Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,108
- 34,933
HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo Misungwi mkoani Mwanza, Restuta Kamani (40) pamoja na karani wa Mahakama hiyo Scholastica John (40), wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi Milion 60 Ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Msafiri Henga wa Ofisi ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mbele ya Hakimu Angelo Lumisha kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Oktoba 7, mwaka 2007.
Henga alidai kuwa waliomba na kupokea rushwa hiyo ili wapindishe ukweli wa kesi namba 163 ya mwaka 2004, iliyohusu mirathi ya nyumba iliyokuwa ikiombwa na moja ya familia iliyoko maeneo la Capri-point.
Ilidai kuwa wakiwa kazini watuhumiwa hao walirubuni na kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye familia hiyo kwa lengo la kupindisha mirathi kutoka familia hiyo.
Hata hivyo washtakiwa hao wote walikana mashtaka, na wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti, ambapo walitakiwa wadhamini wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya sh milioni 20 kila mmoja.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 22 itakapotajwa tena.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa hakimu aliyepangiwa kesi hiyo alijitoa kusikiliza kesi hiyo kwa lengo la kumpisha hakimu mwingine aendelee na kesi hiyo ili haki itendeke . http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2984546&&Cat=1