Bila Shaka wote Mpo salama!
Serikali ilifanya kosa la kiufundi kumkamata Tundu Lisu kwa Makosa ambayo kwa jicho la kawaida tuu unaweza kuona ni ishu ya kisiasa.
Ati Lisu mhaini. mwanasheria msomi kama Lisu ati atangaze waziwazi kufanya uhaini mbele ya camera. Kweli!
Tukio la Lisu kupigwa Risasi miaka Ile lilimuweka karibu zaidi na mabeberu. Lilimuongezea nguvu na connection na viongozi wa magharibi.
Kwa harakaharaka nguvu za Lisu zipo nje ya nchi kuliko ndani. Kama lengo la serikali lilikuwa kumpunguza makali Tundu Lisu basi hatua waliyochukua dhidi yake haikuwa hatua sahihi.
Hatua yoyote ya kumdhibiti Lisu ilipaswa izingatie nguvu ya Lisu IPO wapi. Nani wanamsapoti Lisu.
Je watu hao wanaathari yoyote kwenye uchumi na usalama wa taifa letu kwa kiwango kipi?
Je hatua tutakazozichukua zinaathari gani na kwa muda gani katika taifa?
Je Lisu mwenyewe ataathirika vipi Kwa hatua ambazo tutamchukulia?
Ni Jambo gani Lisu analiogopa ambalo hataki adui zake walifahamu?
Nini kitadhorotesha na kumkatisha tamaa Tundu Lisu?
Ni mtu gani ndani ya taifa hili yupo karibu na Lisu ambaye tukimshawishi akawa upande wetu tutakuwa tumemaliza sehemi muhimu ya nguvu za Lisu?
Ni wapi Lisu anapata ushauri wenye tija anaoutegemea katika harakati zake?
Hapakuwa na haja ya kumweka mahabusu Lisu Kwa makosa yanayomuongezea sifa na CV katika Harakati zake.
Kwa kiwango alichofikia Lisu sio wa kushughulika naye kienyeji na kijingajinga kama unashughulika na watu wa kawaida.
Sayansi ya siasa hapo ndio sehemu Yake.
Tena kwa mazingira ya nchi yetu na watu wake. Hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu kubwa kukabiliana naye.
Kuna watu unaweza kuwatumia kutisha wengine lakini kwa level ya Lisu sio miongoni mwa watu hao.
Ni sawa na shambulizi la Father Kitima halikuwa sahihi kabisa.
Ni shambulizi lisilo na tija. Zaidi linaleta athari mbaya zaidi kwa upande wa serikali.
Moja ya mbinu za kudili na watu Aina ya Lisu na kumkatisha tamaa ni pamoja na;
1. Kujifanya unamsapoti kwa kumpa nafasi ya kufanya kile anachotaka ili aone vile anavyojiona sivyo watu wanavyomchukulia.
Akitangaza mikutano yake serikali itoe sapoti ya ulinzi wa polisi.
Lakini wakati huo serikali iwe imeandaa watu katika Nyanja kadhaa za kukabiliana naye kwa akili na viroja.
Wale vijana wa serikali wenye hulka ya Tundu Lisu nao wangeingizwa mchezoni lakini wao wawe upande wa serikali.
Unapomzuia mtu au kitu unakipa thamani.
Hakukuwa na haja ya kutumia mabavu.
2. Kuchochea migogoro ya ndani ya chama alichopo Lisu.
Hii naona serikali inafanya vizuri.
Hakukuwa na haja ya kumfunga Lisu wakati ungeweza kuwatumia watu wake mwenyewe kukabiliana naye.
Kila mtu anabei yake hilo linajulikana. Ambao hawanabei mara nyingi sio wanasiasa. Na kama ni mwanasiasa asiye na bei huyo ni exceptional na wapo wachache Sana
Mtu akishafika bei hakuna haja ya yeye kuhama chama hasa mtu huyo mkimuona anauwezo mkubwa wa kutoshana na Lisu. Sio mchukue mtu ilimradi tuu kisa anajina kubwa, wengine majina makubwa sio kwa uwezo wao Bali wamebebwabebwa, au kupromotiwa na chama.
