Hakimu Kesi ya Liyumba ajitoa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakimu Kesi ya Liyumba ajitoa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanajamiiOne, Mar 13, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Source: Michuzi blog
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Alitakiwa kufanya hivyo siku nyingi baada ya kuchemsha wakati alipotoa dhamani hovyo hovyo. Amechelewa sana, lakini walau amegutuka kuwa haweza kuendelea na hiyo kesi baada kuonesha upoe mdogo wa kushughulikia kesi kubwa. Isijekuwa ameshinikizwa na wakubwa wake!!
   
 3. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa aliniambia kuwa huyu hakimu anahisiwa kupewa mlungula na washirika wa Liyumba akapokea,sasa baada ya kuiona kesi yenyewe imekaa vibaya akaamua kulazimisha dhamana ili awe ameshaplay part yake,ila kwa imani kwamba upande wamashtaka ungekata rufaa.Kulingana na source ya jamaa,inasemekana hakimu huyu ameshafunguliwa faili takukuru anachunguzwa.Na inawezekana kujitoa huku kukawa ni shinikizo ili apishe watu wafanye kazi ya kumchunhguza vizuri,ebu tusubiri tusikie.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Eboo! alikuwa bado tu????
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  BREKING NYUUZZZZZZZ:AHAKIMU WA KESI YA LIYUMBA AOMBA KUJITOA
  MH. HADIJA MSONGO, HAKIMU ANAYESIKILIZA KESI YA KINA LIYUMBA NA WENZIE, LEO AMEEKLEZA NIA YAKE YA KUTAKA KUJITOA KUISIKILIZA KWA KILE ALICHOTAJA KUWA MWENENDO TATA WA KESI HIYO.

  PAMOJA NA MAMBO MENGINE MH. HADIJA MSONGO AMESEMA MWENENDO WA KESI HIYO UMEKUWA TATA HASA BAADA YA YEYE KUTOA DHAMANA KWA MSHTAKIWA LIYUMBA HATA BAADA YA KUPEWA PASI ILIYOISHA MUDA WAKE, NA BAADA YA KUTOA AMRI YA KUFUTA DHAMANA YA LIYUMBA BAADA YA KUBAINIKA KWAMBA PASIPOTI ALIYOTOA HAIKUWA ILIYOTAKIWA KUTOLEWA.

  AMESEMA MALALAMIKO YA WANANCHI PAMOJA NA JAMHURI (SERIKALI) KUPITIA VYOMBO VYA HABARI VIMEIFANYA KESI HIYO KUONEKANA INA UTATA NA KUONEKANA KAMA VILE HAKI HAITENDEKI.

  HIVYO KAAMUA KUCHOMA NA TAYARI KESHAMWANDIKIA BOSI WAKE HAKIMU MKUU MKAZI MFADWIDHI MAHAKAMA YA KISUTU, MH. ADDY LYAMUYA, KUMOWMBA AMPANGIE HAKIMU MWINGINE KUSIKILIZA KESI HIYO.


  source: issamichuzi.blodspot.com
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Pole mzee kijana Amandus Liyumba. Ni mpole sana kule Keko. Ila naamini kwa muda atakao kuwa huko Keko kutamsaidia aondokane na adiction ya ngono.
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dark City yeye amesema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kuona maamuzi yake ya mwanzo yameleta utata kwa wananchi anahofia wasijesema kuwa haki haikutendeka.
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wakitoka nje, sisi tutawahukumu sisi wenyewe kwa mikono yetu.. kama selikali imeshindwa, tufanye nini sasa?
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Hakimu ajitoa kesi ya EPA
  Neema Mgonja
  Daily News; Friday,March 13, 2009 @19:00

  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam, Hadija Msongo, amejitoa kusikiliza kesi dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.

  Kesi hiyo pia inamhusisha aliyekuwa Meneja Miradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka, wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka waliyokuwa nayo na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha. Akizungumzia sababu za kujitoa jana, Msongo alidai ni baada ya kuona mwenendo wa kesi hiyo na amri alizokuwa akizitoa kulalamikiwa na upande wa mashitaka na wananchi kupitia vyombo vya habari.

  Msongo alisema malalamiko hayo yalianza kutolewa baada ya mahakama hiyo kutoa dhamana kwa Liyumba Februari 17 mwaka huu, baada ya mshitakiwa kuwasilisha mahakamani hapo hati za mali zenye thamani ya Sh milioni 55, jambo lililoifanya mahakama kuahidi kuzihakiki huku mshitakiwa akiwa nje kwa dhamana.

  Aliongeza kuwa siku moja baada ya dhamana kutolewa, mahakama ilitoa hati ya kumkamata mshitakiwa na wadhamini wake, baada ya kugundua kuwa taarifa zilizotolewa na mshitakiwa huyo, zilikuwa za uongo, hasa kuhusu hati ya kusafiria, kwa sababu mahakama ilipokea hati nyingine iliyoletwa na mtu aliyejitambulisha kuwa mtoto wa mshitakiwa huyo, ambayo haikuwa imemaliza muda wake. Alisema baada ya mahakama kutoa hati ya kukamatwa, mshitakiwa huyo alijitokeza Februari 24 mwaka huu na akakamatwa.

  Kutokana na matukio hayo yote, Msongo alisema amekuwa akisikia malalamiko kwamba dhamana hiyo ilikuwa na utata, hivyo anajitoa kusikiliza kesi hiyo ili isikilizwe na hakimu mwingine na haki iweze kutendeka. Aliongeza kuwa atarudisha jalada la kesi hiyo kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Addy Lyamuya, ili aweze kumpangia hakimu mwingine atakayesikiliza kesi hiyo na kutoa amri stahiki.

  Kwa uamuzi huo, upande wa utetezi uliokuwa na Wakili Edison Ndusyepo, uliiomba mahakama kupeleka jalada la kesi hiyo kwa Hakimu Lyamuya jana, ili waweze kufanya majadiliano kuhusu mwenendo wa kesi hiyo. Akijibu ombi hilo, Msongo alisema jalada litapelekwa mapema, ili liweze kushughulikiwa.

  Kesi hiyo ambayo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa maombi yaliyotolewa awali na upande wa utetezi, iliahirishwa hadi Machi 20 mwaka huu, itakapotajwa na kufahamika hakimu atakayekuwa amepangiwa kuisikiliza. Awali, upande wa utetezi uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kufutwa baadhi ya mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao, maombi yaliyopangwa kusikilizwa jana kama hakimu asingejitoa.

  Liyumba na Kweka wanakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 200, wakidaiwa kushindwa kutumia busara na kufuata maadili ya kazi zao na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni hayo ya fedha kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

  Hadi jana Liyumba aliendelea kusota rumande tangu mahakama hiyo imfutie dhamana aliyopewa awali, huku Kweka akiendelea pia kukaa rumande kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa alipofikishwa kwa mara ya kwanza Januari 29, mwaka huu kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
   
 10. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tatizo kwenye hizi kesi za epa, waandishi wa habari wamekuwa kama wao ndo mahakimu, huku wakiwa-feeed wananchi taarifa zinazokinzana, ni vema kuwepo na waandishi wa habari wenye taaluma angalu certificate in law, kujiondoa kwa hakimu huyu si dalili nzuri sana kwenye utawala wa sheria
   
Loading...