
Watanzania wengi ni watu wa kipato cha chini huku wakikabiliwa na majukumu mengi ya kimaisha kiasi kwamba unaweza ukaweka nauli ndogo ila bado wengi wakashindwa kumudu gharama hizo.
Kwa mfano,hata ukiweka nauli ya ndege ya sh 50,000 kwa safari ya Dar-Dodoma wakati kuna Shabiby ya sh 20,000 wengi hutwaona sio kama hawapendi ila tatizo uchumi hauruhusu na huko anakokwenda bado kuna gharama zinamsubiri.
Hivyo kwa hali hii,hata ukishusha nauli bado itakuwa ni vigumu kupata abiria wa kutosha kujaza ndege za mashirika matatu au zaidi kwasababu abiria hao wa kuwavutia nao ni wachache ukilinganisha na mashirika yaliyopo na bei ikishushwa kuputs kiasi hiyo tena haitakuwa biahara bali ni kua mashirika haya.
Viwanja vichache vya ndege vilivyopo
Hili nalo ni tatizo lingine ambalo litajikozea iwapo ushindani wa biashara ya ndege utaongezeka hapa nchini.
Hii ni kwasababu,viwanja vichache vya ndege maana yake ni kuwa, destination zitakuwa chache huku mashirika ya ndege yakiongezeka na hivyo mwisho wa siku mashirika haya yatajikuta yana tatizo la kuwa na destinations zisizowatosheleza kufanya biashara kwa mafanikio na kwa ushindani wenye afya maana bila destination za kutosha tafsiri yake ni kwamba hakuna biashara.
Ubovu wa baadhi ya viwanja
Ubovu wa baadhi ya viwanja nako kutachangia baadhi ya mashirija kushindwa kupeleka ndege zao katika baadhi ya mikoa/maeneo na hivyo kuyafanya mashirika haya kutegemea viwanja vichache vilivyopo kuendesha biashara hii jambo ambalo si zuri kibiashara kwao kwani watakuwa na viwanja vichache vya kufanya biashara ili hali mashirika yanaongezeka.
Shughuli chache za kiuchumi,kijamii na kibiashara mikoani
Uwepo wa shughuli za kiuchumi, kijamii na kibiashara kama vile mikutano, washa, makongamona ,mikutano ya wasomi na wataalamu mbalimbali,miradi mikubwa ya kimaendeleo, n.k, huweza kuchangia kupatikana kwa abiria wanaosafiri kwa ajili ya kwenda kufanya au kuhudhuria shughuli za aina hii sehemu mbalimbali za nchi..
Sasa kwa nchi yetu shughuli za aina hii mara nyingi hufanyika katika mikoa ya Dar-es-salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar tu huku serikali nayo ikipiga marufuku shughuli za aina hii kwa watumishi wake.
Kuendelea Kuimarika kwa mtandao wa barabara nchini
Serikali imejitahidi sana kuboresha mtandao wa barabara hasa zile zinazounganisha mikoa na juhudi hizi bado zinaendelea kuwezesha mikoa yote nchi kuunganishwa kwa barabara za kiwango cha lami jambo ambalo ni jema na la kupongeza.
Kutokana na serikalikali kuendelea kuboresha barabara zinazounganisha mikoa,baadhi ya watu waliokuwa wakipanda ndege kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kwenye barabara mbovu hawatakuwa tena na sababu ya kufanya hivyo.
Kwa mfano, safari ya kutoka Dar-es-Salaam kwenda Kigoma kwa barabara ilikuwa ni adhabu tosha kiasi kwamba ukisafiri mara moja, mara ya pili kama una uwezo wa kupanda ndege utaona ni bora usafiri kwa ndege kuepuka adha ya vumbi, kurushwarushwa na safari ya masaa mengi katika mazingira magumu.
Binafsi nilisafiri na basi la Adventure mwaka 2008 kutoka Dar-es-salaam kwenda Kigoma na ninachokiongea hapa nimeki-experience.Hata hivyo, ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ulikuwa unaendelea katika baadhi ya maeneo ingawa sijui kwa sasa ujenzi umekamilika kwa kiwango gani.
Ujenzi wa Reli ya kisasa
Kama serikali itafanikiwa kujenga reli ya kisasa kama inavyokusudia na hivyo tukawa na mtandao mzuri, bora na wa kisasa wa reli,hakika watu wengi watatumia usafiri wa train ambao ni usafiri wa gharama nafuu zaidi kulinganisha na usafiri wa basi na ule wa ndege.
Watu wengi wenye kipato cha kati watasafiri kwa reli badala ya ndege kwa safari za kwenda na kurudi kati ya Dar-es-Salaam na Tabora,Tabora na Kigoma na Dar-es-Salaam mpaka Kigoma.
Kuboreka kwa mtandao wa reli kwa kujenga reli ya kisasa itakuwa ni tishio kubwa kwa Aviation Industry hapa nchini kwa siku zijazo.
Kwa kuzingatia changamoto hizo hapo juu, ukweki ni kuwa, itakuwa ni vigumu kwa mashirika matatu au zaidi ya ndege ku-operate hapa nchini na yote yakajiendesha kwa faida katika mazingira haya.
Vile vile, iwapo mashirika binafsi ya ndege nayo yataamua kushusha zaidi nauli au kuleta ndege ambazo nazo zitatumia mafuta kidogo, sitashangaa wakati ukafika seriali ikajikuta inalazimika kutoa fedha na kuikopesha ATCL ili imudu ushindani.
Tunaweza kuwa na ushindani lakini sioni uwezekano wa kuwa na ushindani wenye afya katika biashara ya ndege kwa safari za ndani hapa nchini.
Kuna baadhi ya mashirika yatalazimika kujitoa na mengine yatalazimika kuangalia safari za nje ya nchi kama yatataka kubakia katika hii biashara.
Wengi kwa sasa hamtanielewa ila muda ndio utaongea.