Watu wenye uwezo mkubwa wanasifa zap. Kwanza ni smart, lakini kwenye fani zao ni wataalamu kwa kiwango cha juu. Kama ni mchumi ni mchumi haswa. Kama ni daktari ni Yule aliyebobea, kama ni Mwalimu ni wale waliopata ufaulu usio na mashaka. Sio unachukua mtu kisa anabororoja zaidi ya hapo hanaajualo.
Watu aina ya Lisu lazima uwatafutie watu wenye uwezo kama wao na sifa za ziada.
3. Kama lengo ni kuzuia agenda ya No reforms no election. Serikali ingewaambia wapinzani hasa hao chadema akiwepo Lisu kuwa mchakato utakuwa wa Uhuru na haki katika kuunda tume huru ya uchaguzi.
Kamati au tume Fulani itakayohusisha vyama vya upinzani ingeundwa. Kisha kwenye tume hiyo wakati wa mkutano wa Kwanza, ingeletwa hoja ya kuwa muda umeenda kufikia uchaguzi mkuu. Hivyo mchakato uwe mwakani.
Hapo yangezuka makundi mawili lakini tayari serikali kwa Siri ilikuwa na mpango. Kura zipigwe kwa wanaotaka tume kabla ya uchaguzi na wale wanaotaka tume huru mwakani. Kura zinapigwa zinahesabiwa serikali ilishaandaa watu wa kuhakikisha mchakato wa tume huru ufanyike mwakani. Hivyo itashinda.
Ikifika mwakani mipango mingine itaendelea vivyohivyo.
Na sio kukimbizana na watu kwa kutumia nguvu kubwa
4. Kuruhusu midahalo ambayo Lisu anaitaka lakini kuhakikisha miongoni mwa watu wake wanampinga kwenye huohuo mdahalo. Yaani wanakuwa kinyume.
Isiwe ya kuonekana imepangwa, watu wake mkishawaweka sawa. Wakati wa mdahalo waongee kwa akili kanakwamba wapo na lisu lakini hoja zao ziwe zinakinzana au kuleta utata kwa wasikilizaji.
Upande wa serikali wachague mtu mwerevu, mahiri, mwenye kujua mambo mengi, lakini ajuaye kuzungumza. Asiingilie ugomvi baina ya chadema wakati wa mdahalo kazi hiyo aifanye mtangazaji. Yeye atakuwa anachomekea kidogokidogo kuchochea Moto na kuonyesha nyufa za upande wa pili.
Kisha mwisho mtu wa Lisu abaki kumsapoti Lisu na aendelee kuiponda serikali kwa nguvu zote.
Kesho yake vyombo vya habari, influencer WA mitandaoni waendelee na KAZI yao kuonyesha madhaifu yaliyojitokeza kwenye mdahalo.
Hakikisheni influencers watakaojadili ishu ngumu za Lisu wawe wamebobea kwenye masuala ya kisiasa na kijamii. Wakitoa hoja ziwe zinaeleweka.
5. Watu kama kina Kitima sio wakuwashambulia kwani huko ni kuongeza maadui na kuitanua vita. Ni kumpa nguvu Tundu Lisu.
Watu aina ya kitima ni kutafuta eneo lao lenye udhaifu ambalo mtaweza kulitumia kuwanyamazisha.
Hakuna mtu asiye na udhaifu Fulani. Hakuna MTU asiye na Jambo analolificha watu wasilijue.
Utakapolijua Jambo Hilo basi umemmaliza nguvu MTU husika.
Kama umeshindwa kulipata Jambo Hilo ingawaje lazima liwepo. Basi mtengenezee Jambo la aibu mwenyewe kwaakili. Kisha mdhibiti.
Kwenye michezo ya siasa hilo ni muhimu kuliko kushambulia, kuteka au kuua.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam